Nimepata accident mapema asubuhi ya leo

Nimepata accident mapema asubuhi ya leo

Hiyo ni gari ya zamani sana, ni ya mtumba imetumika zaidi ya miaka 10 huko ulikonunua.
 
Nimepata ajali baada ya kumkwepa bodaboda nikakosa muelekeo nikagonga mti uliokuwa pemben ya barabara.
Mafundi naomben makisio ya gharama ya kutengeneza hii gari, Taa mbili za upande wa kulia (juu na chini)zote zimepasuka, air cleaner box limepasuka, bonet imebonyea na kioo cha mbele kimeweka crake. Gari ni Toyota crown Athlete.

View attachment 2122685

View attachment 2122686
Hapo issue ambazo ni pasua kichwa naona ni mbili,Taa na hiyo Bumper,labda kama sioni vizuri ,hilo Bumper naona kama limekatika,hapo kuna mawili liungwe ambapo halitarudisha gari kwenye ubora wake au ununue jipya,taa pia lazima ujipange sidhani kama itakuwa chini ya laki 3,Aircleaner box hiyo inapatikana sio issue sana,huko kwingine ukimpata fundi body mzuri atakunyooshea na kukupigia rangi litakaa vizuri tu...
 
Kwa misingi ya imani zetu kifo utokea kwa ahadi kitendo cha mimi kumkwepa na kugonga mti ata mm ahadi yangu haikuwa imefika. Tahadhari ya kunusuru uhai wake na wangu ndio imepekea mm kutoka nje ya barabara na kugonga mti, uhamuzi wa kutoka nje ya barabara pasipo kukusudia (kwa ishara) nao ulikuwa hatari kwa maisha ya watumiaji wengine wa barabara

Ni kweli lakini ni muhimu kuheshimu haki ya watu wengine kuishi kuna makusudi ya kusema bodaboda unagonga tu si sawa wale ni binadamu wenzetu wana haki ya kuishi,wana familia zao na maisha yao kwanza sio wote japo wengi wao wapo rough.

Kwa principle wanazoshauri hao basi ukiendesha gari kwa miaka 25. utakuwa umeua bodaboda hata 5-10.Sasa kuna faida gani kuua watu? Mwisho wa siku ni kuishi maisha ya majuto tu.
 
Wewe umeweza kununua gari, unakuja huku kuuliza bei ya taa?
Hivi nyie watu mna matatizo gani? Kwahio ukinunua gari ndio unajua kila kitu kuhusu gari? Mnajua dhumuni la kuwekwa jukwaa hili? Hili jukwaa halikuwepo,tumeomba mods muda Sana hadi wakalianzisha ili tusaidiane kwenye changamoto za magari. Wengine hawana muda wa kuhamgaika na magari zaidi ya kuendesha. Kuhusu spare na ufundi wanapata uzoefu Kwa wengine.
 
Naona watu wanawaongelea boda boda oama wanyama hivi na sio binadamu kama wao

Ingawa ni kweli boda boda wengu hawajali usalama barabarani wanafujo sana
Ukiishi kwa Upanga utaondoka Kwa Upanga! Unawajua bodaboda wewe? Hawa wanaogonga watoto service road halafu wanakimbia? Hawa wanaogonga magari ya watu hovyo kwenye foleni halafu wanakimbia huku wanakutukana? Hawa wanaongusha abiria halafu wanakimbia? Siwezi kuingia mtaroni au bondeni kisa bodaboda mpumbavu ataingia yeye. Kama yeye hathamini uhai wake why should I? Acheni sugar coating.
 
Kusema ukweli boada boda ninawachukia....hala akishagonga mtu kwenye zebra, anakimbia anajichanganya kwenye kijiwe cha wenzake...anasikilizia kama kuna noma...

Kama kuna mazingira yasiyo na ushahidi, boda boda ni wakusukumia tu mtaroni
Sikuhizi ukiwa una-drive unakuwa na woga na wasiwasi WA kusababishiwa ajali na bodaboda hawa watu ni wasumbufu Sana, madereva wengi WA magari ni wastaarabu kidogo Ila hawa wenzetu ni kama kuku Akili zao
 
Ni kweli lakini ni muhimu kuheshimu haki ya watu wengine kuishi kuna makusudi ya kusema bodaboda unagonga tu si sawa wale ni binadamu wenzetu wana haki ya kuishi,wana familia zao na maisha yao kwanza sio wote japo wengi wao wapo rough.

Kwa principle wanazoshauri hao basi ukiendesha gari kwa miaka 25. utakuwa umeua bodaboda hata 5-10.Sasa kuna faida gani kuua watu? Mwisho wa siku ni kuishi maisha ya majuto tu.
Kwa hiyo hayo maisha yao uwalinde wewe na wao hawajilindi?

Ukiona watu wanakuongelea vibaya jua tu unashida mahala na hufai.
 
Kuna siku hizi dual carriageway tumesimama mtu avuke, wakati anavuka bodaboda inakuja mbio kutoka wrong side basi mimi naiona jinsi inavyoenda kumgonga mtu tuliemruhusu avuke aisee nilipiga honi yule mtembea kwa miguu akawa ananishangaa huyu ana kichaa nini, basi kule kushangaa kwake sekunde kadhaa ndio ile boda ikapita alinishukuru sana yule mtu ndio akaelewa kwanini nilikuwa napiga honi! Bodaboda ni janga halafu polisi ni kama wamekubali wamewashindwa!
Wapiga KURA hao hakuna wakuwagusa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom