Nimepata accident mapema asubuhi ya leo

Hiyo ni gari ya zamani sana, ni ya mtumba imetumika zaidi ya miaka 10 huko ulikonunua.
 
Hapo issue ambazo ni pasua kichwa naona ni mbili,Taa na hiyo Bumper,labda kama sioni vizuri ,hilo Bumper naona kama limekatika,hapo kuna mawili liungwe ambapo halitarudisha gari kwenye ubora wake au ununue jipya,taa pia lazima ujipange sidhani kama itakuwa chini ya laki 3,Aircleaner box hiyo inapatikana sio issue sana,huko kwingine ukimpata fundi body mzuri atakunyooshea na kukupigia rangi litakaa vizuri tu...
 

Ni kweli lakini ni muhimu kuheshimu haki ya watu wengine kuishi kuna makusudi ya kusema bodaboda unagonga tu si sawa wale ni binadamu wenzetu wana haki ya kuishi,wana familia zao na maisha yao kwanza sio wote japo wengi wao wapo rough.

Kwa principle wanazoshauri hao basi ukiendesha gari kwa miaka 25. utakuwa umeua bodaboda hata 5-10.Sasa kuna faida gani kuua watu? Mwisho wa siku ni kuishi maisha ya majuto tu.
 
Wewe umeweza kununua gari, unakuja huku kuuliza bei ya taa?
Hivi nyie watu mna matatizo gani? Kwahio ukinunua gari ndio unajua kila kitu kuhusu gari? Mnajua dhumuni la kuwekwa jukwaa hili? Hili jukwaa halikuwepo,tumeomba mods muda Sana hadi wakalianzisha ili tusaidiane kwenye changamoto za magari. Wengine hawana muda wa kuhamgaika na magari zaidi ya kuendesha. Kuhusu spare na ufundi wanapata uzoefu Kwa wengine.
 
Naona watu wanawaongelea boda boda oama wanyama hivi na sio binadamu kama wao

Ingawa ni kweli boda boda wengu hawajali usalama barabarani wanafujo sana
Ukiishi kwa Upanga utaondoka Kwa Upanga! Unawajua bodaboda wewe? Hawa wanaogonga watoto service road halafu wanakimbia? Hawa wanaogonga magari ya watu hovyo kwenye foleni halafu wanakimbia huku wanakutukana? Hawa wanaongusha abiria halafu wanakimbia? Siwezi kuingia mtaroni au bondeni kisa bodaboda mpumbavu ataingia yeye. Kama yeye hathamini uhai wake why should I? Acheni sugar coating.
 
Kusema ukweli boada boda ninawachukia....hala akishagonga mtu kwenye zebra, anakimbia anajichanganya kwenye kijiwe cha wenzake...anasikilizia kama kuna noma...

Kama kuna mazingira yasiyo na ushahidi, boda boda ni wakusukumia tu mtaroni
Sikuhizi ukiwa una-drive unakuwa na woga na wasiwasi WA kusababishiwa ajali na bodaboda hawa watu ni wasumbufu Sana, madereva wengi WA magari ni wastaarabu kidogo Ila hawa wenzetu ni kama kuku Akili zao
 
Kwa hiyo hayo maisha yao uwalinde wewe na wao hawajilindi?

Ukiona watu wanakuongelea vibaya jua tu unashida mahala na hufai.
 
Wapiga KURA hao hakuna wakuwagusa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…