Suala la kuolewa Tanzania liko overrated [emoji1783]
Ndiyo na mimi nashangaa bidada anaanzisha uzi baada ya uzi kwenye maada hii, kama yupo obsessed vile.
Yani kuolewa kunakuwa kama Nobel prize.
I am like, what's going on here?
Tuna tatizo hili au tunajitengenezea anxiety tu?
Lakini, dada mkubwa ujue mwanamke mmoja anaweza kuwa amesimama vizuri, ana kazi/ biashara nzuri, amesoma vizuri, ana family support structure nzuri, watu wa familia yake wamesoma vizuri, wamesafiri sehemu mbalimbali duniani na kuona watu tofauti wanavyoishi, hawana pressure za kibongo za kutaka mtu aolewe.
Kwa mwanamke kama huyo, anaweza kusema suala la kuolewa Tanzania liko overrated, na akawa sahihi.
Sasa, hapo hapo umkute mwenzangunamie Maimuna pangu pakavu tia mchuzi, hana elimu, hana family support, tena inawezekana yeye ndiye anaangaliwa na family kutoa support, hana kazi/biashara, hana ujanja wowote zaidi ya kudanga.
Huyo ukimwambia suala la kuolewa Tanzania liko overrated atakuona wewe mchawi, mnaweza kupigana.