Nimepata mgeni yuko rafu sana

Safi sana. Ukicheza na mbwa atakufuata mpaka msikitini. Wengine wangekuja hapa JF kuulizia wafanyeje?
 
Dawa hata unapoanza mara ya 1 unatakiwa uanze kuminya chini. Haiminywi kuanzia juu. Kama ulikua hujui chukua hiyo usije kutoa boko ugenini.
Issue sio kutoa Boko au kutotoa boko, kwanza most of the time kati ya vitu ninavyopack nikiwa safari ni pamoja na dawa ya meno

Ninachojaribu kusema Mimi ni kwamba, mgeni akiminya kuanzia juu au chini, sioni kama ni issue kubwa sana, inavumilika.

Labda nikuulize, ukiachana na shape/muonekano wa hiyo dawa, ni yapi madhara yatokanayo na kubinya dawa tokea kati?
 
Wew ulibahatika kufunzwa na mama yako namna ya kuminya dawa, so utamlaumu vp yeye ambae hakufunzwa juu ya huo ustaarabu.
na unategemea kila kitu utafunzwa kwenye haya maisha..?
Nini maana ya kuishi na watu na kujifunza...?? Mbona vingine hatujafunzwa tumekuja kuona kwa watu tukaona ni kitu chema tukakibeba..?
 
Dawa mnunulie yake,

Hafu mendine muelekeze atarekebika.
 
= glass

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Wakati mwingine tukubali tu

Kuna watu wamekulia mazingira ambayo hakuna utaratibu wa kurudisha kitu chochote ulichotumia mahali pake.

Yaani maisha yao hayana mpangilio.

Usimlaumu, we akienda kinyume na utaratibu wako wewe rekebisha.

Malezi hayo
Nakubaliana na maneno yako. Malezi yna-play part kubwa. Pia kuna watu kwa asili wako rafu tu. Yaani hawajishtukii. Unakuta mtu anaingia chooni, (hivi vya kuvuta) ''anapiga baruti'' paa, anachafua choo na mfuniko wake kwa ''cheche za kinyesi'' na kuacha hivyo hivyo hivyo. Yaani yeye akishavuta kinyesi kikienda ni basi. Au anaacha ''ukoko'' kwenye choo kwa ndani wakati brashi ya kusafishia iko.
 
He kumbe dawa ya meno ina utaratibu wake wa kuminywa dah ckujua hili. Kwaiy ukiminya kwa utaratibu haiishi?. Anyway mvumilie mgeni mana tatizo ni malezi, na kama ukishndwa mpe nauli arudi kwao simiyu.
 
na unategemea kila kitu utafunzwa kwenye haya maisha..?
Nini maana ya kuishi na watu na kujifunza...?? Mbona vingine hatujafunzwa tumekuja kuona kwa watu tukaona ni kitu chema tukakibeba..?
Sasa, kuwa moja ya hao watu(jamii), mfundishe ustaarabu mbalimbali apate kubadirika. Niamini huyo anaweza badirika. Au ni ndugu upande wa mume basi unakosa confidence ya kumuelekeza mambo.
 
Sioni kama kuna tatizo, ni suala la mda tu.
 
Ni kweli, swala la kuminya lina ustaarabu wake.πŸ˜€
 
Tumia ujanja huu:
1. Wakati anakula embe wewe ita mtoto wako kwa sauti kwa kusema ''wewe fulani, umekaa unacheza tu! Mletee mgeni kitu cha kuwekea mabaki ya embe ili akimaliza apate urahisi wa kwenda kumwaga''!
2. Hili japo siyo issue sana, lakini unaweza kutumia tena watoto. Unamwita mtoto (wakati mgeni yupo) unamwambia ''angalia umeanza tena kuminya dawa ya mswaki ndivyo sivyo. Nilikufundishaje? Si nilikuwa uanze kuminya chini kwenda juu?''
3. Hilo nalo ukiona ameshika jagi unapaza sauti. ''Jamani mbona hamjasogezea mgeni glass mnamwacha anateseka kunywa maji na jagi kama yuko kambi ya fisi?''
 
Ila hiyo namba mbili ni unamuonea tu jamani??? Yani unataka kumpa masharti ya namna ya kuminya dawa?
Ila kwa ukweli dawa inatakiwa kuminywa from bottom, sio randomly tu kama unafinyanga unga wa ngano
 
Maelezo marefu sana.
In short umechagua kukaza fuvu mkuu.
Ishu sio madhara ishu ni ustaarabu na adabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…