Nimepata mgeni yuko rafu sana

Nimepata mgeni yuko rafu sana

Baadhi ya watz ni watu wa ajabu. Jamaa alinipigia simu anakuja kwenye interview ya kazi nikasema fresh njoo tu nakupokea hakuna shida. Eeehh naenda stendi kumpokea huyu rafiki yangu "Y" naona yuko na mtu mwingine "x" anatufata nyuma nyuma tunaingia kwenye gari naona "x" anaingia nauliza nani huyu ndo jamaa "Y" anasema huyu ni rafiki yangu. Namuuliza je na yeye "X" kaja kwenye interview? Jamaa anasema hapana yeye kaja kutembea tu.

Kufika home yule mwamba X aliyekuja kutembea kumbe anavuta sigara kama kichaaa. Mimi na moshi wa sigara hatupatani hata kidogo mwamba akiingia ndani nyumba nzima moshi unanuka.

Nikamuambia yule mwamba X mimi na sigara hatupatani naomba usivute sigara nyumbani kwangu mwamba akanielewa. Baada ya kufanya interview yule rafiki yangu Y akasema hawezi kuondoka hadi majibu yatoke nikasema fresh. Baada ya majibu kutoka akawa amekosa nafasi nikajua sasa anasepa heee naona siku na kwanza, ya pili, ya tatu wapo tu.

Nikaona yule mwamba Y mvuta fegi ameanza kufukuzia mwanamke nyumba ya jirani ambao tunaheshimiana sana nikaona wema utaniponza. Mimi nika deal na rafiki yangu tu. Nikamwambia sasa mimi nasafiri rafiki yangu akasema we nenda utatukuta tu mkuu ukirudi. Nikamwambia hapana kubaki mimi nasafiri kesho kutwa nyinyi mnaondoka kesho asubuhi mapema. Ndio ulikua mwisho wa mawasiliano.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
Safi sana. Ukicheza na mbwa atakufuata mpaka msikitini. Wengine wangekuja hapa JF kuulizia wafanyeje?
 
Dawa hata unapoanza mara ya 1 unatakiwa uanze kuminya chini. Haiminywi kuanzia juu. Kama ulikua hujui chukua hiyo usije kutoa boko ugenini.
Issue sio kutoa Boko au kutotoa boko, kwanza most of the time kati ya vitu ninavyopack nikiwa safari ni pamoja na dawa ya meno

Ninachojaribu kusema Mimi ni kwamba, mgeni akiminya kuanzia juu au chini, sioni kama ni issue kubwa sana, inavumilika.

Labda nikuulize, ukiachana na shape/muonekano wa hiyo dawa, ni yapi madhara yatokanayo na kubinya dawa tokea kati?
 
Wew ulibahatika kufunzwa na mama yako namna ya kuminya dawa, so utamlaumu vp yeye ambae hakufunzwa juu ya huo ustaarabu.
na unategemea kila kitu utafunzwa kwenye haya maisha..?
Nini maana ya kuishi na watu na kujifunza...?? Mbona vingine hatujafunzwa tumekuja kuona kwa watu tukaona ni kitu chema tukakibeba..?
 
1. Uchafu anaweka popote, anaweza kula embe kisha maganada akaacha hapo chini ndani yani akawa yuko comfortable kabisa.

2. Dawa ya meno anaminya popote tu.

3. Jagi la maji anakunywa kwa kushika lote na mmekaa wengi mnakula na grass zipo.

4. Inshort things are mess
= glass

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Wakati mwingine tukubali tu

Kuna watu wamekulia mazingira ambayo hakuna utaratibu wa kurudisha kitu chochote ulichotumia mahali pake.

Yaani maisha yao hayana mpangilio.

Usimlaumu, we akienda kinyume na utaratibu wako wewe rekebisha.

Malezi hayo
Nakubaliana na maneno yako. Malezi yna-play part kubwa. Pia kuna watu kwa asili wako rafu tu. Yaani hawajishtukii. Unakuta mtu anaingia chooni, (hivi vya kuvuta) ''anapiga baruti'' paa, anachafua choo na mfuniko wake kwa ''cheche za kinyesi'' na kuacha hivyo hivyo hivyo. Yaani yeye akishavuta kinyesi kikienda ni basi. Au anaacha ''ukoko'' kwenye choo kwa ndani wakati brashi ya kusafishia iko.
 
He kumbe dawa ya meno ina utaratibu wake wa kuminywa dah ckujua hili. Kwaiy ukiminya kwa utaratibu haiishi?. Anyway mvumilie mgeni mana tatizo ni malezi, na kama ukishndwa mpe nauli arudi kwao simiyu.
 
na unategemea kila kitu utafunzwa kwenye haya maisha..?
Nini maana ya kuishi na watu na kujifunza...?? Mbona vingine hatujafunzwa tumekuja kuona kwa watu tukaona ni kitu chema tukakibeba..?
Sasa, kuwa moja ya hao watu(jamii), mfundishe ustaarabu mbalimbali apate kubadirika. Niamini huyo anaweza badirika. Au ni ndugu upande wa mume basi unakosa confidence ya kumuelekeza mambo.
 
kuminya dawa kuna ustaarabu wake pia, sisi tulifunzwa na Mama yetu toka udogoni kabisa..!!
Mfano mzuri, kwetu nyumbani tukiwasha jiko la mkaa huwa hatushiki mkaa na mikono toka utotoni tena Mama ndiye alitukataza..!
Huwa tuna gloves flani ngumu tunavaa ndiyo unaweka mkaa, Mimi till date kugusa mkaa ugenini nababaika sana..!! Niliwahi semwa ugenini mpaka nikakosa raha..!

Hivyo mara nyingi ni malezi tu..!!
Ni kweli, swala la kuminya lina ustaarabu wake.😀
 
1. Uchafu anaweka popote, anaweza kula embe kisha maganada akaacha hapo chini ndani yani akawa yuko comfortable kabisa.

2. Dawa ya meno anaminya popote tu.

3. Jagi la maji anakunywa kwa kushika lote na mmekaa wengi mnakula na grass zipo.

4. Inshort things are mess
Tumia ujanja huu:
1. Wakati anakula embe wewe ita mtoto wako kwa sauti kwa kusema ''wewe fulani, umekaa unacheza tu! Mletee mgeni kitu cha kuwekea mabaki ya embe ili akimaliza apate urahisi wa kwenda kumwaga''!
2. Hili japo siyo issue sana, lakini unaweza kutumia tena watoto. Unamwita mtoto (wakati mgeni yupo) unamwambia ''angalia umeanza tena kuminya dawa ya mswaki ndivyo sivyo. Nilikufundishaje? Si nilikuwa uanze kuminya chini kwenda juu?''
3. Hilo nalo ukiona ameshika jagi unapaza sauti. ''Jamani mbona hamjasogezea mgeni glass mnamwacha anateseka kunywa maji na jagi kama yuko kambi ya fisi?''
 
Ila hiyo namba mbili ni unamuonea tu jamani??? Yani unataka kumpa masharti ya namna ya kuminya dawa?
Ila kwa ukweli dawa inatakiwa kuminywa from bottom, sio randomly tu kama unafinyanga unga wa ngano
 
Issue sio kutoa Boko au kutotoa boko, kwanza most of the time kati ya vitu ninavyopack nikiwa safari ni pamoja na dawa ya meno

Ninachojaribu kusema Mimi ni kwamba, mgeni akiminya kuanzia juu au chini, sioni kama ni issue kubwa sana, inavumilika.

Labda nikuulize, ukiachana na shape/muonekano wa hiyo dawa, ni yapi madhara yatokanayo na kubinya dawa tokea kati?
Maelezo marefu sana.
In short umechagua kukaza fuvu mkuu.
Ishu sio madhara ishu ni ustaarabu na adabu.
 
Back
Top Bottom