Nimepata mtoto wa kiume usiku huu, baada ya kuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 7

Nimepata mtoto wa kiume usiku huu, baada ya kuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 7

Kiongozi hakuna baba halisi anaweza kuwa na hiyo akili walionao Hawa wajinga.

Sisemi kuwa hayatokei, yanaweza kutokea ila inategemea na mazingira.

Binafsi Wala sina shaka kabisa kuhusu uzao wangu, mwenye mashaka basi ujue anajua mashaka yake yalipoanzia.

Mim binafsi Nina alama katika uso wangu na hiyo alama nimeikuta Kwa mwanangu nilipoenda kumwona.

Sasa hapo DNA yanin!? Kama sio upuuzi ni Nini!
[emoji599][emoji599]7 years mtu una kojoa upepo tu afu from nowhere unyanyue kombe ..think outside the box labda kama ume amua kukaza fuvu alama ? wtf is alama[emoji28] Good luck
 
Ubarikiwe na hongera pia🙏

Acha kujichulia Kwa kauli Yako kuwa " Hata ukiondoka Leo...", omba maisha marefu Ili umlee mwanao na WADOGO zake na uone Hadi vitukuu nk nk
 
Kuna msemo wa kiarabu usemao "inna baada Sabri, bushraa" yaani hakika Kila baada ya subra ni habari njema.

Hakika ndo ninavoweza kusema baada ya kuishi na mke wangu Kwa zaidi ya miaka 7 bila mtoto.

Hatimae Leo tarehe 27.07.2024 naandika historia mpya na njema katika mgongo wa ardhi hii ya dunia kwakuwa na mtoto wakiume.

Haikuwa rahisi ila kwakuwa nilimwachia mungu, naamin Leo ameamua kunijibu.

Hakika subra ni dawa na ponyo tosha Kwa wanaadamu.

Baada ya miaka mingi ya majuto na machozi Kwa mke wangu hatimae Leo amemuona mwanae mwenyewe.

Nashukuru mungu nami alinipa subra na uvumilivu wakuamini kuwa ipo siku tutapata mtoto.

Asikuambie mtu ni mtihani mkubwa saana kuwa kwenye ndoa na ukakosa mtoto Kwa muda mrefu.

Mungu alinipa maneno ya kumfariji Kila nilipomuona mke wangu analia.

Hakika nilikuwa mnyonge saana, ila usiku wa Leo mwanangu amenipa nguvu kubwa saana.

Amefuta Kila aina ya huzuni na kufanya nisahau Kila uchungu niliowahi kuwa nao.

Mungu nitunzie mwanangu, nitafanya Kila niwezalo huyu mtoto aishi Kwa furaha.

Hata kama nikiondoka Leo katika dunia hii najua kuwa nimeacha mtoto.

Tafadhali, nakuomba mungu usinicheleweshee na ndugu zake.

Mungu wape subra na uwafanyie wepesi wale wote wanaopitia katika mtihani huu, hakika wewe ndo mjuzi wa Kila kitu. Kwako halicheleweshwi jambo isipokuwa pale utakapo.

Hakika wamesubiri basi wape shufaa nao waone kizazi Chao.

Ameeeen!​
Hongera
 
Hongera sana!

Nilishuhudia ndoa ya afisa mmoja haikupata mtoto hadi uzee!

Walisubiri bila mafanikio na kwa kuwa walikua wakristo hawakua na namna!
 
Uharo mtupu ulio andika hapa. Uchukie Hadi na wazazi kisa mkeo?

Wanaume kama wewe ukifa Leo sa2 asubuhi huyo mkeo ataolewa baada ya mazishi yako tu halafu Watoto wako watazagaa kama Watoto wa Bata.

Heri ungetukuza wazazi wako kwanza then mke. Ambae hata Sasa Hivi mkizinguana utaoa mwingine hata kesho

Si bure huenda karogwa.!
Kwa hao nduguze Sawa labda ni watu wa husuda, sasa hata wazazi nao kweli jamani ?!
Labda mwaya.
 
Nimecheka ujue[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
Kwenye ndoa ndo wanaongoza kutoa mimba eti
Naweza nikakubaliana na wewe..sikuwah kuwa na mawazo ya abortion kioindi chooote za ujana wangu ila jaribu hili nilikutana nalonkwa mara ya kwanza nikiwa tayar nimeoa
 
H

Kuna msemo wa kiarabu usemao "inna baada Sabri, bushraa" yaani hakika Kila baada ya subra ni habari njema.

Hakika ndo ninavoweza kusema baada ya kuishi na mke wangu Kwa zaidi ya miaka 7 bila mtoto.

Hatimae Leo tarehe 27.07.2024 naandika historia mpya na njema katika mgongo wa ardhi hii ya dunia kwakuwa na mtoto wakiume.

Haikuwa rahisi ila kwakuwa nilimwachia mungu, naamin Leo ameamua kunijibu.

Hakika subra ni dawa na ponyo tosha Kwa wanaadamu.

Baada ya miaka mingi ya majuto na machozi Kwa mke wangu hatimae Leo amemuona mwanae mwenyewe.

Nashukuru mungu nami alinipa subra na uvumilivu wakuamini kuwa ipo siku tutapata mtoto.

Asikuambie mtu ni mtihani mkubwa saana kuwa kwenye ndoa na ukakosa mtoto Kwa muda mrefu.

Mungu alinipa maneno ya kumfariji Kila nilipomuona mke wangu analia.

Hakika nilikuwa mnyonge saana, ila usiku wa Leo mwanangu amenipa nguvu kubwa saana.

Amefuta Kila aina ya huzuni na kufanya nisahau Kila uchungu niliowahi kuwa nao.

Mungu nitunzie mwanangu, nitafanya Kila niwezalo huyu mtoto aishi Kwa furaha.

Hata kama nikiondoka Leo katika dunia hii najua kuwa nimeacha mtoto.

Tafadhali, nakuomba mungu usinicheleweshee na ndugu zake.

Mungu wape subra na uwafanyie wepesi wale wote wanaopitia katika mtihani huu, hakika wewe ndo mjuzi wa Kila kitu. Kwako halicheleweshwi jambo isipokuwa pale utakapo.

Hakika wamesubiri basi wape shufaa nao waone kizazi Chao.

Ameeh​

Najua namna gani ulivyo na furaha. Mungu aizidishe furaha yako mara dufu.

Ndugu yangu alisubiri miaka 8 bila ya mtoto. Can u imagine? Tena wote wakiwa na afya njema bila tatizo lolote. Kila kitu kipo sawa, ila mimba haikamati.

Kila upande ukaanza kuinyooshea kidole upande mwingine. Upande wa mume (sisi) tukaanza kusema ndugu yetu hana shida. Tufanye mpango *mke wa pili.

Upande wa mke unamuasa ndugu yao, agawe uroda kwa wanaume wengine. Wamfungulie jamaa njia 🤣🤣🤣. Duh!
.
Tafrani tupu. Maneno mengi sana. Lakini wenza wale waliamua kusubiri. Waliamua kuupa muda uamue.

Baada ya miaka nane ya msoto, hatimaye wakabarikiwa kupata mtoto wa kike, mrembo kweli kweli. Mchangamfu na mjanja sana. Huna haja ya kuulizia kama ni wa babaye, unahitimisha tu.

Bahati ilikuwa kwao. Walioana wangali vijana. Sasa wana watoto watano wenye furaha kubwa.

Usikilize maneno ya watu. Hawajui mateso uliyopitia. Furahia na umshukuru Mungu. Mrejeshee sifa na utukufu. Binadamu hawa wanaokutia wasiwasi ndiyo wale waliokuwa wanakusimanga wewe na mkeo. Kisa mmeshindwa hata kupata mtoto mmoja.

Leo wanaibuka na kukutia hofu, ili uendelee kuishi kwa wasiwasi. Binadamu hajawahi kueleweka.

Kila la kheri.
Hongera sana mkuu...jambo la kher Hilo na kwakuwa uliamni Kwa Allah... hongera pia kwakuwa na uvumilivu wa Hali ya juu.🫡
 
Hongera saaaaaaana kwa kupata mtoto. Hongera kwa kuwa na subira kusimama na mkeo katika huzuni na furaha. Natambua unayo furaha isiyo kifani, basi jitahidi kufurahi mwenyewe ili kujiepusha na kumuepusha mwanao na husda za walimwengu.

Sisi tunao comment hapa ni mfano wa jamii inayokuzunguka. Usituone na roho mbaya zetu, inawezekana sisi ndio jirani/nduguzo.
Watu wanakukejeri hapa sababu ya husda. Husda ni mbaya zaidi ya uchawi. Kutamani jambo LA kheri limponyoke mtu ni husda.

Hizi comment zikupe funzo kuwa wapo majirani/ndugu wanaotamani hata huyo mtoto asiwe wako. Omba sana katika imani yako ulindwe na husda.
Hasidi mtu mbaya
 
mimi sijataka kumuumiza moyo tena watu wenyewe hawa hawana Mungu wa kweli, naomba niishie hapa. ila mpende tu mwanao na mshukuru mkeo amekufichia aibu iwe wakwako au si wa kwako umheshimu sana. ulikuwa unaumbuka hivyo
Kumbe kukosa mtoto ni aibu na kuumbuka?
 
Back
Top Bottom