Nimepewa onyo na wafanyabiashara wenzangu nisipopandisha bei watakatisha uhai wangu

Mama anafungua nchi
 
Katoe taarifa kituo cha polisi kilicho karibu nawewe,usichukulie utani,utauawa.
 
Toa Tangazo, Ripoti Polisi,

Pandisha Bei Kutoka 8000-11000 au Uza 12000 Toa Nyongeza Kilo Moja Kwa Mteja Anayenunua Kuanzia kilo 5
Tafuta Njia Nzuri Ya Kubakiza Wateja Kwa Mfano Toa Zawadi ya limao,Vifungashio Na Fanya derivery kwa wateja wakubwa.
 
Soko huria unampangia mtu bei ya kuuza... Fuata taratibu za kisheria endelea na bei yako. Tena ikibidi waoneshe uwamba, punguza bei mpaka 7,500 ili waendeleaa kuteseka na ikibidi wafunge biashara.

Hii mbinu kwa wachumi tunaita predatory pricing. Wakishafunga, wewe ongeza bei mpaka 12,000 halafu upige hela wao wakipiga miayo.
 
Wewe la msingi ni kupandisha bei na kuhakikisha ubora wa huduma yako. Wapige kwenye huduma. Pia lia na wauzao kitimoto hai. Walalie kidogo. Tengeneza mazingira ya kupunguza gharama
 
Kuna kijiji kimoja niliwah kukuta kuna maduka mawili,hao majamaa wenye hayo maduka ni mamafia balaa,wengi wanaokuja kuanzisha hapo biashara kama hyo wanapigwa mikwara na kuibiwa pia wanabomoa usiku na ukija na bei ndogo ndogo kila siku wanakuwa wanakufata

Kwenye biashara lazima wafanyabiashara muwe kitu kimoja kumkandamiza mnyonge
 
Ongea nao Ili wote muuzw Kwa elfu kumi
 
Bei uliyo shusha haipo kiushindani! Ungefanya hata elf10 au 11 atleast

Sent from my TECNO LB6 using JamiiForums mobile app
Ushindani gani unaozungumzia babu? Biashara ina mbinu nyingi, yeye kaamua kuongeza mauzo Kwa kupata faida ndogo hiyo pia ni technique, kama hapati faida automatically atafunga kijiwe mwenyewe na hakuna wakuja kumshikia panga.
 
Ongea nao muwe mnauza Bei Moja ila kwenye utoaji wa huduma ndio uwe unafanya vizur ,
 
Hata mimi ningekufata, hawa watu humu wanakuvimbisha kichwa ila ukweli ni kuwa unaharibu biashara za watu na watakufanya kitu mbaya ukizidi kuwa kichwa ngumu.
Pandisha bei hadi 11500 au 11000 utaeleweka.
Kuna wapumbavu hii nchi mtaka kuifanya ya Baba yenu, kwanini umpangie mtu bei ya kuuza? Kama anauza bei ya hasara automatically hatachukua round biashara itakufa yenyewe, huku shinyanga na geita miaka ya nyuma jamaa wa kaskazini waliiteka biashara ukanda huu Kwa bei za kuumiza Ila tangu mnyantuzu kaijua biashara jamaa wote wamechora. Wote mnaotaka na kulazimisha kufix bei ni wapuuzi na wapumbavu wakubwa.
 
Nunua bunduki, Kila SIku kabla ya kulala unafyatua Risasi Tatu angani.

Kutishiwa maisha kiwe kigezo cha kupata hiyo bunduki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…