Nimepiga hesabu ningewekeza UTT ningekua niko vizuri

Nimepiga hesabu ningewekeza UTT ningekua niko vizuri

Mimi now 60+ml sina papara na biashara za high return kifupi kila mtu ashinde mechi zake
Sure aisee mie nilipata kamgao ka 100 kwenye michakato january hii nikatupia hapo 35, 5 nakanywa bia na 60 nakajipongeza kwa gari bora ningeizika yote hapo saa hizi ingekuwa kicheko tu. january ijayo sifanyi masihara.
 
12% ya 4,500,000 ni 540,000
12% ya 5,040,000 ni 604,800
12% ya 5,644,800 ni 678,000

Kwa miaka mitatu ungepata 1,823,000
NB; Bado uwekezaji wa ardhi ni mzuri kwako.
Mkuu hesabu zako hizi ni iwapo atakua hachukui faida yake kwa mwaka, kama atakua nachukua faida ita drop

Ikiwa kwenye kodi anachukua 30,000 per month

30,000 x 12 = 360,00 per year
Ukizidisha kwa miaka 3
360,000 x 3 = 1,080,000 Faida kodi kwa miaka 3

Faida ya utt toa faida ya kodi
1,823,00 - 1,080,00 = 743,000

Hapo maana yake una “hasara” ya 743,000 kwa miaka 3 ambayo ungeipata kwenye utt.......

Jambo la msingi kuzingatia hapo ni thamani nzima ya uwekezaji kwa ujumla kadiri siku zinavyokwenda
Je baada ya miaka kumi itakuaje?

Kwenye nyumba utakua unachukua kodi unajikumu halafu nyumba inabaki palepale na thamani yake inazidi kuongezeka

Utt kama utakua unachukua faida na kujikimu thamani ulioiwekeza itabaki pale pale 4,500,000

Kupanga ni kuchagua
 
Back
Top Bottom