generationn Z
JF-Expert Member
- Jun 30, 2025
- 454
- 748
Nina muda wa takribani miaka 10 sijapita barabara ya Mwanza–Mara, lakini sasa nimeipita. Ebwana wee! 🤔
Kuanzia Kisesa, Magu hadi Ramadi, barabara imeharibika kiasi cha kuonekana kama imetelekezwa. Imejaa mabonde na mashimo mengi kiasi kwamba hata barabara ya vumbi inaweza kuwa nafuu zaidi.
Hata hivyo, kuanzia Serengeti, Makutano (Sabasaba) hadi Tarime, barabara iko katika hali nzuri na inapitika vizuri.
Kwa kifupi, ni aibu kwa barabara kuu kama hii kuwa na mashimo kiasi hiki. Hii ni kero kubwa kwa madereva wanaotumia njia hii mara kwa mara. Mamlaka husika, naamini mpo; je, aibu hii hamuioni?