KERO Nimesafiri toka Mwanza-Musoma kiukweli barabara zetu bado ni changamoto

KERO Nimesafiri toka Mwanza-Musoma kiukweli barabara zetu bado ni changamoto

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Nina muda wa takribani miaka 10 sijapita barabara ya Mwanza–Mara, lakini sasa nimeipita. Ebwana wee! 🤔

Kuanzia Kisesa, Magu hadi Ramadi, barabara imeharibika kiasi cha kuonekana kama imetelekezwa. Imejaa mabonde na mashimo mengi kiasi kwamba hata barabara ya vumbi inaweza kuwa nafuu zaidi.

Hata hivyo, kuanzia Serengeti, Makutano (Sabasaba) hadi Tarime, barabara iko katika hali nzuri na inapitika vizuri.

Kwa kifupi, ni aibu kwa barabara kuu kama hii kuwa na mashimo kiasi hiki. Hii ni kero kubwa kwa madereva wanaotumia njia hii mara kwa mara. Mamlaka husika, naamini mpo; je, aibu hii hamuioni?
Barabara nyingi za Tz ni 10% zinatengenezwa kwa kiwango duni sana.
Kuna barabara ya Manyara Babati-Nzega pia ni changamoto mashimo ni mengi kwa sasa ndo inazibwa viraka.

Isingekua 10% ingedumu kama ya DODOMA- BABATI- ARUSHA
 
Sio siri hii ni aibu kubwa
 
Back
Top Bottom