Unadhani
Execute una cha kuwasilisha katika jamii ya kikristo ya catholic kuhusu Mariam ukaeleweka au ukabadilisha mtazamo walio nao kuhusu Maria.
Au unadhani wewe ndie ulie na ufahamu mkubwa wa biblia kuliko wengine wote na kwamba wewe ndie sasa unakua mkombozi wa wengi walio kwenye upotofu kwa mijibu wako?
Kama ni imani ambayo haina mahusiano na wewe au haina athari na wewe unaweza ukaachana nao tu .
Maana imani na dini na madhehebu yapo kila mahali na kila jamii na kila mmoja wao ana mafundisho ya aina yake yasiyo ingiliana na wengine na maisha yanaendelea.
Huwezi kuongeza au kupunguza kitu kwenye mjadala wa Maria kuhusu kuwa mama wa Mungu , huo mjadala ulishajadiliwa miaka na miaka karne na karne, ulileta athari mpaka kutokea kugawanyika kwa kanisa katoliki la rumi na kanisa katoliki la mashariki.
Pamoja na hayo ni zaidi ya miaka 1000 sasa Maria anatajikana kama mama wa Mungu so usidhani kwamba wewe ndie uko bora zaidi kuliko wengine wote au Mungu anae ona hayo na kuyaacha yaendelee.