Nimeshangaa kumuona Profesa mmoja maarufu wa pale UDSM akisali sala ya Bikira Maria

Mambo ya kiimani ni magumu sana hasa kama uelewi vizuri. Wao si wapumbavu wasali vile..
Ivi ushawishi jiuliza kwa jicho la tatu kwanini wanamtaja sana Maria.?
Nakupa hom work hiyo Mkuu.

Wewe uko sahihi na wao wako sahihi kutokana na maandiko waliyosoma..
 
Penye utata ni Yesu kuwa Mungu na Binadamu. Wakubwa wamefanya kuwa dogma, yaani wewe kariri tu na uamini. Mimi sikubali, ni lazima nihoji. Ina maana usali kupitia kwa Kristo, wasiomwamini kama Mungu watasali kupitia wapi?
 
Naunga mkono hoja imani ni dubwana moja lenye nguvu linaloweza hata kuiweka mfukoni rational thinking ya mtu
 
Mkuu waliopo nje ya Kanisa Katoliki hawaelewi yaliopo ndani ya Kanisa hilo wamekaa kulishambulia tu badala ya kufanya analysis.

Wakatoliki tunamuomba Bikira Maria atuombee kama wao wanavyokwenda kwa Mchungaji wao na kumuomba wawaombee hata ile sala ya salamu Maria ipo ndani ya Biblia ni maumkuzi ya Malaika Gabriel aliyetumwa na Mungu kumpasha Maria kuwa atamzaa Yesu ''Salamu;uliyepewa neema;Bwana yu pamoja nawe"(Soma Luka 1:28)pia ni maneno ya Elizabeti aliyetamka maneno baada ya kujazwa na Roho Mtakatifu alipokuwa ametembelewa na Bikira Maria''Umebarikiwa wewe katika wanawake naye naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa" (Soma Luka 1:42)
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Huu ndio upunguani siezi ufanya
 
Mbinguni hatufiki
 
Usimshangae Prof, tulisambaratishwa tangu siku ile mwanadamu alipokuwa anajenga mnara wa Babeli akamuone Mungu .

Kuanzia hapo ndiyo kila kitu kilienda ndivyo sivyo.

Haya mambo ya ujuaji hayakuanza leo , kuna wajuaji hao waliona isiwe tabu wacha tumpandie huko huko tukamuone.
 
Huyo ni prof, means anakuzidi elimu na ufahamu kuhusu vitu vingi, uwezo wake wa kuelewa vitu ni mkubwa, kwanini usiwe inspired ni kwanini mtu wa hivo anasali kwa maria?

Anyways we catholics we dont give a f*ck, keep crying until them tears dry!
 
Nimecheka sana kama mazuri vile dah
 
Mkuu, sasa kama unamshangaa kumuona Profesa akisali, si utulie uendelee kumshangaa hadi uone mwisho wake?NB, Imani yake isiwe kero kwako - Kama hutaki kumuona basi uwe unafumba macho unapopita hapo au acha kufatilia ya wenzio komaa na hali yako boss.
 

Inabidi waikristo mchapwe VIBOKO
ndio mana siku zote manabii wanawafanya kama mosukule yao
Ona hapo alivyofundishwa yaan hapo JUU alichoandika hata yeye mwenyewe SIDHANI kama anaelewa alichoandika
 
Mama Maria Malkia wa Amani...Utuombee

Roman Catholic inawatesa sana halafu ajabu sisi hatuna shida naye i mean hatutaki kufahamu ya nyie mnaojihesabia Haki.

Kupitia Imani yangu ya Romani kusali rozari kwa Mama Bikira, kuabudu Ekaristi, kuhudhuria Misa Takatifu, kuwaombea Marehemu hakuna nliloomba Mwenyezi Mungu akaninyima

Kifupi wewe endelea kuamini huko kwako ndugu yangu

Ya waromani mtuachie waromani
 
Asilimia 70 ya maprofesa nchini ni wakatoliko na wanasali Salaam Maria sasa sijui hii imekaaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…