Nimeshangazwa na kauli ya Rais kudharau msimamo wa Waziri wa Kilimo juu ya kuzuia uagizaji wa sukari nje

Hizi ni sera na sheria za nchi kulinda viwanda vya ndani, unless na Sheria tubadilishe.
Pia hapo tusiishie tu kwenye sukari,Bali kila biadhaa iruhusiwe kuingia kwa wingi. Lakini tuwe tayari kwa athari za kuanguka uchumi, nadhani unaelewa athari za nchi kununua sana nje kuliko kuuza nje
 
Safi sana umefafanua vizuri
 
Prof kwa kulinda heshima yake, bora akae pembeni. Dunia kizungumkuti sana.

Huku mnasema wawekezaji njooni. Huku mnawapiga sindano ya ganzi

Sugar importers wana influence kubwa sana katika Taifa letu, hilo msilisahau, na wala hawazidi wanne, binafsi naona ushawishi wao unaanza kurudi taratibu taratibu mwisho wa siku wataanza kulikalia Taifa letu kooni kwa mara nyingine tena - watahujumu viwanda vya sukari kwa import kile watakacho dai ni industrial Sugar kumbe ukaghai mtupu, wata import sukari inayo karibia muda wa ku-expire wanai-rebag upya na kuingiza sokoni - biashara ya ku-import sukari haina tofauti na biashara ya madawa ya kulevya ukisha ianzisha utaki kuiacha anakuwa kig'ang'anizi tu!!

Cha muhimu hapa kwa Madam President akumbuke kwamba Sugar is a Political commodity washauri wake walikumbuke sana hilo.
 
NONSENSE!
 
1. Kama tukizuia bidhaa za nchi za wenzetu wasiuze hapa nchini, si na sisi za kwetu zitazuiwa kuuzwa huko kwenye mataifa yao?

2. Tunahimiza uchumi wa viwanda ili iweje? Mimi nadhani ni ili tuzalishe kwa wingi na ziada iuzwe nje ili tupate fedha za kigeni nyingi?

3. Kama tangu 2015 alipoingia Magufuli na kutoa wazo hilo la kupanua mashamba nà kuzalisha sukari nyingi, mbona mpaka leo mambo yako vilvile? Nini tatizo? Ni agizo/tamko halikuwa na nguvu au ni tatizo la kisera na mipango mibovu ya serikali hii ya CCM?

4. Kama sukari haitoshi hapa nchini, ni vyema turuhusu ya nje iingie ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa bei. Vivyo hivyo Simenti na bidhaa zingine toka mataifa mengine ziingie kwa wingi mpaka pale akili zitakapokaa sawa ili tuzalishe wenyewe...
 
Hilo bomba walileta kipindi cha Magu na Sukari yao tulizua
 
Uganda wameipa Tanzania biashara ya mabilioni ya dola wangeamua kuipa kenya Tanzania ingekosa biashara.

Biashara hio ni bomba la mafuta, kutumia bandari ya Dar, kukaribisha wawekezaji wa Tanzania nk

Kwa kuweka mizani iwe Sawa ukitaka kupata lazima ukubali kupoteza kuleta uwiano Ndio kanuni ya biashara .

Kodi ya wawekezaji wa sukari ni ndogo kuliko hizo faida 👆🏿.

Na wawekezaji wa sukari wamejikokota tangu muda mrefu wameachiwa nafasi ya biashara bado uzalishaji umekuwa mdogo bei ya sukari imezidi kupanda .
 
Mimi nafikiri kilinda viwanda hufanywa kitaalamu na sera za kodi lakini kutumia nguvu na kuzuia uagizaji ni primitive method,ninavyo wajua wafanya biashara uliwalinda kwa hizo method primitive wataagiza machinery zilizopitwa na technology ambazo nchi nyingine wanatupa.Matokeo yake bidhaa inakuwa ghali,unapo ruhusu bidhaa kutoka nje ukatoza ushuru kwa ajili ya fare competition utaimprove quality yabidhaa,price competition hivyo utamnufaisha mraji.
 
Ikiwa wanazalisha Sana, kwa nini wananunua kutoka Brazil?
Kuna ujanja inafanyika wa kupack tena sukari, naa ndio maana hata Kenya walikataa
 
Kuitwa NONESENSE kwa jambo la halali halafu ukaendelea kubaki ofisini wakati wewe ni mbunge na Profesa tena toka jamii ya akina Mangi ni upumbavu wa Mpumbavu.

Mkenda ungepaswa kujiuzulu usiku ule ule. Labda umeamua kufuata nyayo za Prof mwenzako Mbarawa maana nae aliitwa Mpumbavu hadharani na akaendelea kukomaa
 
Kama sukari ikiagizwa itashuka bei walau 1500 na iagizwe tu hakuna namna,ila kama bei zinahakia mulemule bora tubakie nauzalishiji wa ndani
Sijui Kama mnawaza sawasawa, Bei inaweza kuwa 1500 Ila kwa sukari iliyoisha muda wake na ndio hiki wafanyabiashara wengi wanataka. Brazili wanazlisha Sana sukari na inapokaribia muda kuisha huuzwa kwa Bei ndogo Sana na ndio hapo wajanja wa Africa hukimbilia kuinunua na kui-pack upya
 
Unapoona USA wanaizuia Huawei kuuza simu zake kule Marekani unafikiri hawana sera zozote za maana?
 
Professor Mkenda bado hajajiuzulu tu? Kuna watu wana roho ngumu sana.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Unapoona USA wanaizuia Huawei kuuza simu zake kule Marekani unafikiri hawana sera zozote za maana?
Hapo ni quality mbona wengine wanaruhusiwa kuuza,au politics kama China anazuia basi naye anazuia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…