Nimeshangazwa na kauli ya Rais kudharau msimamo wa Waziri wa Kilimo juu ya kuzuia uagizaji wa sukari nje

Nimeshangazwa na kauli ya Rais kudharau msimamo wa Waziri wa Kilimo juu ya kuzuia uagizaji wa sukari nje

Tunalinda viwanda vya ndani vyenye uwezo mdogo kwa gharama kubwa sana na kwa kubebesha mzigo wananchi. Sukari ikiingia kutoka Brazil bei yake haitazidi TSH. 1800, ukilinganisha na bei ya sasa ya TSH 2600 hii si kulinda viwanda vya ndani bali ni rushwa. Mambo ya monopoly yalishaisha zamani! Kwanini tunalinda viwanda vya sukari tu na vingine vinashindana na vya nje kama kawaida. Natamani kujua viwanda vya sukari vinamilikiwa na nani maana vilibinafsishwa.
Hizi ni sera na sheria za nchi kulinda viwanda vya ndani, unless na Sheria tubadilishe.
Pia hapo tusiishie tu kwenye sukari,Bali kila biadhaa iruhusiwe kuingia kwa wingi. Lakini tuwe tayari kwa athari za kuanguka uchumi, nadhani unaelewa athari za nchi kununua sana nje kuliko kuuza nje
 
You are totally misinformed buddy,UG wanatumia Mombasa Port kwa almost 82% ya mizigo yake the rest ndio ifikirie TZ. Again SGR ya KE now inatoboa mpaka Naivasha mpaka Busia mdomoni kabisa mwa mpaka wa UG na KE, na wamepewa free land area kwa ajili ya kujenga Dry Port ya Mizigo.

Bomba la mafuta kupitiishiwa Tanga ni kwa sababu ya inflated costs na sheria za KE kulipa maradufu fidia, ardhi Mali ya mtu na si serikali. Mwekezaji yeyote huangalia cheap option kwa ajili ya ku maximize profit.

Again, monsoon winds ambazo huwa zaidi ya miezi 3 kwa mwaka ilikua ni tatizo katika njia ya kupitisha bomba, bomba lingefika bandari ya Lamu ambayo ilikua chini ya ujenzi haijakamalika by then wakati Tanga iko operational. Hakukua na njia mzuri na a lot of anti gravity katia njia ya Kenya tofauti na TZ. To top up, usalama kwani Lamu iko near na Somalia kwa Al Shabaab militants ambao pia hutarget Kenya na Uganda.

Get all the facts right.

Ni hayo tu.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
Safi sana umefafanua vizuri
 
Prof kwa kulinda heshima yake, bora akae pembeni. Dunia kizungumkuti sana.

Huku mnasema wawekezaji njooni. Huku mnawapiga sindano ya ganzi

Sugar importers wana influence kubwa sana katika Taifa letu, hilo msilisahau, na wala hawazidi wanne, binafsi naona ushawishi wao unaanza kurudi taratibu taratibu mwisho wa siku wataanza kulikalia Taifa letu kooni kwa mara nyingine tena - watahujumu viwanda vya sukari kwa import kile watakacho dai ni industrial Sugar kumbe ukaghai mtupu, wata import sukari inayo karibia muda wa ku-expire wanai-rebag upya na kuingiza sokoni - biashara ya ku-import sukari haina tofauti na biashara ya madawa ya kulevya ukisha ianzisha utaki kuiacha anakuwa kig'ang'anizi tu!!

Cha muhimu hapa kwa Madam President akumbuke kwamba Sugar is a Political commodity washauri wake walikumbuke sana hilo.
 
Bro ni vizuri pia ujue kuwa uganda nao wamesucrifice sana kwa kuleta bomba tanzania,hilo bomba kiuhalisia lilitakiwa lipite kenya but wao wakalileta kwetu na pia kuna benefits kubwa tunazipata kwa waganda kutumia bandari za tanzania badala ya za kenya hivyo na sisi ni lazima tuoneshe mkono wa shukrani
NONSENSE!
 
Mkuu!

Magufuli hakuzuia sukari toka nje kwa sababu ya roho mbaya hapana.

Alisema kabisa tuna mashambe mengi tuzalishe sukari yetu hapa hapa nchini na kufaidisha viwanda vyetu vya ndani.

Yule mzee aliambulia matusi toka wapumbavu badala ya kutumia fursa hiyo kuongeza uzalishaji ili kuinua vipato na kuongeza ajira.!

Kila siku huwa nasema hapa kwamba kumpigania mpumbavu malipo yake ni upumbavu!

Ona sasa tunaenda kuwa dampo la sukari toka uganda!

Nmeona uzi hapa jana mtu anashauri Samia aruhusu cement toka Kenya, na usishangae na yeye akafanya hivyo.
1. Kama tukizuia bidhaa za nchi za wenzetu wasiuze hapa nchini, si na sisi za kwetu zitazuiwa kuuzwa huko kwenye mataifa yao?

2. Tunahimiza uchumi wa viwanda ili iweje? Mimi nadhani ni ili tuzalishe kwa wingi na ziada iuzwe nje ili tupate fedha za kigeni nyingi?

3. Kama tangu 2015 alipoingia Magufuli na kutoa wazo hilo la kupanua mashamba nà kuzalisha sukari nyingi, mbona mpaka leo mambo yako vilvile? Nini tatizo? Ni agizo/tamko halikuwa na nguvu au ni tatizo la kisera na mipango mibovu ya serikali hii ya CCM?

4. Kama sukari haitoshi hapa nchini, ni vyema turuhusu ya nje iingie ili kuwapunguzia wananchi mzigo wa bei. Vivyo hivyo Simenti na bidhaa zingine toka mataifa mengine ziingie kwa wingi mpaka pale akili zitakapokaa sawa ili tuzalishe wenyewe...
 
Bro ni vizuri pia ujue kuwa uganda nao wamesucrifice sana kwa kuleta bomba tanzania,hilo bomba kiuhalisia lilitakiwa lipite kenya but wao wakalileta kwetu na pia kuna benefits kubwa tunazipata kwa waganda kutumia bandari za tanzania badala ya za kenya hivyo na sisi ni lazima tuoneshe mkono wa shukrani
Hilo bomba walileta kipindi cha Magu na Sukari yao tulizua
 
Uganda wameipa Tanzania biashara ya mabilioni ya dola wangeamua kuipa kenya Tanzania ingekosa biashara.

Biashara hio ni bomba la mafuta, kutumia bandari ya Dar, kukaribisha wawekezaji wa Tanzania nk

Kwa kuweka mizani iwe Sawa ukitaka kupata lazima ukubali kupoteza kuleta uwiano Ndio kanuni ya biashara .

Kodi ya wawekezaji wa sukari ni ndogo kuliko hizo faida 👆🏿.

Na wawekezaji wa sukari wamejikokota tangu muda mrefu wameachiwa nafasi ya biashara bado uzalishaji umekuwa mdogo bei ya sukari imezidi kupanda .
 
Mkuu!

Magufuli hakuzuia sukari toka nje kwa sababu ya roho mbaya hapana.

Alisema kabisa tuna mashambe mengi tuzalishe sukari yetu hapa hapa nchini na kufaidisha viwanda vyetu vya ndani.

Yule mzee aliambulia matusi toka wapumbavu badala ya kutumia fursa hiyo kuongeza uzalishaji ili kuinua vipato na kuongeza ajira.!

Kila siku huwa nasema hapa kwamba kumpigania mpumbavu malipo yake ni upumbavu!

Ona sasa tunaenda kuwa dampo la sukari toka uganda!

Nmeona uzi hapa jana mtu anashauri Samia aruhusu cement toka Kenya, na usishangae na yeye akafanya hivyo.
Mimi nafikiri kilinda viwanda hufanywa kitaalamu na sera za kodi lakini kutumia nguvu na kuzuia uagizaji ni primitive method,ninavyo wajua wafanya biashara uliwalinda kwa hizo method primitive wataagiza machinery zilizopitwa na technology ambazo nchi nyingine wanatupa.Matokeo yake bidhaa inakuwa ghali,unapo ruhusu bidhaa kutoka nje ukatoza ushuru kwa ajili ya fare competition utaimprove quality yabidhaa,price competition hivyo utamnufaisha mraji.
 
Hiyo issue ya hao wafanyabiashara naijua vizuri lkn sitabishana nawe baada ya kuacha takwimu na kuongelea nguo. Jamaa kasema hakuna viwanda huko mimi nikaonyesha kuwa vipo na wanabakiza maana wao wanahitaji tani 360,000 tu kwa mwaka. Hii ndiyo issue ya muhimu hapa
Ikiwa wanazalisha Sana, kwa nini wananunua kutoka Brazil?
Kuna ujanja inafanyika wa kupack tena sukari, naa ndio maana hata Kenya walikataa
Screenshot_20211129-100232_1.jpg
Screenshot_20211129-102516_1.jpg
 
Kuitwa NONESENSE kwa jambo la halali halafu ukaendelea kubaki ofisini wakati wewe ni mbunge na Profesa tena toka jamii ya akina Mangi ni upumbavu wa Mpumbavu.

Mkenda ungepaswa kujiuzulu usiku ule ule. Labda umeamua kufuata nyayo za Prof mwenzako Mbarawa maana nae aliitwa Mpumbavu hadharani na akaendelea kukomaa
 
Kama sukari ikiagizwa itashuka bei walau 1500 na iagizwe tu hakuna namna,ila kama bei zinahakia mulemule bora tubakie nauzalishiji wa ndani
Sijui Kama mnawaza sawasawa, Bei inaweza kuwa 1500 Ila kwa sukari iliyoisha muda wake na ndio hiki wafanyabiashara wengi wanataka. Brazili wanazlisha Sana sukari na inapokaribia muda kuisha huuzwa kwa Bei ndogo Sana na ndio hapo wajanja wa Africa hukimbilia kuinunua na kui-pack upya
 
Mimi nafikiri kilinda viwanda hufanywa kitaalamu na sera za kodi lakini kutumia nguvu na kuzuia uagizaji ni primitive method,ninavyo wajua wafanya biashara uliwalinda kwa hizo method primitive wataagiza machinery zilizopitwa na technology ambazo nchi nyingine wanatupa
Unapoona USA wanaizuia Huawei kuuza simu zake kule Marekani unafikiri hawana sera zozote za maana?
 
Nimeshangazwa na kauli hii ya Mh Rais, kuita msimamo wa mteule wake Waziri wa Kilimo juu ya kuzuia uagizaji wa sukari nje, kuwa NONSENSE, tena hadharani.

Nimesikitishwa na kauli hiyo kwa sababu mbili.

Moja, public reprimand kwa kiongozi mwandamizi, sidhani kama ni utawala bora.

Na hii naanza kuhisi ile power is getting to the head, and power corrupts.

Pili, nimesikiliza arguments za Mkenda, though pompous, kuna relevance pale.

Argument ni kuagiza sukari kama kuna shortage, si kwa matakwa ya wafanyabiashara.

Sasa wale wawekezaji wanaovipanua viwanda ili ku boost uzalishaji wa sukari, wale ni nonsense?

All in all, Mkenda anapaswa kujiuzulu ku-save face.
Professor Mkenda bado hajajiuzulu tu? Kuna watu wana roho ngumu sana.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Unapoona USA wanaizuia Huawei kuuza simu zake kule Marekani unafikiri hawana sera zozote za maana?
Hapo ni quality mbona wengine wanaruhusiwa kuuza,au politics kama China anazuia basi naye anazuia
 
Back
Top Bottom