Sijatua hapa KIA tangu 2016. Jana nimetua hapa kwa mara nyingine. Kama ningezibwa macho nikasafirishwa mpaka hapa then nikaachiwa nione bila matangazo na mabango yaliyoko hapa kwa haraka haraka nisingeweza kutambua kama pale nilipokuwa ni KIA, asimilia kubwa
ya miundombinu imeboreshwa na imebadilika kutoka uhalisia wake wa awali kwa kiwango cha juu sana.
Pongezi kwa wote mliohusika kuleta mabadiliko haya, Japo sikukuta ndege kubwa pale uwanjani lakini nina uhakika madege makubwa kama yale ya Qatar yanaweza kutua pale kwa sasa.
Vyumba vya kupumzika wageni vimeongezwa na vinapendeza kwa ujumla wake vyote kwa upande wa wageni wa nje na ndani.
Ombi langu kwa serikali ruhusuni makampuni mengine ya ndege mfanye nayo ushindani hasa kwa safari za ndani, ATCL wana bei kubwa sana na timetable zao hazieleweki, ratiba inaweza kuonesha mnaondoka saa 4 asubuhi, mkaondoka saa 4 unusu au saa 5 na dakika zake.
Hongereni kampuni ya KADCO mnaoendesha uwanja wa ndege wa KIA.