Nimeshazichoka vurugu za watoto, bora shule zifunguliwe

Nimeshazichoka vurugu za watoto, bora shule zifunguliwe

Kuna wa bro hao....mpaka unachukua video ya ushahidi lakini wanakataa kutenda makosa 😂😂😂
Kuna siku wameambiwa wakaoshe vyombo, kumbe wanachukua mapovu wanarushiana, wakija wameloana ukiwauliza wanasema maji yanatoka kwa nguvuu ilihali water tap ya dishwasher ipo adjusted isitoe maji kwa speed.
Wakati wakula ukiwasha tv imekula kwako msosi wao unakuwa wabaridi kabisa 😅😅
 
Kuna vitu watoto wanahatibu hadi unajiuliza huyu dogo amewezaje kuharibu hiki kitu, na nini alikua anatafuta huku? Ila uwezi pata jibu kamwe.

Kitu kingine cha ajabu hawa watoto wa siku hizi hawachoki, kuanzia asubuhi hadi usiku wapo active tu.
Bora warudi shule.
Waende tu kwakwelii mpka sasa buku jero limeenda, Kila nikiweka bando linabebwa, vitu vinajidowload tu , wamekorokochoa yaani nimeboeka vibaya mno.
 
Waende tu kwakwelii mpka sasa buku jero limeenda, Kila nikiweka bando linabebwa, vitu vinajidowload tu , wamekorokochoa yaani nimeboeka vibaya mno.
Ahahah wao kiboko mimi nilikuta simu yote ina magem ya mpira kila kona nakoenda mpira na bando la mwezi GB 35 nikakuta GB 16 wakati uhi nimejiunga siku tatu nyuma
 
Kuna vitu watoto wanahatibu hadi unajiuliza huyu dogo amewezaje kuharibu hiki kitu, na nini alikua anatafuta huku? Ila uwezi pata jibu kamwe.

Kitu kingine cha ajabu hawa watoto wa siku hizi hawachoki, kuanzia asubuhi hadi usiku wapo active tu.
Bora warudi shule.

Shida mnaachia shule iwalelee watoto. Onaona hata hujui pa kuanzia unamsukuma dogo shule.
 
Shida mnaachia shule iwalelee watoto. Onaona hata hujui pa kuanzia unamsukuma dogo shule.
Zamani watu wanaanza shule,wakiwa na miaka 7 kuendelea. Sasa hivi,mtoto wa mwaka na nusu eti anafundishwa madudu mbali mbali. Naonaga tu ni wazazi kukimbia majukumu,na wengine kutapeli watu;mwalimu aliesomea,hata akimpokea atakupa ukweli. Kuna umri watoto si wa kupelekwa shule. Af watu wanajiuliza ohhh, mbona wanasoma bado wadogo,shule nzuri,ada ndefu,af wanatoka hawana kitu kichwani. Mtoto amehalibiwa na wazazi. Sasa na huyu anaesema bora waende shule, natamani hii post angeisoma mke wake na ashuke na nondo tuone. Yeye siku tu keshachoka. Mama yao je?
 
Kuna vitu watoto wanahatibu hadi unajiuliza huyu dogo amewezaje kuharibu hiki kitu, na nini alikua anatafuta huku? Ila uwezi pata jibu kamwe.

Kitu kingine cha ajabu hawa watoto wa siku hizi hawachoki, kuanzia asubuhi hadi usiku wapo active tu.
Bora warudi shule.
Watoto ni baraka na ni uhai na ni furaha! Kuna wengine hawana hata wa kusingiziwa na wanatamani mno kuitwa wazazi😭
Mimi kila wakifanya vurugu namshukuru Mungu kwamba hawana tatizo
Ogopa sana watoto wakimya na wanaojifungia chumbani muda wote.. Wapo wapo tu hawana harakati zozote.. Akiumwa hujui akiwa mzima hujui
An idle brain is a carpentry of a devel
Hata hivyo inatukumbusha karama kubwa waliyo nayo walimu huko shuleni.. Imagine una watatu tu lakini unaona tabu lakini huko shuleni wanao mia mbili kama hao wako😂
 
Kuna vitu watoto wanahatibu hadi unajiuliza huyu dogo amewezaje kuharibu hiki kitu, na nini alikua anatafuta huku? Ila uwezi pata jibu kamwe.

Kitu kingine cha ajabu hawa watoto wa siku hizi hawachoki, kuanzia asubuhi hadi usiku wapo active tu.
Bora warudi shule.
Halafu wengi wao wamekaa kisharishari na kiugomvugomvi. Hawana cha mkubwamkubwa wala mdogomdogo. Wanachokozana, wanajibizana, wanapigana, wanalizana. Kutwa kucha kazi ni kuamua kesi zao tu. Kwa kweli januari sio mbali warudi zao shuleni tu. Yaani inafika mahali hadi kuwaacha pekeyao uende kazini unaogopa unahisi lazima kitanuka tu
 
Kuna vitu watoto wanahatibu hadi unajiuliza huyu dogo amewezaje kuharibu hiki kitu, na nini alikua anatafuta huku? Ila uwezi pata jibu kamwe.

Kitu kingine cha ajabu hawa watoto wa siku hizi hawachoki, kuanzia asubuhi hadi usiku wapo active tu.
Bora warudi shule.
Mbona wakibamizwa shuleni mnapiga kelele?

Hizo ni wiki 2, hujamaliza mwezi. Tulia, hayo ndo machungu ya kulea.
 
Ni vizuri mtoto akiwa mchangamfu, muda wake bado ubongo unahitaji vitu vingi katika ukuaji, labda cha kukushauri hapo mpunguzie kiwango cha sukari hasa muda wa jioni/usiku.

Sukari namaanisha za candy, chocolate, soda na vingine kama hivyo.
 
Back
Top Bottom