Nimeshazichoka vurugu za watoto, bora shule zifunguliwe

Nimeshazichoka vurugu za watoto, bora shule zifunguliwe

Kupunguza kero najifanya naumwa ili watulie walau kidogo... Sofa wamevunja, nimewapambia kamti ka krismas kamenyofolewa kote sebule iko Kama karakana
Wakwangu huwa haharibu vitu, wee anajua mziki wake, atapata adhabu hata ya kufagia uwanja. Si endekezaji mtoto mimi. Sasa hivi wanacheza mpira na wenzake au michezo mingine nje. Ndani marufuku, anaangalia katuni kwa adabu zote bila kuharibu. Hata mtoto wa mdogo wangu akiwepo wanajua hakuna kuharibu vitu.
 
Huu ni muda mzuri wa kukaa na watoto na kuwafundisha majukumu madogo madogo Kwa ajili ya Maisha Yao ,asubuhi kama kuna nguo Zao chafu waelekeze wafue Hata kama Sio Kwa usahihi lakini watajua mdogo mdogo Hata kama una mashine Yako ya kufulia wao wafue Kwa Mikono ukiweza fua nao Ili wajifunze Kwa vitendo,waoshe vyombo,kufagia,kudeki,lima nao,panda nao ,uza nao kama una biashara n.k usilee watoto kama Mayai mbeleni wataishi vibaya Hata akitaka kwenda Kwa ndugu kila Mtu atamkataa Kwa sababu hakuna anachoweza.
Mpangie ratiba ya kila siku na majukumu yake,kila kitu afanye Kwa kiasi Sio kuanzia asubuhi Mpaka jioni mtoto ni kuzurara afanye kazi Kwa kiasi na acheze Kwa kiasi usimuachie sana na usimfungie sn
 
Bado kula sana na kila dakika ....akiingia juice akitoka ndizi .....akipakua huwezi amini atamaliza
🤣🤣🤣 Tabu Tu! wako wawili mdogo NI baunsa na mkubwa nae baunsa hakuna anaekubali kushindwa, kila baada ya Dakika 2 au 3 utasikia kimewaka! Unabaki kukemea Tu, na adhabu nafukuzia kwenda kulala ata iwe saa 5 asubui
 
Back
Top Bottom