Nimeshazichoka vurugu za watoto, bora shule zifunguliwe

Nimeshazichoka vurugu za watoto, bora shule zifunguliwe

Mzazi ni mzazi,na wote tumepitia,ila siyo siri utoto noma. Hapa yapo mapacha yana vituko,hadi unajiuliza hawa watakuwa waache? Jiko likiwashwa,anamwagia maji,anakimbia. Laptop,kamwagia maji. Wakianza kujipaka mafuta ya kula utatamani wahame kabisa. Ila hata hivo walau mtu anavuka hasira anacheka tu. Na kwa hilo,kama mama home anajielewa na ndo anabaki nao, ni wa kumheshimu. Kama wanabaki na msaidizi wa kazi,ndo ujiulize mshahara wake ni sawa na kazi anayoyifanya?
 
Kuna vitu watoto wanahatibu hadi unajiuliza huyu dogo amewezaje kuharibu hiki kitu, na nini alikua anatafuta huku? Ila uwezi pata jibu kamwe.

Kitu kingine cha ajabu hawa watoto wa siku hizi hawachoki, kuanzia asubuhi hadi usiku wapo active tu.
Bora warudi shule.
Tukiwaambia mtupatie jero zenu tukae nao tuwatie makwenzi kidogo mnalalamika walimu tuna njaa. Mzazi tulia tu wavunjeee na Januari tunataka ada🤣🤣🤣

Evelyn Salt kumeanza kuchangamka huku🤣
 
Huu ndio mda wao kwenu wazazi kuwafundisha maadili mema kiasi wapo na nyie
Watoto wanahitaji mafunzo na maisha pia
Toka nao kazunguke hata farm au hata maeneo yoyote na wafundishe kujikinga na hatari
Huko shule wanajifunza mambo mengi henda hata mabaya pia kutoka kwa watoto watukuta
Kwa hiyo ni wajibu wako kuwapa darsa la maisha
Ndio mda wako huo
Ukitaka liache liende tu
Is up to you
 
Back
Top Bottom