Nimeshazichoka vurugu za watoto, bora shule zifunguliwe

Nimeshazichoka vurugu za watoto, bora shule zifunguliwe

Kuna vitu watoto wanahatibu hadi unajiuliza huyu dogo amewezaje kuharibu hiki kitu, na nini alikua anatafuta huku? Ila uwezi pata jibu kamwe.

Kitu kingine cha ajabu hawa watoto wa siku hizi hawachoki, kuanzia asubuhi hadi usiku wapo active tu.
Bora warudi shule.
Ngoja Mungu atakapoamua kukupunguzia hizi Kero kiaina ndiyo utajua ulikuwa unalalamikia upumbavu!
 
Hii likizo nimekuwa mlinzi watoto hawasikii wamekata miche yangu wazazi wao wanawaangalia Tu hawagombezwi na likizo ilivyo ndefu mpaka mwezi wa pili Kazi ipo
 
Kuna vitu watoto wanahatibu hadi unajiuliza huyu dogo amewezaje kuharibu hiki kitu, na nini alikua anatafuta huku? Ila uwezi pata jibu kamwe.

Kitu kingine cha ajabu hawa watoto wa siku hizi hawachoki, kuanzia asubuhi hadi usiku wapo active tu.
Bora warudi shule.
Mi wameenda kwa bibi
Huyu wa kiume alivunja vase ya maua ile ya mbao
Mpaka sasa najiuliza alitumia dhana gani
Alibeba tindo au alipiga chini
Na kwa nini sasa?
Aiseeee madogo ni noma
 
Huwa nawashangaa sana wanao-wish kuwa na mapacha humu ndani, ni wasumbufu sana yaani.
Mzazi ni mzazi,na wote tumepitia,ila siyo siri utoto noma. Hapa yapo mapacha yana vituko,hadi unajiuliza hawa watakuwa waache? Jiko likiwashwa,anamwagia maji,anakimbia. Laptop,kamwagia maji. Wakianza kujipaka mafuta ya kula utatamani wahame kabisa. Ila hata hivo walau mtu anavuka hasira anacheka tu. Na kwa hilo,kama mama home anajielewa na ndo anabaki nao, ni wa kumheshimu. Kama wanabaki na msaidizi wa kazi,ndo ujiulize mshahara wake ni sawa na kazi anayoyifanya?
 
Back
Top Bottom