Nimeshazichoka vurugu za watoto, bora shule zifunguliwe

Nimeshazichoka vurugu za watoto, bora shule zifunguliwe

Kuna vitu watoto wanahatibu hadi unajiuliza huyu dogo amewezaje kuharibu hiki kitu, na nini alikua anatafuta huku? Ila uwezi pata jibu kamwe.

Kitu kingine cha ajabu hawa watoto wa siku hizi hawachoki, kuanzia asubuhi hadi usiku wapo active tu.
Bora warudi shule.
Ndio Raha za utoto hizo
 
Watoto ni malezi
Nina watoto wa sis wamekuja likizo
Ni watulivu na kazi zote wanafanya
Wanajua kujipangilia na muda wa kucheza wanapata..walikuja watoto wa jirani basi wakipiga kelele tu utasikia usipige kelele aunt atawafukuza hapendi kelele
 
Tusipende kukimbia malezi na kuwafukizia watoto shule..ili walimu wawalee, sisi tubaki na mishe zetu..basi tusingezaa! Kuna raha kulea watoto..kuna kuwa na vipindi vya likizo kwa ajili ya wazazi kulea watoto wao..fujo na hekaheka za watoto ni sehemu ya maisha ya mazazi
 
Hii ndo raha kamili ya kuitwa mzazi hakika kelele zao ni wimbo kwenye maskio ya mzazi sema saa nyingine unahitaji utulivu ila ndohuwezi pata ukiwa nyumbani sababu na wewe lazima ugeuke umri wao ili mwendane sawa,wakiumwa na sisi tunaumwa wakifurahi na sisi tunafurahi
 
Kuna vitu watoto wanahatibu hadi unajiuliza huyu dogo amewezaje kuharibu hiki kitu, na nini alikua anatafuta huku? Ila uwezi pata jibu kamwe.

Kitu kingine cha ajabu hawa watoto wa siku hizi hawachoki, kuanzia asubuhi hadi usiku wapo active tu.
Bora warudi shule.
Kama mzazi unawachoka wanao kwa hadi kusema vipi huko shule mnakotaka warudi? Funzeni watoto good manners
 
Watoto ni malezi
Nina watoto wa sis wamekuja likizo
Ni watulivu na kazi zote wanafanya
Wanajua kujipangilia na muda wa kucheza wanapata..walikuja watoto wa jirani basi wakipiga kelele tu utasikia usipige kelele aunt atawafukuza hapendi kelele
Wamelelewa kwa misingi mizuri
 
🤣 Jana tu nimetoka kusema hili, kuna watoto wa jirani hapa wanakusanya watoto wenzao niambie huo mkutano ni kelele tupu!. mara wapigane mara wacheze kombolela mwengine anaacha kulilia huko anasogea ulipo analia mpk unaona kidaka tonge!.
Ndo anakupa taarifa na ww uzae hahaah
 
Madogo naona wako kawaida tuu ila hapa wanavyo hadithiwa utadhani ni mazombie
Sisi wakati wetu tulikuwa tuna kwea mpka minazi 😄
 
Wakwangu huwa haharibu vitu, wee anajua mziki wake, atapata adhabu hata ya kufagia uwanja. Si endekezaji mtoto mimi. Sasa hivi wanacheza mpira na wenzake au michezo mingine nje. Ndani marufuku, anaangalia katuni kwa adabu zote bila kuharibu. Hata mtoto wa mdogo wangu akiwepo wanajua hakuna kuharibu vitu.
Mama mzuri wewe, watoto wasituendeshe hata kidogo. Wafundishwe namna ya kuishi kwa nidhamu
 
Kuna vitu watoto wanahatibu hadi unajiuliza huyu dogo amewezaje kuharibu hiki kitu, na nini alikua anatafuta huku? Ila uwezi pata jibu kamwe.

Kitu kingine cha ajabu hawa watoto wa siku hizi hawachoki, kuanzia asubuhi hadi usiku wapo active tu.
Bora warudi shule.
Watakuwa wa kiume
 
Back
Top Bottom