DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tafuta wakili mwenye tamaa ya hela fungua kesi ya madai yenye interest rate ya ajabu wakili yake 10% na gharama ya kuendesha kes juu yao uone watu wanavyotajirikaga wakipata loopholes za hivi nendq kawadai 500m
 
Aende mahakamani. Atoe ushahidi. Apate haki yake.

Mimi wala sikuandika kuhusu mleta mada. Wala lingekuwa ni jambo langu nisingekuja JF na nisingedai 27M pekee. Ningedai na fidia ya usumbufu.
 
Tafuta wakili mwenye tamaa ya hela fungua kesi ya madai yenye interest rate ya ajabu wakili yake 10% na gharama ya kuendesha kes juu yao uone watu wanavyotajirikaga wakipata loopholes za hivi nendq kawadai 500m
🤣🤣🤣🙌
 
Umeongea sahihi sana kwenye betting kuna utapeli mkubwa sana, ni vile watu wengi hawashindi wanaona kawaida tu.

Mimi nilishawahi kushinda 17m wakafungia Account yangu, hao Gaming board ni takataka tu hawana msaada wowote
Mkuu ilikuwa kampuni gani?
 
Tafuta wakili mwenye tamaa ya hela fungua kesi ya madai yenye interest rate ya ajabu wakili yake 10% na gharama ya kuendesha kes juu yao uone watu wanavyotajirikaga wakipata loopholes za hivi nendq kawadai 500m
Mkuu unahisi tangu 2024 mpaka leo hajawahi pata hii idea. Kwamba ni ngeni hajawahi ambia mtu yeyote aliyekuwa anayo?

Au unahisi hajawahi sema kwingine ndio kwa mara ya kwanza kaomba ushauri JF?
 
Kwani mpaka betpawa Kuna verification au mpaka ushinde mabilioni ndiyi verification
Kuna verification ukishinda hela nyingi na mechi zenye ukakasi. Inaweza chukua siku mbili hivi, unapiga picha na vitambulisho.

Ukitazama akaunti ya mtu aliyewahi kula hela nyingi iko verified na kwa muda fulani inaweza kuwa limited kwenye stake.
 
Nimekuuliza ili ujibu nikuelewe. Anyway kama hakuna majibu ni sawa tukimaliza kwa style hii ya kuelekezana kwenda mahakamani.
Ndio maana nikasema suluhisho ni mahakamani. Mimi mwenyewe fixed games nimebashiri sometimes hela inarudishwa, sometimes nashinda, sometimes mimi nashinda mwenzangu aliyeweka vilevile anakataliwa anarudishiwa hela yake, sometimes stake kwangu inakataa juu ya 300,000 kwa mwingine inakataa juu ya 120,000. Ila ukibeti ambazo sio fixed unakuta stake ya 2,000,000 inakubali.

Kwahiyo criterias za fixed inajulikana vipi sijui zaidi ya maelezo niliyotoa.

Ila utakuwa unajiumiza kichwa kama unaamini mtu anajua ana haki since 2024 analalamika tu haijafika mahakamani. I can bet 95% hiyo kesi anashindwa na sio kwa kuonewa. Angekuwa wa kushinda angefika mahakamani hiyo 2024 na sio kutafuta sympathy. Suala la gharama na muda si kampuni ileile ingelipa na fidia yake.
 
Hao walioshinda milioni 600 una uhakika walilipwa zote au wanapewa milioni 10 kisha wanawarekodi na kutuma tangazo kwenye TV kuwalaghai watu kuwa mshindi kapata milioni 600.
Sijawahi kuwaamini watu wa mchezo wowote wa kamari uhuni mwingi
 
Duh kumbe kazi yao inahusisha hadi kufanya fitina uwanjani?
Na hii inafanyika hadi kwenye timu za ulaya au ni bongo tu?
 
Hao walioshinda milioni 600 una uhakika walilipwa zote au wanapewa milioni 10 kisha wanawarekodi na kutuma tangazo kwenye TV kuwalaghai watu kuwa mshindi kapata milioni 600.
Sijawahi kuwaamini watu wa mchezo wowote wa kamari uhuni mwingi
Mimi nimewahi kumuona mwalimu mmoja alipiga milion 28 na alilipwa yote hao walikuwa ni sportpesa
 
Tafuta mwanasheria akusimamie jambo lako ndani ya muda mfupi tu utaweka kibunda chako kibindoni.

Tena hapo ukiwa na mwanasheria anajua namna ya kudai hadi fidia za namna mbalimbali ili hata zisipotiki zote lakini zipo zitakazotiki baada ya hoja kukubaliwa na mahakama.
 
Duh hawa jamaa ni wajanja wamejiwekea kinga kuwashinda mahakamani ni shughuli pevu
Ukijiwekea kinga ama vigezo vinavyokubeba wewe tu bila consideration ya upande mwingine ukienda mahakamani itatengua maana mkataba hauwezi kuegemea upande mmoja tu.

Mikataba ina mwongozo wake hata kama mnaingia mkataba watu binafsi bado kuna terms and conditions huwezi kuzikiuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…