DOKEZO Nimeshinda Sh 27M kwenye kubet, Kampuni inataka kunipa Sh 3M, Gaming Board hainisaidii

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Na kwa nini yote hayo yatokee kama mhusika ana haki ya ushindi πŸ˜‚?
Kwamba TGB na Pigabet wajinga sana mpaka wapoteze muda wao kukaa na mtu asiyestahili kulipwa?
 
Una uhakika gani? Je kama aliscreenhot mapema kama ushahidi wa lolote linaloweza kutokea? Halafu kumbe hujaelewa mtoa mada anazungumzia kufutwa kwa mkeka baada ya kushinda na sio wakati game zikiendelea
Wewe ndio hujaelewa pengine umeangalia juu juu. Kabla ya mkeka kuwini kunanaesha screenshot na kiwango atakachoshinda. 2. Kuna screenshot imepigwa baada ya mkeka kukamlika na kuwa haujashinda na dau limerejeshwa sasa hapo mkeka umefutwa katika hatua gani katika hizo mbili ikiwa mkeka kabla ya kushinda anazo taarifa. Na mkeka baada ya kikamlika anazo taarifa? Fungua ubongo kijana ,, mkeka kufutwa nilabda baada ya matokeo asingeuona mkeka huo kwamba umefutwa ilihali umeshinda
 
Kampuni za michezo ya kubahatisha hua zina maximum amount watakayokulipa hua wanaiweka kwenye terms and conditions. Mfano maximum amount ni 15M ukishinda 16M wanarudi kwenye terms and conditions na kukulipa waliyoisema.

Ubaya ni kwamba, hawatokataa betslip uliyoweka ambayo inavuka maximum amount ila ukishashinda ndiyo unapitishwa kwenye terms and conditions.
 
Huyo member anaongea logic na taratibu zilivyo lakini kwenye hii ishu hakuna logic wala taratibu.

Kama ushindi ungekua una shida ilibidi watoe ushahidi na kugomea kumlipa.

Kama terms and conditions zinasema maximum amount ni 3M ilibidi watoe hiyo hoja kwa gaming board.

Kisha gaming board ingetoa maamuzi ya kwamba mleta uzi alipwe 3M kwakua ndiyo maximum amount.

Mleta uzi angefika mahakamani na kumbukumbu zingeonyesha kwamba gaming board ilifanya maamuzi.

Mahakama ingejaribu kuona kama maamuzi yalikua sahihi ama la.

Lakini kwa scenario aliyoeleza jamaa hapa kuna upuuzi upande wa gaming board na upande wa kampuni.
 
Kwa kampuni ninazo zijua zenye maximum payment kiwango kitakachoonekana kwenye mkeka ndicho utakachoshinda na kulipwa,, ukizidisha timu utalipwa kiwango hicho hicho kama utashinda na kuongeza timu hakutapandisha maximum payment. Kampuni nyingine hawakuruhusu kuzidi hicho kiwango walichoweka kama umeweka odds nyingi watakulimit kwenye stake unaweka. Kampuni nyingine wana limit kwenye Stake pesa unayoweka kwa mkeka husika au timu zisizidi 50 ,, kampuni nyingine unaweza kuweka kiwango chochote mradi huvuki timu hamsini na hawakulimit kwenye kiwango utakachoshinda isipokuwa wanakulimiti kwenye option utakazo chagua . Lakini kwenye mada mkeka wake haujapewa hata huko kushinda kwenyewe na bado 27 M haiwezi kuwa limit hata kama kampuni ni ndogo kiasi gani ( Japo miaka ya nyuma mbet waliwahi kuwa na kiwango cha chini)

kwasababu kwenye betting huwa kuna mtaji unatakiwa uufikie ndipo upewe leseni ndio maana unaona sio rahisi kukuta watanzania wanamiliki kampuni za betting kwasababu inahitaji mtaji mkubwa na operation zinazohitaji fedha nyingi tena At risk
 
Kama ni mambo ya maximum payment kwanza hapo walitakiwa wampe win kwenye mkeka na wachukue dau lao na alipwe na malalamko yangekuwa kwanini amelipwa kiwango kidogo na jibu liwe alivuka maximum payment.

Tatizo hapo mkeka timu zimeshinda lakini hajapewa ushindi kwenye mkeka na hapa lazima wampe majibu yanayoeleweka
 
Kampuni ina omba mungu πŸ˜„
Ila kamari mambo yake yana endeshwa kikamari kamari
Kwenye T&C zao unakuta wanasema wana uwezo wa kufunga AC wanapo ona inafaa au kukulipa kile wanacho ona kinawafaa wao sasa si balaa hilo
Hizo T&C ndo wanaztumia kampuni uchwara uchwara kama hao piga Nini sjui kupiga watu ..
Kampuni inakuibia mpaka stake ya buku3 unategemea wakulipe millions ..
 
Unazurula zurula tu kifupi kampuni lenu ni la kitapeli na haliaminiki
 
Oya mzee Kaza wakupe pesa zote, hao gaming boards n kama vile wamepewa pesa wakukatae, ukishindwa kabisa fanya namna utegeshe bomu kwenye ofisi zao ili wote mle hasara kmmk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…