Habarini wakuu,
Kama kichwa kinavyosema hapo juu, Uraibu ya kujichua (punyeto) sio rahisi kuushinda hasa pale unapokuwa huna mahusiano, domo zege, mpenda ngono na mtazamaji wa ngono film, mtu wa kupenda kujitenga sana wale wa kujiita introvert sijui n.k (hayo ni makundi ambayo yapo on top kwenye kuizagamua mikono yao).
Halafu nyeto ni roho ya ajabu kweli yaani, kama umezoea kujichua na mkono wa kulia basi siku ukijaribu kujichua na wa kushoto basi inakuwa kama umechepuka vile yaani.
Kiufupi nyeto inahitaji dhamira ya dhati kuiacha nje na hapo omba rehema za Mungu au jaribu kuwa na mahusiano na mtu ambae kama ukihitaji anytime akuchanii mkeka itakusaidia kupunguza makali au kama hujaathirika sana basi utaacha, utakuwa hujaishinda punyeto bali umepumzika.
Mimi msoto nilioupitia kuacha hii kitu na huku bila kuwa na mahusiano ni Mungu tu anajua, yaani akili haisomi sometimes hisia zipo to the highest zinanichochea japo nifanye ngono na mwanamke yeyote ila kidume nikadhamiria kuzituliza hizi hisia za kichochezi za kimwili zikae chini yangu kunisikiliza mimi.
Hadi sasa nathibitisha nimeishinda kabisa, 3yrs sio poa halafu ukizingatia nilikaa 1.5yrs bila kufanya mapenzi kabisa basi nathubutu kusema nimeishinda hii kitu. Ila nimechafua mashuka na boxer sana, yaani inafika hatua kwenye daladala umekaa na mwanamke pembeni akigusa kidogo hivi kutokana na mneso wa gari basi akili inavurugika kabisa, ila asante Mungu muweza wa yote.
Nakupa mbinu chache ambazo nazifanya kuvishinda vichocheo hivi vya kufanya ngono au kujichua. Ili kama na wewe ni muanga wa hizo mambo ukapitie kwa nia dhati na hakika itakusaidia.
Ya kwanza: Nimekuwa mtu wa kutokuyapa macho yangu kutaza vitu vinavyoweza kunifanya nitamani kufanya mapenzi mf: Porn Videos, Wadada wanaokaa uchi kwenye mitandao na wakata mauno, yaani ikitokea nimeplay au kuhisi whats next basi naskip fasta, sina company ya washkaji ambao 24/7 ni stori za wanawake na kuwala.
Ya pili; Mazoezi, Hapa nimegundua miili yetu wanaume inapaswa kuumia, yaani ukiupa mwili muda wa kurelax sana unajitengenezea uchochezi wa kuhitaji kukanda, so hapa nahakikisha nikianza kuhisi dalili tu za mwili kuhitaji basi napiga push ups zangu 20 nikiamka hisia zote zimepotea. Pia before kulala make sure unafanya mazoezi ili ukiingia kitandani tu kutokana na uchovu basi utalala kwa haraka.
Nyingine niwape mbinu wale ambao mnadinda dinda hovyo wakati mwingine sehemu zisizo rasmi jambo ambalo linawafanya mkose confidence kusimama, ikitokea hali hiyo bana pumzi usipumue kwa sekunde 15 kisha vuta pumzi moja alafu ubane kwa sekunde 15 ukija kuachia uume umelala yaani unakuwa umeutuliza uume ndani ya 35sec kisha confidence yako inarudi.
Ya tatu: Mikono isipende kushika sehemu zako za siri au pia usipende kujitazama sana maungo yako au muonekano wa mwili wako kwenye kioo, itakuchochea kutaka kuona mengi zaidi ya hiyo mikono, six packs na kifua.
Ya nne: Jiweke karibu na Mungu itakujenga kiimani na kukupa nguvu ya kuzidi kupambana kuishinda tabia hiyo mbaya.
Mungu nimemuweka kwenye hatua yangu ya mwisho kwa kuwa alishatuhasa kwamba dhambi ya uzinzi haikemewi bali inakimbiwa, so anza kwanza kuiepuka kwa hatua hizo tatu za mwanzo kwa nia moja kisha ongezea na Mungu unatoboa.
Shukran sana.