Nimeshindwa kusema uongo kwa kisingizio cha uzalendo

Nimeshindwa kusema uongo kwa kisingizio cha uzalendo

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2018
Posts
5,636
Reaction score
8,777
Wandugu; kuna inquiry kutoka nje (mimi ni mwanachama kwenye forum fulani inayojihusisha na investments kwenye agribusiness na SMEs). Kuna potential investor ameniuliza maoni yangu - akinukuu alichosema Dangote miaka miwili iliyopita na kuhusu maneno yasemwayo na watawala wetu - kuhusu hali ya uwekezaji hapa nchini kwa sasa.

Anataka kuwekeza kwenye food processing. Nimeshindwa kumpa maneno matamu ili aje awekeze (kumbuka kuna uwezekano wa mimi binafsi kufaidika na yeye kuwekeza hapa). Nimempa facts zifuatazo:

1. Huwezi ku-predict sasa hivi kuwa serikali itafanya nini katika mazingira yeyote
2. TRA wanaweza kukudai kiwango chochote cha kodi watakayojisikia (na ili ukate rufaa ni lazima ulipie theluthi moja ya hicho walichokuambia kuwa wanakudai; na hata ukishinda rufaa hawarudishi ulicholipa).

Nimemshauri asubiri angalau miaka 5 ijayo kunako majaaliwa tuone hali itakuwaje.
Mataga mnaruhusiwa kunitukana muwezavyo; LAKINI huo NDIO Ukweli halisi.
 
Huo ni ukweli kama wewe unavyouona ila si wote tunaona uonavyo.
 
Mtumie huu mchoro wa kipanya unaoonyesha hali halisi ya Tazania kwa sasa!
masoudkipanya_B9OFAe2DHHu.jpeg
 
Huo ni ukweli kama wewe unavyouona ila si wote tunaona uonavyo.

Najua kuwa kuna wengine mmeamua kubuni "ukweli" wenu wenyewe na mnauamini. Bahati mbaya kwenu; investors' confidence haitokani na imagination but hard facts. Na baadhi yake ndizo hizo nilizozianisha. Sasa wewe na wenzio njooni na ushahidi kuthibitisha kuwa nilichokiandika si kweli.
 
Siyo wote mambumbu humu ndani.
 
Hongera kwa kuwabania watz wenzako riziki

Ingewasaidia nini hao Watanzania wenzangu kwa mimi kumdanganya huyo mtu ili aje na hatimae akute hayo niliyomwambia kabla? Najua kuna watu msiojua thamani ya kusema ukweli, mimi najua. Sijamkataza kuja, akiamua kuja pamoja na yote niliyomweleza mbona anakaribishwa tu. Na nitampa ushirikiano wa kutosha.
 
Wee muongo mkubwa si wote na nani! Huo mkutano wa kukubaliana kuwa si kweli mliufanya wapi! Sema wewe na si wote mnakubaliana naye.
Nasikitika kwa kutoelewa nilicho andika ila nafarijika sana kufahamu humu jamvini kuna wengi wameelewa.
'To keep silent when you can say something wise and useful is as bad as keeping on propagating foolish and unwise thoughts'
 
Ingewasaidia nini hao Watanzania wenzangu kwa mimi kumdanganya huyo mtu ili aje na hatimae akute hayo niliyomwambia kabla? Najua kuna watu msiojua thamani ya kusema ukweli, mimi najua. Sijamkataza kuja, akiamua kuja pamoja na yote niliyomweleza mbona anakaribishwa tu. Na nitampa ushirikiano wa kutosha.
Huoni kuwa wangepata ajira?
Kwani hawa waliopo wanajiendeshaje? Au wao hawakuambiwa ukweli... Na mbona bado wapo hawaondoki kama hali ni mbaya kiasi hicho?
 
Mfiaukweli,
Wambie ukweli kwamba 'there is policy uncertainty' tuna sera za majukwaani nyuma ya mikamera ambazo zimesababisha biashara nyingi zifungwe 'you ca not plan growth of business with policy uncertainty'
 
Miaka yangu 20 kwenye ajira nimefanya na wewekezaji na kwa sehemu ndogo serikalini kupitia taasisi zake.... Ni lazima kuwa wakweli pamoja na nia ya dhati ya kubana mianya ya rushwa lakini kuna mahali tumekosea hasa kwenye usajili wa biashara na kupata viambata muhimu na eneo zima la Kodi
Kuna utiriri wa nyaraka, kuna utiriri wa kodi kuna utiriri wa michakato ambayo mingine inaingiliana... Kwa mfano USALAMA kazini kuna vitengo vitatu vinafanya kitu kinachofanana OSHA, FIRE na NEMC...
Ukifungua Hotel leo hii kuna kodi zisizopungua 33
Ukiwa na kampuni yako ya uzalishaji watakuja
NEMC
FIRE
OSHA
MUNICIPAL
TMDA
TRA
NSSF
TUICO
nknk

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom