Nimeshindwa kuvumilia, naomba msaada wenu jinsi ya kuachana na mzazi mwenzangu

Kuna watu wanahoji sababu nadhan umeshaziweka wazi hapo ingawa mengine mengi hujayaeleza

Ila nikwambie kitu kimoja km umeteleza ukamtia mimba huyo ni wako haijarishi ni mshirikina au ana kiburi na mengineyo ila huyo ni wa kwako kwa hio nenda nae sawa angalia yeye anataka nini kile ambacho una uwezo nacho mfanyie usichokua na uwezo nacho usimfanyie

Nitakupa mfano wa mwanandoa mmoja ni ndugu yangu, yeye kuna kipindi alikua ana shida ya km 2 Million, aliekua anataka kumkopa akamwambia njoo uchukue nyumbani kwangu zipo, Jamaa akaongea na mkewe akamwambia anaenda kuchukua/kukopa 2 Million kwa mtu fulani kwa ajili ya matumizi ya hapo nyumbani, mwanamke akamwambia km anataka kwenda kwa mahawala zake kwa gia hio hataki aende popote akiondoka tu ajue na yeye akirudi hamkuti,

Basi Jamaa ikabidi apige simu aeleze kwamba zile pesa hatozifuata akaulizwa imekuaje akasema mkewe amesema asiende kuzichukua kwa hio amechukua maamuzi hayo ili kuepusha Shari,

Ndoa nyingi unazoziona zinaendeshwa kisharishari yaan linazushwa jambo la ajabu tu ambalo hukulitegemea anytime anything can happen mda wowote kinaweza kikanuka

Tukija kwenye suala la mtoto, inaonyesha wazi weewe ulikua unataka kujipooza tu na sio kuzaa na huyo mwanamke, sasa imekuaje umeanza kuganda unamtaka mtoto awe wa kwako peke ako na sio mtoto wa kwenu wewe na yeye?
Hapo ndipo ninapokosa uelekeo

Nitarudi tena mkuu..
 
Yani mkuu niliyoandika hapa yanastahili kuandikwa Kuna majanga mengi nimeamua kufukia. Mfano Kuna kipindi alisema pesa ninayompa haimtoshi(200k Kwa mwezi) wakati huo nyumba nalipa Mimi Kodi yake na baadhi ya vitu vya msingi Kama mchele, sukari, mafuta, gas Kuna sehemu nilishamlink vikiisha analetewa Mimi natuma hela Kwa hao watu Kwa wangu.

Basi nikaona isiwe tabu Kuna acc nilikuwa naweka vipesa vyangu vya madeal kadhaa nikampa Ile kadi kwamba hela ikiisha utaenda kutoa humo ili umalize matatizo Yako.

Aisee sijui alijenga huyu mtu? Kuanzia mwezi Jana tareh Kama 10 mpaka juzi tarehe 9 mwezi huu nilivyokwenda kuchungulia acc kidogo nizimie.
 
Duh! Ulimpa hadi card ya bank aisee
 
Tundika Daluga kwa muda mkuu,mpe muda mtatafutana huko mbeleni
Niliwaza hivi ila... Namfikiria sana huyu dogo. Na hawa wanakujaga kusema walitelekezewa watoto na mengine mengi. Ila muda unavyozidi kwenda Kuna kitu nitaamua tu hakuna namna.
 
Waambie ndoa imenishinda bas,maana taarifa ni muhimu sana
Kifupi hatuna ndoa na Kila mtu anaishi kivyake ila nahudumia Mimi hiyo familia ya yeye na mtoto.
 

Leta majibu haya kisha nikupe way forward:
1. UNAMPENDA? kwa moyo wako na unadhani uko tayari kuishi naye?

2.Una uhakika na hayo mambo ya kilozi/uganga uliyosema?

3.Mmewahi kuongea kwa uwazi nini hasa tatizo maana isije ikawa mtoto wa watu anakupenda hadi hawezi kuishi bila wewe?

4.Wakati mnaanza uhusiano plan zako zilizkua ni zipi?

5. Iwe mvua au jua kama mtoto ni wako angalia namna nzuri ya kutoa matunzo .

Kila la heri
 

Mkumbushe kua utatunza mtoto, pia ajue wazi wewe HUTAOA!
 
Story ipo nusu sasa hilo tatizo la kukushauri lipo wapi hapo?

Ila usimuache mtoto wako wala usije ukakubali alelewe na baba mwingine lazima baadae ujutie
Mtt hawezi kuwa fimbo ya kunichapia hata siku moja,mzazi mwenzangu akizingua sitaangalia eti tuna mtt,acha niwe baba jina tuu
 
Tafuta anamna mtoto kumchukua sasa huwezi. Hata huyo mzazi mwenzio bila shaka ni mwanamke na yeye anampenda mtoto maana kambeba tumboni miezi 9. Usijiwazie wewe tu kuwa ndo una haki na unastahili mtoto kuliko aliye mbeba tumboni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…