Nimeshindwa kwenda kumzika Mama haya maisha hayako fair naombeni msaada😭

Ni kweli wengi wetu ni tia maji ila humu scammers wengi sana, sio kwamba hatutaki kusaidia ila trust me humu kuna mambo sana...utapeli nje nje!
Lakini fikiria mtu hadi anasema ili kuondoa utata wa utapeli nikatieni tu tiketi

Bro haya maisha mimi yananiumizaga sanaa hayako fair hata kidogo soma maoni uone masikhala wanayofanya
 
Shida unaweza ukatuma kumbe kafa mbuzi au kifo hewa
 
JF imefikia huku kwa kua na omba omba, twafa. From Great thinkers hadi kufikiw a na ma omba omba. Nimeamini dunia duara.
Ndo nimeingia online nakutana na mleta uzi kapatwa na tatizo ambalo Kila binadamu likimtokea lazima litamuumiza mara ghafla nakutana na fala fala kama hili linaandika upuuzi wewe kweli MAKU.

Hivi umelazimishwa kutoa mkuu?? Na mhusika mwenyewe kasema kama humuamini basi mkatie tiketi online kisha ongea na agent kama abiria kapanda. Hivi watanzania mnakuwa wajinga wajinga kiasi hiki
 
Niliwahi kutapeliwa na rafiki wa kaka yangu kuwa anawenda msibani Dar tukitokea Tanga, nikamlipia nauli na kumpa pesa ya mlo njiani kumbe anakwenda kwa mwanamke Sinza
wewe mleta uzi hili liwe funzo, unaona hii komenti? Hii ndio 99% ya watu watu wa humu tutakuletea mastory ya kifala fala tu na msaada hupati

Next time utajifunza nenda facebook wanapopabeza kule msaada ni mkubwa hujawahi kuona popote pale

Humu tumejaa majuaji na mamasikini tu
 
Amekutapeli nini? mbona kama umeumia yeye kupata msaada? Bahati ya mwenzio usiilalie boxer wazi
hakuna mtu anae muonea wivu,ana thread zake nyingi na comment nyingi za kuomba pesa.
Nimeanza nae mbali tangu page ya 2.
Ina maana kila siku yeye ndio mwenye shida!!
Mwambie apambane sio kuomba omba misaada kila wakati
 
Lakini fikiria mtu hadi anasema ili kuondoa utata wa utapeli nikatieni tu tiketi

Bro haya maisha mimi yananiumizaga sanaa hayako fair hata kidogo soma maoni uone masikhala wanayofanya
Nyakati ngumu mwanaume usipende kutia huruma, shirikisha akili. Kama Melo hawezi ku'verify hii kitu wewe unaaminije kirahisi, una pesa nyingi sana za kutoa hovyo?
 
Kuna watu wanakatiwa ticket wanaenda kuuza magufuli tena kwa bei pungufu nimekutana nao sana
Hilo linakuuma? Shilingi elfu 90 inakuuma.

Tiktok watu wanaingia Live wanasaidiana kwa saa 1 tu tena vimtu vidogo dogo tu vina raise hadi million 5 alafu hawana muda na wewe anakuja mwingine naye anasaidiwa

Hawahitaji uthibitisho wowote as long as umeeleza shida na watu wanazijua shida kwa sababu wameziishi
 
Kwa akili zako hii unaiita bahati? Kwa hiyo mtu kufiwa na kuchangiwa nayo ni bahati? Ondoa Dr kama initial yako.
Kuitikiwa na watu kwenye jambo lako ni bahati, sio wote wana hiyo karama, kumuita mtu tapeli bila kuthibitisha utapeli wake ni upumbavu wa hali ya juu, kilichokupanikisha hapo nini umelazimishwa uchangie au ujuaji usio na maana
 
Nyakati ngumu mwanaume usipende kutia huruma, shirikisha akili. Kama Melo hawezi ku'verify hii kitu wewe unaaminije kirahisi, una pesa nyingi sana za kutoa hovyo?
Maxence ni nani yani kwenye shida za watu yeye nani?

Amewahi kushinda njaa? Amewahi pigwa na maisha haelewi anatokaje na akaja kuwa rescued na watu baki?

Oya we jamaa huyo max wenu hapa namkataa mimi nasaidia watu sanaa na sijawahi weka doubt kwao na uwezo wangu huu huu mdogo sana

Eti nauli tu ya bukoba umwite Maxence mello WTF
 
Na Mimi nakazia WHO IS MELLO BY THE WAY😡😡maaaarakapiiii
 
hakuna mtu anae muonea wivu,ana thread zake nyingi na comment nyingi za kuomba pesa.
Nimeanza nae mbali tangu page ya 2.
Ina maana kila siku yeye ndio mwenye shida!!
Mwambie apambane sio kuomba omba misaada kila wakati
Sasa ngoja nikwambie kitu David, kuomba omba na utapeli ni vitu viwili tofauti, huenda bado shida zake hazijatatuliwa maana watu wanampa vijipesa tu hawampi kazi, hebu mpeni mchongo wa kazi halafu tuone kama atakua omba omba
 
ULichoongea ni sahii hapa ni story tu utakula kwako
Jamiiforum hata useme utangaze biashara ni ngumu sana kupata wateja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…