This is old news. Huwa mnaangalia nini online kama ulikua hujui Hilo siku zote?
Unaposikia nchi zenye uchumi mkubwa Africa unadhani ni nchi gani na kwa kiwango gani?
Mimi nakushangaa wewe ulikua hujui Hili all this time. Punguza kuangalia X mitandaoni.
Mkuu, si sawa kufikiri hivyo.
Nakuomba uwe mtu mwenye nature ya kujifunza na kufundisha, usiwe mtu mwenye nature ya kudharau. Nature ya kudharau inaweza kuku cost maisha.
Mtu mwenye nature ya kujifunza anaweza kujifunza popote, hata kwenye mambo ambayo ukiyaangalia kwa juu unaweza kuyaona ni ya kijinga.
Na mtu mwenye nature ya kudharau, hata akipata nafasi kubwa sana ya kujifunza, ataendekeza dharau.
Mimi nilikuwa najua habari hizi kwamba Nigeria imeipita Tanzania kwa GDP siku nyingi, ila mtoa mada kachokoza mjadala ambao umenifanya nisome article ya Joseph Stiglitz, Nobel laureate wa Economics 2001, iliyoongelea mapungufu ya GDP kwa kumnukuu mtu aliyebuni concept ya GDP, Simon Kuznets, Nobel Economics 1971.
Ingawa nilikuwa najua kwa muda mrefu jinsi wachumi wanavyoonesha mapungufu ya GDP kama kipimo cha uchumi, nilikuwa sijasoma hii article, sijajua kwamba GDP imebuniwa na Simon Kuznets, na sijajua kuwa hata huyo mtu aliyeibuni GDP alionya kwamba GDP haifai kutumiwa kama kipimo cha uchumi. Mada hii imenifanya nisome zaidi na kujifunza yote hayo.
Unaweza kufuatilia hiyo article ya Joseph Stiglitz katika post yangu #185 kwenye thread hii.
That's what JF is all about. Kuchokoza na kupanua mijadala.
Tumeanza kwa mtu kushangaa Nigeria imeizidi Tanzania kwa GDP, tumefika mpaka kujadili kama GDP inafaa kuwa kipimo cha uchumi kwa kuangalia maandiko ya nguli wa uchumi waliopata nishani za Nobel, Siglitz na Kuznets.
So, namshukuru mtoa mada kwa kuchokoza mjadala huu.
Hapa kuna watu wana miaka 70, na wengine wana miaka 14.
Sasa, kama wewe ulijua hii habari miaka 40 iliyopita, kwa sababu una miaka 60, hutakiwi kushangaa ikiwa kuna mtu ana miaka 14 anajua hili leo.
Unatakiwa kumuongezea vitu vingine ambavyo havijui.
Juzi nimeona kuna mtu kaanzisha uzi hapa JF, amekuwa so excited kagundua kitu kinaitwa podcasts Spotify, anauliza podcast ni nini?
Mimi nimekuwa nafuatilia podcasts kwa zaidi ya miaka 15 sasa.
Wala sikujisikia kumzodoa huyu mtu na kumwambia wewe mbona mshamba ndiyo unajua podcasts leo?
Kwanza hata sijui ana umri gani, inawezekana ni mdogo ndiyo ana explore internet, inawezekana ni mkubwa ila hakuwa na nafasi ya kujua podcasts.
Nilichofanya ni kumjibu na kumueleza tu podcasts ni nini, zina faida gani, anaweza kuzipata vipi, mfano wa podcasts na sofware zake. Na yeye akajifunza. Nilipata furaha sana kuona mtu ana experience kujua podcasts kwa mara ya kwanza.
Wala sikujisikia kusema "wewe ndiyo unajua podcasts leo wakati watu tumezijua miaka 15 iliyopita?".
Unaweza kusema hivyo halafu mtu akakwambia "Mzee usichukulie miaka 15 poa hivyo, wengine miaka 15 iliyopita tulikuwa hatujazaliwa bado" 🤣🤣🤣
Uzi uko hapa.
Habar wakuu, mimi ni mgen kidogo kwenye matumiz ya app ya spotify Ninachofaham ni ku search nyimbo na kuiskiliza , mbaya zaidi ninapochagua nyimbo unakuta nikii play ina play nyimbo nyingine Ukiachana na hiyo kuna kitu kingine nimekutana nacho kinaitwa podcast sasa naomba nifahamishwe nini...