Nimesikitika baada ya kuona Nigeria ina GDP karibu mara tano ya Tanzania

Nimesikitika baada ya kuona Nigeria ina GDP karibu mara tano ya Tanzania

Canada wako milioni 40, Korea Kusini million 50, Finland milioni 5 na yote haya ni mataifa bora sana

Pakistan wako milioni 230, Bangladesh millioni 170, Ethiopia milioni 120, DRC milioni 100 na yote haya ni mataifa ya hovyo tu.
Huwezi kuiita Ethiopia Taifa la hovyo wakati wanamiliki shirika la ndege bora dunia nzima likiongoza.

DRC huwezi kuiita Taifa la hovyo wakati wana madini aina nyingi tu tena yale bora kabisa yanayotumika kwa ajili ya viwanda nyeti.

Wingi wa watu ni mtaji ambao hata maneno matakatifu yanaunga mkono. Kinachopatikana huko Canada, Korea Kusini na Finland na kukosekana Bangladesh na DRC ni uongozi bora, kile ambacho Mwalimu Nyerere alikiita siasa safi.

Vinginevyo ni mataifa yenye kila sababu ya kuwa na uchumi unaopaa.
 
Si kuna mtu amesema ukiwa na population kubwa unakuwa na GDP kubwa? Vipi kuhusu Singapore, vipi kuhusu Luxembourg, vipi kuhusu South AFRICA, au Algeria, haya kuhusu Egypt au hawa nao waliwaibia. Talk about substance, siyo mnaongea pumba.
Hii point kubwa.
 
Kinachokusikitisha ni nini? 60% ya Uchumi wao unategemea Mafuta na hao ndio Wanaongoza Kwa mafuta Afrika unategemea nini?

Unadhani wangekuwa wanategemea mahindi na migomba na Madini ya kubahatisha bahatisha Kwa idadi Ile ya watu wangekuaje?

Mwisho mlaumuni Baba yenu wa Taifa Kwa ujamaa wake wa miaka 25 ambao hakuna Cha maana ulisaidia as far as economy is concerned.
Ukikaa chini ukafikiria haya yote chanzo ni nyerere, hasa hapa kwenye lugha tu ndo alipo jaribu jumla
 
Huwezi kuiita Ethiopia Taifa la hovyo wakati wanamiliki shirika la ndege bora dunia nzima likiongoza.

DRC huwezi kuiita Taifa la hovyo wakati wana madini aina nyingi tu tena yale bora kabisa yanayotumika kwa ajili ya viwanda nyeti.

Wingi wa watu ni mtaji ambao hata maneno matakatifu yanaunga mkono. Kinachopatikana huko Canada, Korea Kusini na Finland na kukosekana Bangladesh na DRC ni uongozi bora, kile ambacho Mwalimu Nyerere alikiita siasa safi.

Vinginevyo ni mataifa yenye kila sababu ya kuwa na uchumi unaopaa.
Tatizo ni uongozi tu, hakuna kingine.
 
This is old news. Huwa mnaangalia nini online kama ulikua hujui Hilo siku zote?

Unaposikia nchi zenye uchumi mkubwa Africa unadhani ni nchi gani na kwa kiwango gani?

Mimi nakushangaa wewe ulikua hujui Hili all this time. Punguza kuangalia X mitandaoni.
Mkuu, si sawa kufikiri hivyo.

Nakuomba uwe mtu mwenye nature ya kujifunza na kufundisha, usiwe mtu mwenye nature ya kudharau. Nature ya kudharau inaweza kuku cost maisha.

Mtu mwenye nature ya kujifunza anaweza kujifunza popote, hata kwenye mambo ambayo ukiyaangalia kwa juu unaweza kuyaona ni ya kijinga.

Na mtu mwenye nature ya kudharau, hata akipata nafasi kubwa sana ya kujifunza, ataendekeza dharau.

Mimi nilikuwa najua habari hizi kwamba Nigeria imeipita Tanzania kwa GDP siku nyingi, ila mtoa mada kachokoza mjadala ambao umenifanya nisome article ya Joseph Stiglitz, Nobel laureate wa Economics 2001, iliyoongelea mapungufu ya GDP kwa kumnukuu mtu aliyebuni concept ya GDP, Simon Kuznets, Nobel Economics 1971.

Ingawa nilikuwa najua kwa muda mrefu jinsi wachumi wanavyoonesha mapungufu ya GDP kama kipimo cha uchumi, nilikuwa sijasoma hii article, sijajua kwamba GDP imebuniwa na Simon Kuznets, na sijajua kuwa hata huyo mtu aliyeibuni GDP alionya kwamba GDP haifai kutumiwa kama kipimo cha uchumi. Mada hii imenifanya nisome zaidi na kujifunza yote hayo.

Unaweza kufuatilia hiyo article ya Joseph Stiglitz katika post yangu #185 kwenye thread hii.

That's what JF is all about. Kuchokoza na kupanua mijadala.

Tumeanza kwa mtu kushangaa Nigeria imeizidi Tanzania kwa GDP, tumefika mpaka kujadili kama GDP inafaa kuwa kipimo cha uchumi kwa kuangalia maandiko ya nguli wa uchumi waliopata nishani za Nobel, Siglitz na Kuznets.

So, namshukuru mtoa mada kwa kuchokoza mjadala huu.

Hapa kuna watu wana miaka 70, na wengine wana miaka 14.

Sasa, kama wewe ulijua hii habari miaka 40 iliyopita, kwa sababu una miaka 60, hutakiwi kushangaa ikiwa kuna mtu ana miaka 14 anajua hili leo.

Unatakiwa kumuongezea vitu vingine ambavyo havijui.

Juzi nimeona kuna mtu kaanzisha uzi hapa JF, amekuwa so excited kagundua kitu kinaitwa podcasts Spotify, anauliza podcast ni nini?

Mimi nimekuwa nafuatilia podcasts kwa zaidi ya miaka 15 sasa.

Wala sikujisikia kumzodoa huyu mtu na kumwambia wewe mbona mshamba ndiyo unajua podcasts leo?

Kwanza hata sijui ana umri gani, inawezekana ni mdogo ndiyo ana explore internet, inawezekana ni mkubwa ila hakuwa na nafasi ya kujua podcasts.

Nilichofanya ni kumjibu na kumueleza tu podcasts ni nini, zina faida gani, anaweza kuzipata vipi, mfano wa podcasts na sofware zake. Na yeye akajifunza. Nilipata furaha sana kuona mtu ana experience kujua podcasts kwa mara ya kwanza.

Wala sikujisikia kusema "wewe ndiyo unajua podcasts leo wakati watu tumezijua miaka 15 iliyopita?".

Unaweza kusema hivyo halafu mtu akakwambia "Mzee usichukulie miaka 15 poa hivyo, wengine miaka 15 iliyopita tulikuwa hatujazaliwa bado" 🤣🤣🤣

Uzi uko hapa.

Korea Kusini ni vibaraka wa USA, makampuni makubwa yote huko yanamilikiwa kwa asilimia kubwa na USA.
UONGO. Bila hata ya soni. usoni.

LG; Samsung; Hyundai Motors, SK Hymix na mengi mengine ni makampuni ya Korea kwenyewe.
Watu, hasa wa aina yako mnapenda sana kupotosha kila jambo ili kuhalalisha ujinga mnaofanya hapa.
 
Canada unauliza tena? Huelewi kuwa Canada mpaka leo hii ni nchi ya wahamiaji? Kama ilivyo USA na Australia. Hata Singapore ni nchi ya wahamiaji.

Korea Kusini ni vibaraka wa USA, makampuni makubwa yote huko yanamilikiwa kwa asilimia kubwa na USA.
Lete ushahidi wa makampuni ya Korea kumilikiwa na Marekani.
 
Lete ushahidi wa makampuni ya Korea kumilikiwa na Marekani.
Huwa sik isii.

Wengi sana, wala siyo wakutafuta. Nakupa mmoja ukafanye homework:

Top insider stockholders Of Hyundai​

Hyundai has a few holders among the former and current executives. By far, the biggest individual Hyundai stockholders are Euisun Chung (Chairman) and José Muñoz (GCOO)

Kafanye homework ya kumjuwa Jose Munoz ni nani?
 
UONGO. Bila hata ya soni. usoni.

LG; Samsung; Hyundai Motors, SK Hymix na mengi mengine ni makampuni ya Korea kwenyewe.
Watu, hasa wa aina yako mnapenda sana kupotosha kila jambo ili kuhalalisha ujinga mnaofanya hapa.
Kafanye homework yako vizuri uone ka hayo makampuni hayapo listed kwenye "stock markets" za nchi za Magharibi.
 
Rwanda hawana lolote ndugu yangu.Ulishawahi sikia Waethiopia wanaenda Rwanda kutafuta maisha?
Kila nchi ilitakiwa watu wake wakae Nyani ya nchi Yao ya asili waendeshe maisha yao. Wakienda ugenini waende kama wataalamu na SIO wakimbizi . Wamarekani hua hawataki nje ya Marekani kutafuta KAZI zaidia ya kuwekeza au Utalii au Kwa ajili ya utaalam Fulani na SIO kwenda kubeba mabox.

Iko Hivi Waethiopia na wasomali wanakwenda Afrika Kusini Kwa Sababu Wazungu kule Afrika Kusini hawawaamini watu weusi Kabisa . Watu wanaoaminika ni Wahabeshi na Wasomalia peke Yao. Hata Waafrika Kusini Weusi ni ngumu sana kuajiriwa kwenye makampuni ya wazungu.
Watu weusi ni wezi na majambazi Wa kutisha .
Hivyo wasomali wakifika Kule wanapata KAZI kwenye migodi na maeneo mengine ya Wazungu . Huko wanafanya KAZI Kwa mapengo ya kupata mitaji. Wakiata mitaji wananzisha biashara na kujitegemea kisha wanatumia pesa Nyumbani Somalia kuwasafirisha ndugu Zao wengine wakafanye Kazi walizoacha Baada ya kupata mitaji . Wasomali na Waethiopia ni waaminifu na wanamalengo ya kujitegemea Zaidí.

Maendeleo ya Afrika Kusini ni Mavi ya uharo kwa Waafrika weusi ambao ni wazawa.
Wanaofaidi Afrika Kusini ni wanasiasa na familia Zao. Ule ni uhuru Wa kisiasa na kijamii tu na SIO kiuchumi.

Rwanda Wananchi wazawa wanaishi maisha yao wenyewe bila kunyonywa na mgeni au matajiri Wachache. Serikali inasimamia haki za Wananchi wake kwnye Sekta zote .
Usiombe hii nchi ifikie ule ubepari na Unyonyaji Wa Afrika Kusini. Japó awamu ya Sita inatupeleka huko Kwa Kasi Kubwa sana.

Wanaoumia kule Afrika Kusini ni Watu weusi. Kuna maeneo MTU mweusi Hawezi kukanyaga Kabisa na hathaminiwi Kabisa.
Wazungu Kule Afrika Kusini wanavitalu na mazoo ya Kufuga wanyama .
MTU mweusi Hawezi Hata kuonja nyama ya swala labda arudi porini akaishi kama mabushmen.
Hiyo ndiyo Tanzania ya Mafisadi inakoelekea Kwa Sasa. Eti ni maendeleo na ajira za kufagia mabanda ya Kufugia majoka ,Simba ,mbwa na farasi Wa mafisadi na majizi ya Mali za umma waliojivika Koti la wawekezaji.
 
Huwa sik isii.

Wengi sana, wala siyo wakutafuta. Nakupa mmoja ukafanye homework:

Top insider stockholders Of Hyundai​

Hyundai has a few holders among the former and current executives. By far, the biggest individual Hyundai stockholders are Euisun Chung (Chairman) and José Muñoz (GCOO)

Kafanye homework ya kumjuwa Jose Munoz ni nani?
Sasa huyo ndio mmiliki? Kila nchi makampuni mengi yanakuwa na wanahisa kutoka mataifa mbalimbali.
 
Huwa sik isii.

Wengi sana, wala siyo wakutafuta. Nakupa mmoja ukafanye homework:

Top insider stockholders Of Hyundai​

Hyundai has a few holders among the former and current executives. By far, the biggest individual Hyundai stockholders are Euisun Chung (Chairman) and José Muñoz (GCOO)

Kafanye homework ya kumjuwa Jose Munoz ni nani?
Umefilisika akili kabisa.
 
Back
Top Bottom