Uchaguzi 2020 Nimesikitishwa na ubinafsi wa CHADEMA katika mkakati wa wapinzani kusimamisha mgombea mmoja

Uchaguzi 2020 Nimesikitishwa na ubinafsi wa CHADEMA katika mkakati wa wapinzani kusimamisha mgombea mmoja

Amini nawaambia ukweli kuwa kuna baadhi ya vyama ni kichaka cha watu wa usalama ( kitengo) wapo kwenye hicho chama ili kuudanganya umma tu.
Utakua unawasema chadema walipomteua mgombea toka ccm mwaka 2015
 
Chadema haijajaribu kuungana na ACT ila ACT ndio inajaribu kuungana na Chadema.

Umeshawasikia viongozi wa Chadema wakisisitiza kila mara suala la kumsimamisha mgombea mmoja 2020?Sanasana utamsikia Zitto ndio akililia huo muungano ambao mwaka 2015 aliukataa kabisa.
Nilimsikia Lissu akizungumzia kushirikiana na si kuungana, na akasema kama wasiposhirikiana basi watachakazwa kwelikweli.
 
Watu wanakosea sehemu moja au kwa kujua au kutojua kuwa ACT ya sasa ni sawa na cuf ambayo bila ukawa haikuwa tishio kwa Tanzania bara. Hivyo hata sasa ACT ili wafanikiwe ni lazima wahitaji uungwaji mkono wa cdm tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Unachosahau CUF ya 2015 haikua na mtu mwenye kariba ya Zitto na Mwenye kariba ya Membe, mimi nashauri kama wewe wala wasishirikiane hata kidogo, halafu tuje hapa baada ya uchaguzi kufanya tathmini ya Nani kapata nini na nani kakosa nini, bila kulialia kuhusu faulo zilizochezwa na tumeccm&policeccm.
 
Kwa maana yako Zitto ndiyo kinara wa upinzani hapa Tanzania? Twambie mafanikio ya Zitto akiwa pekee yake maana mwaka 2015 ACT ilishiriki pia uchaguzi!
Zitto alishiriki uchaguzi huku chama chake anachosemekana kuanzisha akiwa ndani ya CDM kikiwa na mwaka mmoja, alibahatika kupata mbunge mmoja, nahalmashauri moja huku akiwa katikati ya dhoruba kali ya CDM&CCM kutomtaka arudi bungeni, na alifanikiwa pia kupata madiwan baadhi ya maeneo kama Mbeya&Dodoma&Tabora.

Sasa sasahivi chama kinakaribia miaka 6, huku akiongezewa nguvu na Maalim&Membe ambae Kwa haraka tu hata kwa faulo za ccm ACT pembe itanyakua majimbo yote, huku Zitto akiwa nauhakika wazaidi ya asilimia 85 yakurudi bungen hata kupitia faulo za ccm. Kwa mantiki hio ACT ilivyokuwa baada ya uchaguzi wa 2015 haitokua hivyo baada ya uchaguzi wa 2020 itakua imekua na kila mwenye macho anaona.

Kuja kwa Membe ACT na kama akisimama membe Kwanza itakua imewakuza kisiasa na kujijenga kitaasisi na ile propaganda iliyokua CUF ilikua inahamishiwa ACT itakua imekufa rasmi kuwa ACT nichama cha kidini, kwa msimamisha Membe ambae nimseminar.

Jambo lingine nikuwa sehem ambapo CUF ilikua na nguvu 2015 ndio ACT inanguvu 2020,kwa mfano mikoa ya kusini CUF ilikua na nguvu 2015 lkn kwa sasa nguvu hio imegeukia ACT, na nguvu hio imeongezeka maradufu baada ya Membe kuhamia ACT. Mikoa ya pwani pia ACT inanguvu kulingana na misimamo yao waliyonayo mikoa hio ya pwani kama Tanga. Magharibi pia naamini kwa sasa wamejijenga vizuri hasa Tabora&Kigoma&Rukwa&Katavi huko kote naamini ACT inanguvu kwa sasa kulingana na watu wengi wa mikoa hio kuwa na unasaba wa kimazingira na Zitto na wanaamini ACT kitakuwa ndio chama chao.

Mwisho naamini ACT bara haina Jambo lakupoteza kama isiposhirikiana na CDM kwa maana naamini watapata wabunge zaidi ya 3 bara . Na Pemba itapata wabunge pia, kwenye uraisi ACT haina Cha kupoteza kama ikimsimamisha Membe zaidi itaongeza Kura zaidi ya mara 10 ilizopata 2015 na ruzuku itaongezeka. Lakini pia CDM itapoteza katika uraisi kwa maana kuwa wafuasi kindakindaki waliokuwa CuF na waliobaki CUF hawako tayari kumchagua mgombea toka CDM kulingana na propaganda zilizojengwa juu ya CDM tofauti na 2015.

Tukutane baada ya uchaguzi huku kuangalia nani kapata nini na kakosa nini, Jambo lingine hatutaki kusikia kelele za wapinzani kuwa waligawana kura maana tunawaasa washirikiane lkn hawataki.
 
Vema kabisa, sasa kama mnalijua hili kuwa ACT ni kubwa sana kwa sasa kuliko vyama vingine inakuwaje mnalia lia juu ya cdm kukataa kuwaunga mkono?

Nyinyi mlikataa kujiunga na ukawa na watu wakasonga zao mbele, sasa nanyi tulieni tu maisha yasonge tu
Hakuna mahala niliposema ACT nikubwa kuliko CDM, nawala mimi sio ACT bali nimtu naetaka ACT&CDM washirikiane ili kuongeza nguvu katika urais ili tuone angalaua @Maguful akipata kashkash, sisi wengine tutaenda kupiga kura kama wapinzani watashirikiana tofauti na hapo siwezi kwenda kupiga kura kuongezea vyama ruzuku, huku nikiwa naamini bila ushirikiano ccm haiwezi toka madarakani.

Yaani tukose tumehuru, na tukose ushirikiano wa vyama vya upinzani halafu tutegemee ccm itatikisika huko nikujidanganya. Na ukiangalia kabisa mazingira ya 2015 yalikua na uhuru kidogo ,kuliko 2020 ambapo wizi na unyang'anyi wakura utatamalaki.
 
Tupatie sababu iliyo mfanya Zitto akakataa kujiunga na ukawa mwaka 2015!
Zitto hakukataa kujiunga na ukawa aliandika barua yakuomba kujiunga ukawa lakini alikataliwa. Kwa mazingira hayo kila alilolifanya kuelekea uchaguzi na baada yauchaguzi alikua sahihi maana hakua sehem ya ukawa. Na hata sasa kama wasiposhirikiana kila chama kitakua huru kufanya yale kinayoyaona yanafaa hata kama nikushirikiana na ccm kudumisha chama kingine ilichenyewe kipate sababu ya kukua.

Mfano NCCR inayoyafanya tunaweza kuona haiko sahihi kwa sababu tunahitaji mageuzi, lkn kwa ukuaji wake wako sahihi kushirikiana na ccm ili kiendelee kuishi.

Kama pia CDM ilivyoshirikiana na ccm 2005 ili kuua nguvu ya CUF, nahata kuchukua magari kwa baadhi ya makada wa ccm ili wasiweke wagombea katika baadhi ya majimbo ili wapite bila kupingwa.
 
Kama Act hawataki kuwa chini ya Chama kingine huo muungano unafanyikaje? Hakuna Muungano ambao kila mmoja anatoa maelekezo yake. Kila Muungano una pande moja yenye maamuzi ya Mwisho.
 
Salaam Wakuu,

Hii hali ya kujiona CHADEMA ndo Baba lao kwenye vyama vya Upinzani, inaumiza watu wanaounga mkono Upinzani. Nimesikitika kuona CHADEMA wanaweka Mashariti magumu kwa vyama Vingine kuunganana as if wana haki miliki na wapiga kura.

Mbowe alisema lengo ni kuiondoa CCM madarakani, kwanini leo watu wagombanie fito wakati lengo lao moja?

ACT wapo tayari kwa Ushirikiano ila sio kuonekana wapo chini ya chama fulani.

Wanasiasa wa Sera mbadala, kama watampa nafasi Mwenyekiti wa CHAUMA Mheshimiwa Hashim Rungwe awashauri na kuweka Mikakati ya kuungana, watafanya Vizuri sana.

Chonde chonde CHADEMA chini ya Mbowe, kuweni na Moyo uliopondeka na wenye kupenda Umoja bila kiburi.

Mkikataa Ushirikiano, mtachakazwa na CCM hadi Mshangae. Sababu vyama vya upinzani mtagawana gawana kura za wafuasi wenu walio wengi.

TANZANIA hakuna chama Kidogo. ACT haina hata miaka 10 lakini inaonekana sawa na zaidi ya vyama vyenye miaka zaidi ya 20
Umeanza lini kuwashauiri wa chamema? Watakati wanataabika na kutaabishwa na serikali dhalimu ulikuwa wapi?
 
Chadema yana tamaa sana,

Na kwa tamaa zao hizo mwaka huu hawaoati kura!

Zitto ataendelea kushine hasa Zanzibar, huku Chadema ikiendelea kushine Kilimanjaro pekee.
Mkuu, hivi unajua hakuna kitu kibaya kama kulishwa sumu na mtu na ukakubali kuimeza, kumbuka huyo magufuri yeye ana chuki binafsi na wapinzani hasa chadema, na ndio maana alitaka kumuua Lissu, sasa chuki yake hiyo ambayo ni yeye anayejua ilikoanzia yaani kiini chake amekuwa akiwalisha watu na kwa bahati mbaya watu wanakubali kuimeza na kuiweka kwenye mioyo yao, unamchukiaje mtu kwa sababu kulishwa maneno ya sumu na mbaya wake ilhali wewe huna ubaya na huyo mtu ?, ifike mahala watanzania tujitambue, kama musa ana chuki na bakari haipaswi Hamadi alishwe sumu ya chuki na aamue kuungana na musa kumchukia bakari, Mkuu una chuki ya hatari sana na Upinzani, ninakuombea kwa Mungu akuponye, kwa sababu Neno la Mungu linasema Tafuteni kwa bidii kuwa na AMANI na watu wote ili muweze kuurithi Ufalme wa Mungu.
Siku Njema
 
Basi kila mtu atazame kitakacho mfaa wacheni kulia lia tunajua kuwa mnatumiwa na ccm
Hatutaki baadae mje kulia mnahujumiwa humu , kuwa mnahujumiana huku mnaendekeza ruzuku badala ya kuangalia namna bora ya kuitoa ccm.
 
Mkuu, hivi unajua hakuna kitu kibaya kama kulishwa sumu na mtu na ukakubali kuimeza, kumbuka huyo magufuri yeye ana chuki binafsi na wapinzani hasa chadema, na ndio maana alitaka kumuua Lissu, sasa chuki yake hiyo ambayo ni yeye anayejua ilikoanzia yaani kiini chake amekuwa akiwalisha watu na kwa bahati mbaya watu wanakubali kuimeza na kuiweka kwenye mioyo yao, unamchukiaje mtu kwa sababu kulishwa maneno ya sumu na mbaya wake ilhali wewe huna ubaya na huyo mtu ?, ifike mahala watanzania tujitambue, kama musa ana chuki na bakari haipaswi Hamadi alishwe sumu ya chuki na aamue kuungana na musa kumchukia bakari, Mkuu una chuki ya hatari sana na Upinzani, ninakuombea kwa Mungu akuponye, kwa sababu Neno la Mungu linasema Tafuteni kwa bidii kuwa na AMANI na watu wote ili muweze kuurithi Ufalme wa Mungu.
Siku Njema
Kama chuki ya Zitto na MBOWE ishahamia kwenye taasisi huku wao wanajua chuki zao ni za nini, wanachekeana huku wanaviziana kila mtu ammalize mwenzake.
 
Chadema bila nyota ya Lissu haina lolote jipya.... Ndio alikibeba sana chama 2015 hadi 2017. Alipokuwa kwenye matibabu Zitto Kabwe ndiye aliubeba upinzani wakati mgumu sana yaani 2017 hadi hii 2020 na mmekuwa mkisapoti sana hoja zake hapa. Kurudi kwa Lissu ndiko kunakowabeba sasahivi na anataka ushirikiano aliouomba kwa dhati kwenye mkutano wa ACT. Ninyi mavuvuzela ya chadema badala yakusonga mbele mmerudi kwenye kui_attack ACT eti ni chama cha mamluki na wasaliti.... Subirini mshindwe uchaguzi ndipo mtaona wakina Lijualikali na Mollel wengine waliobaki huko chamani watakavyojiuza na kununuliwa kama njugu mawe.........

Yaani ninyi Chadema mna ruhusa ya kuiongea hovyo ACT kama mlivyoanza nyodo toka Lissu arudi nchini. Tukianza kuwapiga 'spana' mnaanza kulialia hivi. Upinzani ukienda kwenye uchaguzi na siasa za majitaka za kushambuliana wenyewe kwa wenyewe nina uhakika Chadema ndiyo itapoteza pakubwa huku bara......Yaani msiungane muendelee kushambuluana halafu hiyo November tupeane mrejesho wa siasa za majitaka......

CHADEMA wakileta nyodo basi ACT isimamishe watu kila jimbo na kwenye kiti cha uraisi halafu tuone kama CHADEMA itapata hata wabunge 20

ACT ina uhakika wa kupata viti Vya Ubunge Zanzibar na pia ikiamua kwenda peke yake huku bara itakikuza chama chao huku bara haswa kwenye mikoa ya kusini. Kwa vyovyote vile baada ya Uchaguzi huu ACT itakuwa imegain na Chadema ikileta nyodo haitopata urais na wala haitopata idadi ya wabunge iliyowapata mwaka 2015

Kinachomsukuma Zitto kutaka ushirikiano na CHADEMA ni kiu yake ya kuing'oa CCM na Magufuli tu baasi. Sasa moyo huu wa kujitolea wa Zitto kuna watu wanataka kumtake advantage

Mimi nasema, Kama CHADEMA watakuwa wanaleta tamaa kupita kiasi kwenye ushirikiano huu, basi Kila Chama kisimamishe wagombea wake kila sehemu then tuone nani atagain na nani atalose!
 
Salaam Wakuu,

Hii hali ya kujiona CHADEMA ndo Baba lao kwenye vyama vya Upinzani, inaumiza watu wanaounga mkono Upinzani. Nimesikitika kuona CHADEMA wanaweka Mashariti magumu kwa vyama Vingine kuunganana as if wana haki miliki na wapiga kura.

Mbowe alisema lengo ni kuiondoa CCM madarakani, kwanini leo watu wagombanie fito wakati lengo lao moja?

ACT wapo tayari kwa Ushirikiano ila sio kuonekana wapo chini ya chama fulani.

Wanasiasa wa Sera mbadala, kama watampa nafasi Mwenyekiti wa CHAUMA Mheshimiwa Hashim Rungwe awashauri na kuweka Mikakati ya kuungana, watafanya Vizuri sana.

Chonde chonde CHADEMA chini ya Mbowe, kuweni na Moyo uliopondeka na wenye kupenda Umoja bila kiburi.

Mkikataa Ushirikiano, mtachakazwa na CCM hadi Mshangae. Sababu vyama vya upinzani mtagawana gawana kura za wafuasi wenu walio wengi.

TANZANIA hakuna chama Kidogo. ACT haina hata miaka 10 lakini inaonekana sawa na zaidi ya vyama vyenye miaka zaidi ya 20
Hujaeleza Chadema wamefanya nini
 
Unachosahau CUF ya 2015 haikua na mtu mwenye kariba ya Zitto na Mwenye kariba ya Membe, mimi nashauri kama wewe wala wasishirikiane hata kidogo, halafu tuje hapa baada ya uchaguzi kufanya tathmini ya Nani kapata nini na nani kakosa nini, bila kulialia kuhusu faulo zilizochezwa na tumeccm&policeccm.
Subiri kelele za ACT imetumiwa na CCM kupunguza kura za CHADEMA.
 
Back
Top Bottom