Nimesononeshwa sana mpaka leo hii kama nchi tunatafuta mwekazaji wa usd million 27

Nimesononeshwa sana mpaka leo hii kama nchi tunatafuta mwekazaji wa usd million 27

Uwekezaji wote wa China Tanzania haufiki dola bilioni kumi na mbili na ndiyo mwekezaji mkubwa.Mleta mada anaposema mwekezaji asiruhusiwe mpaka awe na mtaji wa dola bilioni moja ni wawezekaji wangapi watachukua risk ya kuwekeza kwenye Nchi ambayo hata umeme ni shida.
Ametolea mfan
Lakini haijawahi kutokea kwa mtu binafsi kuwekeza zaidi ya dola bilioni moja kwenye biashara yoyote Tanzania ukiondoa miradi ya kiserikali na ikitokea TIC itabidi ipongezwe.
Jamaa ametoa mfano tu kwamba lazima kuwe na minimum investiment sio waje na uswahili swahili.
 
Miradi mingi Serikali inaweza wekeza na management ikatafuta hata foreigner,.
ILa mingi inafeli sababu tunalazimisha management lazima itoke Tanzania hapo ndo tunapofeli
Ni kweli, na hiyo inatutafuna sana.

We angalia mashirika yetu ya Ndege, reli n.k

Tunatanguliza uchama na itikadi badala ya kuangalia uwezo wa CEO tunayemteua
 
Waafrika tumetishiwa sana yaani uyachimbe madini alafu ukose pa kuyahuzia sio kweli

Madini yote masoko yao yanajulikana na tukiendelea na hizi mindset ni ngumu sana kujikwamua
Hujui dynamics za international business na cartels zinavyofanya kazi
 
Kwa hiyo watu wamepoteza ajira ambazo zingetengenezwa, bidhaa, mapato, kodi pamoja na mazingira na miundombinu ya jirani imedumaa
Kuna tatizo kubwa sana
Hata Rais mmoja aliwahi kusema, hata yeye hajui kwanini sisi ni masikini

Kama Rais alisema hivyo hao wanaoongozwa je
 
Back
Top Bottom