Habari Za sahivi wanajamii wenzangu. Mimi ni msichana nina miaka 29. Natamni Sana kujiajiri Kwa sababu kazi zimekuwa ngumu Sana, nimetafuta mpaka nimechoka sasa nimeuza simu yangu Na radio yangu nimejikuta mkononi nina laki 3 Tu.
Naombeni ushauri japo wa mawazo nifanyie biashara Gani ambayo naweza nikazalisha na kupata walau faida Na baadae hata kurudisha both vilivyopotea.
Nawaza biashara Nyingi Lakin Naona kama mtaji hautoshi. NB: Msiniseme naombeni mawazo mazuri ya kunijenga natamni nisimame mwenyewe kama wengine.
Location nipo Dar es Salaam
Hongera sana dada yangu, huwa napenda sana wanawake wanaofanya kila juhudi njema kujikomboa.
Hio laki tatu ulio nayo ni nyingi mno unauwezo wa kukufikisha sehemu hutaamini.
Wengi wetu tulianza na robo ya hio na tupo sehemu tunadhubutu kusema asante Mungu.
Binafsi huwa naamini katika shuguli au biashara ya mfumo wa kuzalisha na kuuza, kuliko kununua na kuuza.
Unapozalisa unajiweka katika nafasi ya kukua na kujenga msingi wa biashara inayo dumu.
Naomba nitoe mifano mdogo , kwa vile umesema upo dar, unaweza kutafuta bonde au sehemu unayo weza kulima mboga, kwa hiyo hela inatosha kikamilifu, utalima mboga zinaweza kua za aina yoyote, zikisha fikia wakati wa kuvuna unazinua kama vile ungenunua kwa mtu au mkulima mwingine, unaenda kuuza kwa bei iliyopo sokoni, hapo unaweza ukawa umetengeza faida mbili,na kwa mwendo huo unaweza siku ukajikuta upo mbali sana, kumbuka pia mboga karibu zote hakuna zinazo vuka miezi miwili.
Unaweza pia ukaanzisha biashara kuchoma vitu, mfano mihogo ya kuchoma, mahindi ya kuchoma, ndizi za kuchoma, viazi vya kuchoma nyama na kadhalika, yaani pasiwe na kitu cha kuchemsha wala kukaanga ni kuchoma tu.
Mwanzo inaweza kuwa na ugumu kidogo lakini baada ya muda itazoekeka na itakua sehemu amazing sana.
Unaweza pia kuvunja mwiko, mfano kijiwe cha kahawa mara nyingi kinahudumiwa na wanaume, sasa ukifanya wewe mwanamke unaweza ukafanya biashara kuliko unvyo dhani , kuandaa kahawa na tangawizi na kashata unaweza ukajifunza kwa muda mfupi na hio hela ulio nayo unaweza kufika mbali sana.
Unaweza pia ukatafuta sehemu yenye mzunguko wa watu wengi ukaweka meza ukawa unauza vitu kama mwiko wa kupikia, fagio za Chelewa vibao vya chapati, viboksi vya kuhifadhia hela au vibubu, Vigari vya watoto, stendi za friji,vigoda enga za kutundika nguo nk, kwa hela ulio nayo ukaenda kwa fundi local akakuelekeza aina za mbao za kununua then anakuchongea hivyo vitu , ukamlipa kiasi natumaini utafanya biashara na utakuwa Brand kubwa.
Yote nakutakia kufanikiwa ndugu yangu, kumbuka Mungu huibariki nia njema, jitihada hazizidi kudra, hivyo sambamba na unavyotafuta cha kufanya uwi hivyo kwa kumtegemea Mungu na kuweka nia njema, Asante.