Nimetafuta kwenye Quran hakuna sehemu Mungu amesema waislamu muoane

Nimetafuta kwenye Quran hakuna sehemu Mungu amesema waislamu muoane

Ni mimi wako UWESUTANZANIA ✍️

Sipo hapa kwa kubeza wala kukejeli nataka kupewa elimu kutoka kwa muislamu aliyesoma Quran tukufu ambayo ndio muongozo wa muislamu na usinilete hadithi kutoka muslim na tilmizu eti alimsikia mtume akisema hapana.

Nataka kwa mwenye andiko kutoka kwenye kitabu (Qur-an
  • wapi Mungu kasema tuoane
  • wapi Mungu kasema uoe wanawake wanne
  • wapi Mungu kasema ukioa mkigombana umpe taraka na watoto.
  • wapi Mungu kasema ukimkumbuka uende kwao ukamlejee.

Asanteni.

Kama mambo ya kawaida kama hayo hujayaona, basi wewe hujasoma Quran....
Acha upotoshaji eti nimesoma Quran??? Usijipe sifa ambazo huna
Ili kukutoa ujinga....Jaribu kusoma Sura An Nisaa...utapata majibu ya maswali yako!!!
 
Sijui wapi imesema wanawake wavae Hijab, Nicab etc.
Surah An-Nur (24:31)

31. Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao, na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika. Na waangushe khimaar (shungi) zao mpaka vifuani mwao, na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao, au wana wao wa kiume, au wana wa kiume wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kiume wa kaka zao, au wana wa kiume wa dada zao, au wanawake wao (wa Kiislamu), au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi wanaume wasio na matamanio ya jimai miongoni mwa wanaume au watoto ambao hawatambui kitu kuhusu sehemu za siri za wanawake. Na wala wasipige miguu yao yakajulikana yale wanayoyaficha katika mapambo yao (vikuku na kadhaalika). Na tubuni kwa Allaah nyote, enyi Waumini mpate kufaulu.

Surah Al-Ahzab (33:59)

59. Ee Nabiy! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wanawake wa Waumini wajiteremshie jilbaab zao.Hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane (kwa heshima) wasiudhiwe. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
 
Mleta Mada Na Makafir Wenzio Lengo Lenu Haliwezi Kutimia.
Rudini Makanisani Mkajipange Upya.

Uislamu Ni Dini Ya Hoja Na Quran Ni Kitabu Kisicho Na Shaka Humo Hakuna Mambo Ya Petro Kumiminwa Wala Neno Kuwa Kwa Neno Mtafungua Nyuzi Mpaka Mjambe .
 
Mumeleta maandiko marefu sana bila kuweka andiko wapi Mungu anampa muislam amri ya kuoa!.

Nilipenda kuona hiyo amri, vigezo na masharti ya kuoa. Lakini maandiko yenu yote yame skip hitaji langu mama

Kingine unaposema "amri" hii moja kwa moja inakuwa ni lazima kuifuata hiyo amri waislamu hatujaamrishwa kuoa , Allah (the almighty) ametupa machaguzi na mtume muhammad (peace be upon him ) akasisitizia sana kwa mwenye uwezo na aoe maana ni bora sana kwake kuliko kutofanya hivyo na kwa sababu tunawafuata mitume kama walimu wetu na kuoa ni sunna ya mitume wote hadi nabii isa bin maryam ( peace be upon him) akirudi kwa mara nyengine ataoa ataishi duniani kwa wakati alioandikiwa na atakufa pia.

Ila si lazima kuoa na hapa kuna maelezo meengi sana ya mtu wa aina gani hatakiwi kabisa kuoa /kuolewa , mtu wa aina gani kwake ni lazima kuoa / kuolewa na asipofanya hivyo atajiingiza kwenye madhambi but hii ni topic ya muda mwengine uzuri swali lako limeshajibiwa .
 
Sijui wapi imesema wanawake wavae Hijab, Nicab etc.

Al-Ahzab 33:59

يَآأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ قُل لِّأَزۡوَٰجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَآءِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ يُدۡنِينَ عَلَيۡهِنَّ مِن جَلَٰبِيبِهِنَّۚ ذَٰلِكَ أَدۡنَىٰٓ أَن يُعۡرَفۡنَ فَلَا يُؤۡذَيۡنَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورࣰا رَّحِيمࣰا

Swahili - Ali Muhsin Al-Barwani

Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

English - Tafsir Ibn Kathir (Abridged)

3595

Jilbab ni ile inayofunika mwili mzima na pana na si hizi zinazobana wanazofaa wadada wa siku hizi ni zile wanazovaa wanawake wa ki ahlu sunna waljama'a/salafy ambazo hazichori mwili
 
Kuoa
Surah An-Nisa (4:3). Aya hii inasema:

"Ikiwa mnaogopa kutokuweza kutenda kwa haki kwa mayatima, waoe wanawake wenye kujivunia wawili, watatu au wanne, lakini ikiwa mnaogopa kutokuwa sawa, basi oeni mmoja tu au wale mlio na haki yao.

Talaka

Surah Al-Baqarah (2:229) inasema:

"Talaka ni mara mbili. Kisha, iwe na wema au kuachana kwa njia nzuri. Na siyo halali kwenu kuchukua chochote mlichowapa wanawake, isipokuwa kama wote wawili wanashikilia mkataba wa kuishi kwa njia nzuri."

We mgalatia biblia yenyewe umeshindwa kusoma na kuielewa utaelewa vipi Quran
 
Ni mimi wako UWESUTANZANIA ✍️

Sipo hapa kwa kubeza wala kukejeli nataka kupewa elimu kutoka kwa muislamu aliyesoma Quran tukufu ambayo ndio muongozo wa muislamu na usinilete hadithi kutoka muslim na tilmizu eti alimsikia mtume akisema hapana.

Nataka kwa mwenye andiko kutoka kwenye kitabu (Qur-an
  • wapi Mungu kasema tuoane
  • wapi Mungu kasema uoe wanawake wanne
  • wapi Mungu kasema ukioa mkigombana umpe taraka na watoto.
  • wapi Mungu kasema ukimkumbuka uende kwao ukamlejee.

Asanteni.
Kama unajpenda unapoenda kuishsi maisha marefu na familia yako achana nayo hayo...
 
Sijui wapi imesema wanawake wavae Hijab, Nicab etc.
Kuvaa hijab
Ipo katika surat An Nur aya ya 31

31. Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, au wafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambao hawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chini miguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Na tubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ili mpate kufanikiwa.
 
Kingine unaposema "amri" hii moja kwa moja inakuwa ni lazima kuifuata hiyo amri waislamu hatujaamrishwa kuoa , Allah (the almighty) ametupa machaguzi na mtume muhammad (peace be upon him ) akasisitizia sana kwa mwenye uwezo na aoe maana ni bora sana kwake kuliko kutofanya hivyo na kwa sababu tunawafuata mitume kama walimu wetu na kuoa ni sunna ya mitume wote hadi nabii isa bin maryam ( peace be upon him) akirudi kwa mara nyengine ataoa ataishi duniani kwa wakati alioandikiwa na atakufa pia.

Ila si lazima kuoa na hapa kuna maelezo meengi sana ya mtu wa aina gani hatakiwi kabisa kuoa /kuolewa , mtu wa aina gani kwake ni lazima kuoa / kuolewa na asipofanya hivyo atajiingiza kwenye madhambi but hii ni topic ya muda mwengine uzuri swali lako limeshajibiwa .
Kila kilichoelekezwa katika quran ni amri hamna siasa ukiambiwa , Simamisha swala nenda kasali kweli, ukiambiwa acha zinaa acha kweli, usipoacha umekufuru, ila yako mambo yaliyoelekezwa na kutolewa option ya pili mfano unaruhusiwa kuoa wake wanne ila kama huna uwezo oa mmoja na uwe muadilifu, kwenda kuhiji ni kwa yule mwenye uwezo usipokua na uwezo basi hamna namna kwahiyo hakuna negotiation ni maelekezo vipi muumini aishi.

Unasema haujaamrishwa kuoa sasa mwanaume uliekamilika unaweza vipi kuishi bila mke? Kama unaweza sawa ishi bila mke ila hakikisha haufanyi zinaa maana zinaa ni uchafu na ni katika dhambi zenye kuangamiza zilizokatazwa kwenye Quran
 
Attachments

  • Screenshot_20250304-125706.png
    Screenshot_20250304-125706.png
    140.9 KB · Views: 1
Surah An-Nur (24:31)

31. Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao, na wala wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa yale yanayodhihirika. Na waangushe khimaar (shungi) zao mpaka vifuani mwao, na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao, au wana wao wa kiume, au wana wa kiume wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kiume wa kaka zao, au wana wa kiume wa dada zao, au wanawake wao (wa Kiislamu), au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, au wafuasi wanaume wasio na matamanio ya jimai miongoni mwa wanaume au watoto ambao hawatambui kitu kuhusu sehemu za siri za wanawake. Na wala wasipige miguu yao yakajulikana yale wanayoyaficha katika mapambo yao (vikuku na kadhaalika). Na tubuni kwa Allaah nyote, enyi Waumini mpate kufaulu.

Surah Al-Ahzab (33:59)

59. Ee Nabiy! Waambie wake zako, na mabinti zako, na wanawake wa Waumini wajiteremshie jilbaab zao.Hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane (kwa heshima) wasiudhiwe. Na Allaah daima Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
Jazzakallah khaira 👃👃 mmungu akulipe na atukubalie swaum nzetu👃👃
 
Back
Top Bottom