Nimetapeliwa nauli na mrembo niliyekutana naye mtandaoni

Nimetapeliwa nauli na mrembo niliyekutana naye mtandaoni

Mnavyojua tena, maisha ya harakati huwa hayana mwisho. Wiki tatu zilizopita nilikuwa nachat na mrembo mmoja matata, niliyekutana naye katika mtandao mmoja wa kuonyesha sura.

Nilitokea kumpenda sana huyo binti, na tukafahamiana vizuri tu. Yeye yuko kwenye mambo ya mitindo.

Tatizo yeye anaishi mkoa tofauti na niliopo mimi; nikawa nimemjulisha wikiendi ijayo tuweze kuonana, na tukawa tumeafikiana. Sasa leo asubuhi, akawa amenijulisha anataka aje kuniona; mi nikaona sawa tu hakuna shida.

Akaomba nauli, nami nikamtumia mara mbili yake. Kilichonishtua zaidi, kuwa nauli imeliwa, alianza kuniambia nitume na hela ya mafuta fulani kwa ajili ya massage, yanagharimu 50,000; nikatafakari, nikamwambia tutayanunua huku huku ukishafika.

Baada ya hapo, nikipiga simu haipokelewi, meseji hazijibiwi, w/app hajibu. Imebidi ni hitimishe tu; nauli yangu imeliwa. Ingawa angekuja ningetumia zaidi pamoja na posho ya kwake, lakini kilichoniuma zaidi ni kutokuwa muaminifu.

Wakuu, nimfanyeje huyu mkulungwa?
Wajinga ndio waliwao!! Pole Sana.
 
Kama kuna nyingine imebakia unaweza kunitumia mimi tadhari yaani iwe kama sadaka as you know this is Sunday [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kwa muonekano ule pale hamna kitu hata Kama ungesema wewe ndo umeenda mkoa alipo asingejitokeza.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mkuu we acha tu, utapeli hauishi; kanitumia w/app yuko njiani, lakini najua ni usanii. Nilianza naye mwaka jana, baana ya kuona miyeyusho nikavunja mawasiliano. Hivi karibuni ndio alianzisha yeye
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] ebwana filter zinaharibu kinyama juzi kuna jamaa yangu kaniomba nimaindikize akakutane na demu waliojuama mtandaonii akanionyeshaa tukaenda tulichokutana nacho sikuaminii mwamba aliishiwa pozii
JamiiForums1297672963.jpg
 
Back
Top Bottom