Nimetapeliwa zaidi ya Tsh. 45,000,000 kwa kuuziwa kiwanja feki

Wengine kumuita wakili wanaona gharama.
Hawajui kuwa wakili ndo mtetezi wako hata ikitokea matatizo anayekwenda mahakamani kufuatilia kesi NI yule hakimu .
Wakati wewe unaendelea na Mambo yako
Nakazia...

Hata Serikali za Mitaa siku hizi nao ni wale wale tu...
Wanachojali ni ile asilimia yao.. likikupata janga huko unapambana mwenyewe..
 
Kaka serikali ni kubwa na Ina mkono mrefu.
Kama unachotaka kuuziwa hakijulikani na serikali.
KIMBIA.
Mfano viwanja vilivyopo uko vikindj ndani ndani je wizara ya ardhi inavijua ama inakuwaje apa?
 
Mkuu mimi sikubishii unachoamini ila kama umeamua mkataba wako wa kununua ardhi usimamiwe na mwenyekiti wa serikali ya mtaa sawa na ninakutakia kila la kheri maana unaamini kuwa wanajua historia.
Ila ninakupa task, nenda kafuatilie migogoro ya ardhi ambayo mauzo yalisimamiwa na hai unaosema wanajua historia halafu uje hapa utueleze.
Kwamba mwenyekiti akajue taarifa za mirathi, familia, vikao vya familia, kama kuna mikopo, kama mali ilichumwa na wenza, nk? Sawa, kila la kheri mkuu.
 
  • Wana umuhimu wao kwa ardhi ambazo hazijapimwa,
  • Na hao serikali ya Mtaa ndio wameleta mabalaa ya kuuza Ardhi Mara mbili
  • Unasema Wakili amekaa ofisini hivi unajua maana ya neno 'official search'?
Yamkini anaamini kuwa ili uonekane unafanya kazi ni lazma uchafuke na tope ama hadi jasho likutoke😂😂😂😂😂😂. Na ndio maana hawataki kuwafuata mawakili. Lakini naamini gharama nje ya wakili ni kubwa sanaaa tofauyi na wanavyodai; mfano, kwenye kiwanja cha 45M mwenyekiti anakula 4.5M cash, dalali anakula si chini ya 4M jumla 9M. Hapo hapo kazi akipewa wakili unaweza kumlilia kwa hata 3M akamaliza kila kitu
 
Sasa tufanyeje aisee...upigaji umeanza upyyaaaaa yaani, hizo process wengi wetu tunafanya ivyo ulivyosema
 
Sasa tufanyeje aisee...upigaji umeanza upyyaaaaa yaani, hizo process wengi wetu tunafanya ivyo ulivyosema
Safi, hakikisha ukitaka kununua kiwanja ama eneo sehemu nyingine tumia wakili akusaidie kukuelekeza tahadhali za kuchukua.
Pia, ukiona mtu yeyote anataka kununua mshauri kuwa huo mkataba husika unaandaliwa na wakili pia anampa kazi nzima ya uchunguzi huyo wakili, hii haitaepusha kutapeliwa bali itasaidia kwa zaidi ya 85% kiepusha kutapeliwa, isikaze ubongo kulazimisha utakacho baada ya kushauriwa na wakili maana atakukubalia halafu baadae unaingia kwenye hatari.

Asante.
 
Ninyi Serikali za mitaa hamna mamlaka hayo kisheria, HAMTAMBULIKI POPOTE kisheria. Usilazimishe kwaajili ya 10% Mkuu.
 
Sawa sawa meku
 
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
 
Kiufupi ni kwamba nimetapeli million 45, nimekuja kugundua huu ni mtandao mkubwa unaongozwa na Diwani mstafu ambae alikuwa anajimilikisha maeneo ambayo wenyewe hawayajaendeleza au kutoonekana kwa mda mrefu na baadae anawapa vijana wake wa kazi na madalali wauze.

nimeshangazwa wenyeviti wa mitaa hata watendaji hawajui maeneo yao vizuri nao wamekuwa sehemu ya mgogoro, manunuzi yangu nimefata taratibu zote na zaidi nimeyafanya kupitia mwanasheria.

Tapeli wangu tayari nimemkamata jana usiku Dodoma vijini huko Kibaigwa, nimemrudisha morogoro nimemkabidhi polisi mwenyewe.

Hawa matapeli napelekana nao kimafia, lazima nifidiwe hata kwa kuuza makazi yao
 
Kaka kosa nililofanya ni kutokupitia kwa wenyeviti wa seriklai za mitaa nikamtumia direct mwanasheria lakini wenzangu walionitangulia kununua walipitia huko kwa wenyeviti lakini mambo ndo yamekuwa hivo
Ndio maana imekuwa rahisi kutapeliwa pole sana mkuu
 
Haya mambo yasikie tu.

Nina siku ya nne leo tangu nigundue kwamba nimepigwa, hata kula vizuri siwezi, nawaonea wivu wenzangu walionunua maeneo madogo kwa bei za 15m kushuka chini. Naona hasara yao ni ndogo kuliko yangu.
Hebu weka mkasa mzima mkuu na sisi tujifunze! Ilikuwaje hiyo! Mimi mwenzio nilitapeliwa 2m lakini nilijidharau karibia wiki nzima, nawaza tu nilivyotapeliwa kiboya (ingawa kwangu niliona kuna nguvu za giza zilitumika). Sasa wewe 45m si unaweza kuchizika kabisa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…