Nimetelekezwa na ujauzito, natafuta kazi

Nimetelekezwa na ujauzito, natafuta kazi

Watu wa Mungu mpoo?

Mimi ni member wa JF tangu miaka ilopita nimekuja na ID tofauti ili nieleze yaliyonikuta iwe funzo na ushuhuda kwa wengine.

Niliweka post hapa mika ilopita na kwa bahati tu sijui niseme nzuri au mbaya ila Mungu ndio anajua, nikapata mwanaume ambaye tulianza mahusiano ambayo yalikuwa siriazi kidogo.

Baada ya muda tukapanga mipango ya kuanza mikakati ya kufunga ndoa. Na wakati huo huo ujauzito ukawa umeingia kwangu. Sasa tangu nilipomwambia yule mwanaume kuwa nina ujauzito aliniblock simu na namba zote mawasiliano hakuna. Hadi leo amenitelekezea ujauzito. Alichoniambia mara ya mwisho kabla hajanikimbia ni "wewe ulivyobeba ujauzito si ulijua unabeba ujauzito na sina pesa za kukutunza" kwa maana hiyo nipambane na hali yangu mwenyewe.

Kiukweli maisha kwangu yamekuwa magumu maana ujauzito umefikisha miezi saba na siwezi kufanya kazi nilokuwa nafanya hapo mwanzo. Daktari alinisahuri niachane nayo maana ni kazi ya kusimama zaidi ya masaa saba endapo nitapata wateja mfululizo.

Me nimeleta hili janga lilonipata ili tuendelee kuwa makini humu. Tusikurupukie watu sio wote ni wazuri kama tunavyodhani

Pia nimekuja kuomba kwa yeyote anayeweza kuniajiri kwa kazi yoyote ambayo sio ya kusimama muda mrefu kwa muda wa miezi hii mitatu ya mwishoni nina uhitaji wa kazi ili walao nipate pesa kwa ajili ya kujifungua maana sina msaada wowote wa kifedha wala vifaa vya kujifungulia. Sina matatizo yoyote ya afya hadi sasa yatakayonifanya nishindwe kuhuduria kwenye kazi hiyo nitakayoipata.

Kwa vigezo mimi ni mhitimu wa elimu ya kidato cha sita najua lugha ya kiswahili na kiingereza pia ninajua kutumia komputa vizuri. Naahidi kwamba atakaeniajiri hatajuta licha ya kuwa mimi ni mjamzito.

Mungu awabariki sana.
Pole sana mrembo. Mungu akufanyie wepesi..
 
Pole sana mwaya. I hope utapata wa kukusaidia.

Japo ndo inahitaji utulivu mkubwa mno katika kufanya haya maamuzi ya kumpata wa kukusaidia huku mitandaoni kwani sio wote watakuwa na nia njema.
 
Pole sana dadake,

Niliwahi kuweka bandiko hapo jamani wadada tunajiangusha, unabebaje UJAUZITO hujaolewa na wala kwao hufahamiki wala YEYE kwenu hafahamiki?

Mwanaume akitaka ngono CHOCHOTE ANAWEZA KUKUFANYIA ila kumbuka akishapata anachitaji SIYO AJABU KUKUTELEKEZA!!!

Wadada JAMANI mbona mnatuangusha!!!

Anyway uko wapi tuangalie linalowezekana kama upo within the range maana hali uliyonayo ni nzito sana
 
Mimi hata sikuonei huruma... Nyie wanawake mashetan sana si bure hata hii adithi umeitunga na hata kama ni kweli haituhusu... Mwanaume na akili zake timamu akufanyie hvyo kwanin..? Lazima utakuwa una matatizo sio bure..? Yaani nyie wanawake mkitaka misaada mnaona njia nzuri ni kusingizia wanaume... Sister nakushauri muombe mungu wako akupambanie hakuna namna... Tatzo mnapenda kuparamia wanaume wa watu nina uhakika umepora wanaume za watu sasa malipo ni hapahapa duniani yamekukuta zamu yako sasa... Eti unasema una watahadharisha wenzako hivi unadhan nyie mnajitambua basi? Sasa hivi kuna wenzako wanakucheka tu wapo inbox wanajibebisha kwa wanaume wa watu humu JF IG FB Twtr...
Wanaume ni watu wazuri sana ukiishi nao kwa heshima ila ni mbwa 😂 (kama mnavyotuita) kama ukionyesha dharau kiburi na jeuri... KARMA is Real ✌️ am out
Kwa hakika ni UOVU kumpachika binti wa watu mimba na kumtelekeza.... Hakuna justification ya hilo zaidi ya kudhihirisha ULIVYO NA ROHO MBAYA YA KINYAMA!!!

Unakitelekeza vipi KIUMBE kisicho na hatia kilichopo tumboni??? Basi leo KIUMBE hicho akijifungua tunza mtoto na YEYE achane naye..
 
Kinachoumiza single mother wanazid watoto wasio na malez ya mama na baba wanazidi

Tatizo wadada wana kimuhemuhe cha kuzaa hovyo pasina utaratibu na hyo ni laana toka kwa mwenyez Mungu mnafanya uzinifu mnapata watoto wanakuwa kizaz cha uzinifu haraka haraka haina baraka

Muwe mnatuliza akil zenu hakuna anae wahi kuzaa wala kuchelewa subira huvuta heri
 
Sio sijanogewa mimi nimekaa kwenye uchumba miaka 4 nilikuwa nacheza na sindano tu hadi jamaa akasema naweza kuwa mgumba ila alivyo nioa tu kitu kikaitika mwisho akaanza lawama kumbe ulikuwa unanifanyia umafia usishike mimba😬😁😁😁
😀😀😀Wew mjanja
 
Pole sana mwaya. I hope utapata wa kukusaidia.

Japo ndo inahitaji utulivu mkubwa mno katika kufanya haya maamuzi ya kumpata wa kukusaidia huku mitandaoni kwani sio wote watakuwa na nia njema.
Hili nalo neno mpendwa
 
Pole sana mwaya. I hope utapata wa kukusaidia.

Japo ndo inahitaji utulivu mkubwa mno katika kufanya haya maamuzi ya kumpata wa kukusaidia huku mitandaoni kwani sio wote watakuwa na nia njema.
Kabisa Inahitaji utulivu sana Huwa nawaza usumbufu wa mimba alafu mwenzio haonekani inaumiza sana
 
Kabisa. Hili ndio la msingi kwenye huu uzi, kashfa,matusi ushauri wa kinafiki wakati mambo yameshaharibika mimi naona ni makelele tu. Kama mtu anaweza kumsaidia kupata hitaji lake na amsaidie tu nina imani kama kuna lolote la kujifunza ameshajifunza tayari
mtu anayekashifu huyo hajielewi bado
 
Mimi nikuhudumie kila kitu ila kwa sharti moja tu.
Mtoto atakuwa wangu, na mawasiliano na huyo bwege yakome
Usije ukajaribu, hawa viumbe hawaaminiki....😊
Tena utashangaa akisha jifungua ataanza kumtafuta mzazi mwenzie kwa speed ya 5G....☺
Ukijiskia kumsaidia wewe fanya kwa utashi wako pasipo masharti yeyote mkuu, kwani hayo masharti ndio utakua mwanzo wa majuto na makwazo makuu juu yako....🙄
 
Unaonekana hujasoma hata mada vizuri. Amesema ameshindwa kuendelea na kazi aliyokuwa akifanya kwa kuwa inamtaka kusimama muda mrefu. Na hata angekuwa amepata hiyo mimba ndani ya ndoa mume akawa kapuku bado angehitaji kazi ya kuendeshea maisha yake. Anyway nahisi wewe ndio mwenye mimba. I rest my case
Usitete Upumbavu hapa mkuu.

Anyway yaishe tu. Na mimi sio mwenye mimba unitake radhi tu siwezi tafuta mke humu ndani.
 
Back
Top Bottom