Nimetembea mikoa mingi Tanzania, moja ya mikoa iliyochoka mbaya basi ni Mara

Ni kweli maeneo mengi ya kanda ya ziwa yana mchango mkubwa kwenye mapato lakini je mapato hayo yanaendeleza sehemu yanakotoka ?

Hayo mapato yote unakuta yanaenda kuendeleza sehemu ambazo zinachangia mapato kidogo sana
Ndio nakuuliza simanjiro, longido, kiteto, handeni, pangani zina utofauti gani na wilaya za Kanda ya ziwa?
 
'Vijana wengi wanaofanikiwa nje ya mkoa hawana utamaduni wa kujenga mkoa wao' Nakazia📌
 
Basi bado hujatembea vizuri na kujua uhalisia wa mkoa mzima
Mwaka wa fedha uliopita, katika halmashauri top 10 zilizoongoza kwa mapato ya ndani 4 ni za Kanda ya ziwa, Hakuna ya Kanda kaskazini iliyoingia
View attachment 3472795
Tarime DC mapato makubwa hivyo na Bado stendi yao ya Tarime ni ovyo kuliko hata ya Musoma mjini aliyoiongelea mleta mada. Pesa wanapeleka wapi hao?
 
Tarime DC mapato makubwa hivyo na Bado stendi yao ya Tarime ni ovyo kuliko hata ya Musoma mjini aliyoiongelea mleta mada. Pesa wanapeleka wapi hao?
Ndio maana hitimisho langu lilikua hizi wilaya iwe kaskazini au kusini au wapi zote zinalingana hali, kote bado
 
Ndio nakuuliza simanjiro, longido, kiteto, handeni, pangani zina utofauti gani na wilaya za Kanda ya ziwa?
tofauti ni kubwa sanaaaa, hizo sehemu zote ulizotaja zimo ndani ya mikoa yenye makao makuu yenye huduma bora kuliko mikoa ya kanda ya ziwa

Mfano mwanafunzi wa Handeni akimaliza form 6 hana haja ya kutoka nje ya mkoa, kuna vyuo vikuu Tanga mjini kama TIA, Utumishi na tayari wameanza kujenga tawi la Mzumbe university.

Mwanafunzi wa Kiteto, Simanjiro, Longido akimaliza form 6 anaweza kwenda babati kuna chuo kikubwa cha uhasibu.

Huko mikoa ya kanda ya ziwa hadi watoke nje ya mkoa waende Dar, Mbeya, Arusha, Moshi, kwasababu hata Mwanza vyuo ni vichache
 
Ni kweli maeneo mengi ya kanda ya ziwa yana mchango mkubwa kwenye mapato lakini je mapato hayo yanaendeleza sehemu yanakotoka ?

Hayo mapato yote unakuta yanaenda kuendeleza sehemu ambazo zinachangia mapato kidogo sana
Ni kweli, mfano mbuga ya serengeti inainufaisha arusha kuliko serengeti yenyewe, hadi inafika mahali watu wanadhani serengeti ipo arusha, mtalii anayeenda kutembea serengeti analipia kila kitu arusha, na mwisho wa safari anarudi arusha kula bata na kuondokea hapo, kilimanjaro pia kama siyo wachagga kushtuka watu wa arusha walishajimilikisha mlima, angalau sasa wameurudisha kwao kwa sehemu kubwa.
 
Tz yote ni ya kidwazi tu hata hiyo Dar mnayoisifia imejaa vichochoro na mitaro ya maji taka. Bora hata mikoani nature.inatia moyo
 
Tz yote ni ya kidwazi tu hata hiyo Dar mnayoisifia imejaa vichochoro na mitaro ya maji taka. Bora hata mikoani nature.inatia moyo
Kweli, hapa ni kijijini kabisa, imagine
 

Attachments

  • Mamba-Komakundi.jpg
    152.8 KB · Views: 20
  • Rongai-Rombo-1(0).jpg
    92.2 KB · Views: 33
  • Old-Moshi-Kikarara.jpg
    61.7 KB · Views: 18
  • KKKT-Mamba-Kotela-1.jpg
    45.6 KB · Views: 22
  • Makoa-Machame.jpg
    39.4 KB · Views: 30
chuo cha maendeleo ya jamii buhare, musoma cotc hivi vyuo jamaa havijui....musoma huwa napakubali sana hasa mitaa ya kennedy na shabani
 
Sasa kama asilimia,,90 ya mbuga ya Serengeti Iko mara, Kwa nini kiwanja Cha international airport kijingwe Kilimanjaro,kiufupi tu Moja ya makosa ya Nyerere ni kufukarisha Mkoa wa Mara , haya ni matokeo ya poor allocation of resources or nepotism,gate away ya utalii ilitakiwa iwe Mika wa Mara,Kuna ziwa ,wana dhahabu ardhi ya pia , Kilimanjaro vijijini wa Tap water mara ziwa ni km 10 tu hawana maji sio makosa Yao ni serikali .
 
# Akili ndogo huyo ,mkoa wa Mara umekuwa marginalized wame fukukarishwa Kwa kunyimwa kipaumbele ikiwa resources wanazo
 
Arusha na nyie mnajiona mna stand kabisa?
Hivi uko serious kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…