Nimetembea mikoa mingi Tanzania, moja ya mikoa iliyochoka mbaya basi ni Mara

Moshi nitaitafutia wiki niende kuicheki vizuri
mzee moshi hamna kitu kimji kimedumaa hakibadiliki majengo ni yale yale kila siku.bora hata wilaya ya siha ina majengo mapya mengi. Mkoa wa kilimanjaro umedumaa. Asusha ukiondoa jiji na meru wilaya zake zote chovu tofauti na mkoa kama mbeya wilaya zake zote zimechangamka kama mbarali chunya rungwe busokelo na kyela mungu kawapendelea hawa watu. Mkoa mwingine wa hovyo kuliko hata mara ni kagera
 
Moshi nitaitafutia wiki niende kuicheki vizuri
mzee moshi hamna kitu kimji kimedumaa hakibadiliki majengo ni yale yale kila siku.bora hata wilaya ya siha ina majengo mapya mengi. Mkoa wa kilimanjaro umedumaa. Asusha ukiondoa jiji na meru wilaya zake zote chovu tofauti na mkoa kama mbeya wilaya zake zote zimechangamka kama mbarali chunya rungwe busokelo na kyela mungu kawapendelea hawa watu. Mkoa mwingine wa hovyo kuliko hata mara ni kagera
 
Yaleyale tu, nafuu ipo mjini Ila wilayani huko kugumu. Nenda simanjiro, kiteto au mbulu utaelewa
Ulisemalo kweli.. nimekaa moshi mjomba vumbi la pale moshi qmmk ni hatari.. sasa jaman wachaga wavijijini wanataabika jmn mpk huruma naona mimi πŸ˜ͺπŸ˜ͺ CCM waache hii nchi tujaribu wapinzani...
 
Utakuwa umepita kitambo kidogo mkoa wa Mara:
1. Musoma mjini walishabomoa ile stendi yote. Kwa sasa panajengwa nyingine
2. Wilayani Butiama kipo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Nyerere
3. Tohara ya hadharani bila ganzi ni mila ilianzia kwa Nabii Ibrahim. Hii leo hawa wanaoitwa wabantu (wakiwamo wana Mara wengi) chimbuko lao ni early hebrews-Israelites (search google). Makabila mengi tuu waliifanya bila ganzi
4. Udumavu wa mzunguko wa hela Musoma ni kwa vile sio njia panda kuu na hamna viwanda. Kama umeitembea Tanzania utagundua miji yote ambayo sio njia panda kuu au haina viwanda ina tatizo la mzunguko wa hela
 
Naijua Mara na Mtwara.
Nasikitika kusema Mara imepitwa mbali sana na Mtwara.
Hakuna wilaya hata moja ya Mara unaweza kufananisha na Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
Hapo hujafika Mtwara makao Makuu ya Mkoa.
 
Acha porojo wewe, moshi mjini inabadilika taratibu mno, na hiyo inatokana na tabia ya wachagga na wapare kupendelea kujenga kwenye maeneo walipozaliwa kuliko mjini, pale moshi mjini ni market place, watu wanakuja pale asubuhi na jioni wanarudi migombani kulala, hebu tuambie hao wanaotaabika huko kijijini ni kitu gani wamekosa? Maana sehemu kubwa ya kilimanjaro hasa upande wa juu, hawana shida ya maji, barabara,umeme, chakula, hiyo shida unayoisema wewe ni ipi?
 
sasa wewe mwenyewe ukubali moshi hakubadiliki na mimi nimeandika tofauti na ulicho kiandika?
 
Inasikitisha sana kuona raia wa Mara na wilaya zake zote inawalazimu kupita Mwanza/Simiyu-Shinyanga-Nzega-Singida-Manyara ili kuufikia mkoa jirani yao kabisa wa Arusha hali wangekuwa na lami yao kuingia Arusha bila mzunguko usio wa lazima.
 
sasa wewe mwenyewe ukubali moshi hakubadiliki na mimi nimeandika tofauti na ulicho kiandika?
Nasema moshi mjini inabadilika taratibu, wewe unasema ipo vilevile tokea zamani, nimepita huko miezi miwili iliyopita,

Nimeona majengo mengi tu mapya hali inayoonyesha kuwa mkoa umeanza kuchangamka tena,

Hali ya maisha kwa upande wa vijiji hasa vya uchagani ni nafuu sana kulinganisha ni vijiji vingi vya mikoa mingine, bila hata jitihada binafsi za wakazi wa huko nature inawabeba, kule maji watu wameyakuta tu yanatiririka kutokea juu mlimani huko,

Kuna mtu anasema kuna vumbi sana, hali hiyo ipo upande wa chini ambao wenyeji wa ukanda wa juu hupaita porini, sehemu kama kahe huko vumbi ni nyumbani kwao, sehemu ya Mwanga pia, ila kwa sehemu kubwa hasa uchagani pana nafuu sana.
 
wewe umepita mimi nipo hapa na mda huu nipo kwenye noah naenda rombo kisha tarakea kwa walevi wa mapombe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…