Nimetembea mikoa mingi Tanzania, moja ya mikoa iliyochoka mbaya basi ni Mara

Hebu acha kutetea ujinga, stendi ya bweri ile iliyoota majani na madimbwi ya maji ndo unaita stendi bora?

Au bro unaishi Musoma, umezaliwa Musoma na hujawahi kabisa kutoka huko kwenda kutembea maeneo mengine ?

Pale bweri hamna stendi ni kiwanja tu cha wazi kimeitwa stendi
 
Babati ni makao makuu ya manyara lakini haifikii maendeleo ya Manispaa ya Kahama , kwahiyo siyo kweli kwamba inazidi maeneo yote ya kanda ya ziwa ukitoa Mwanza, hata Kahama ipo juu na ina hadhi ya Manispaa lakini Babati bado siyo manispaa.

Lakini naungana na hoja yako kuwa kanda ya ziwa imechoka sana hasa mkoa wa Mara huko Musoma
 
Ustaarabu mbovu wa watu wa Arusha ni upi sasa? Usiiangalie Arusha ya mtandaoni utaona kama ni sehemu ya wahuni, ila ukija kuishi physically hata hao wahuni hutawaona , watu wapo cool sana , na katika watu wanaogopa matatizo hasa ya kisheria ni huku Arusha , asili ya watu wengi wa huku ni wapole hadi uzingue wewe tena uzingue sana
 
Wilaya ya Monduli imeendelea sana kuliko Mara nzima, kuanzia Barabara, mzunguko wa pesa, Taasisi zakielimu, za kidini n.k
 
Kama mbulu hakuna shida basi hata wilaya za Kanda ya ziwa hazina shida
Wilaya ya Mbulu ni wilaya KONGWE kuliko hata Arusha na Moshi lakini KAMWE HAIENDELEI, yaani shule ya Imboru imekuwa gofu na stand ni ndogo na ni vumbi tupu...na usafiri wake ni Toyota land cruiser namba A zote, mkifika wanne au sita inaondoka🤣🤣
 
Inasikitisha sana kuona raia wa Mara na wilaya zake zote inawalazimu kupita Mwanza/Simiyu-Shinyanga-Nzega-Singida-Manyara ili kuufikia mkoa jirani yao kabisa wa Arusha hali wangekuwa na lami yao kuingia Arusha bila mzunguko usio wa lazima.
Kutoka Musoma kwenda Arusha Siyo lazima kupitia Simiyu,mwanza,singida,manyara, kuna njia ya mbugani kupitia Serengeti , ngorongoro unaingia karatu uelekeo Arusha, ila haiwekwi lami kwasababu hawataki kuharibu asili ya hifadhi za wanyama, wanasema barabara kuwa ya vumbi ni adventure pia
 
Hapana Cruiser ya kwenda mbulu haiondoki na watu wanne, zile cruiser akikosekana hata abiria mmoja haiondoki kama abiria mnaharaka labda mchange kuilipia hiyo siti na inabeba watu zaidi ya kumi

Pale mbele wanakaa abiria wawili alafu nyuma siti ziko designed kama mabenchi zipo siti 3 ambayo kila siti wanakaa watu wanne kwahiyo ni 2+4+4+4 inakula abiria 14 na inaenda Cruiser tu kupitia ile njia ya magari kwakua kuna mlima mkali na kosa za kushtukiza bus ndefu hiwezi kupita ila kuna njia ya bus ambayo inazunguka sana ila nauli yake ipo chini kuliko cruiser
 
I visited there March last year, tulibebwa kama 8 pale Babati then next morning tukarudi Babati tukiwa Abiria 6 tu asubuhi
 
Umeishi mikoa 9 kwenye nchi yenye mikoa zaidi ya 25.

Ila umehitimisha kwa kusema , mkoa wa Mara ndio mkoa wenye stendi ya Basi mbovu kuliko zote nchini.

Umewahi kuiona stendi ya Bukoba?
Ukiiringanisha na stendi ya Bweri vip?
 
I visited there March last year, tulibebwa kama 8 pale Babati then next morning tukarudi Babati tukiwa Abiria 6 tu asubuhi
Basi inawezekana hali ya upatikanaji wa abiria ulikua mgumu sana ila mara nyingi huwa hawaondoki hadi zijaze
 
Kapimwe Mkojo. Yaani Mkoa aliotoka GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE uwe mbaya wakati Watu Geniuses kabisa na Shupavu wanatoka huko?
 
Sasa hiyo ya vumbi inachosha sana ndio maana mabasi kama SATCO wanazungukia Singinda.

Kule Morogogo-Iringa lami imepita Mikumi na wanyama tunawapita pembeni tu wakiendelea na maisha. Hata pale Lamadi-Bunda/Musoma lami imepita na wanyama wanakatisha kwenda ziwani kunywa maji Hivyo hata huko Musoma-Arusha ingipigwa lami tu ili kupunguza mzungo kwa wasafiri kati ya Mara na Arusha.
 
ukiangalia wabunge wao wengi ni Darasa la saba, form 4, form 6 na Diploma.
Profesa Muhongo (waziri wa nishati) na Wakili Mkono sio darasa la saba, hata wakili mashuhuri Nimrodi Mkono.
Labda kama unaongelea wilaya ya Musoma Mjini ila kama unamaanisha Mara kama mkoa, Tarime iko poa sana. Ila hata Musoma mjini suala la kijiografia linaifanya kuwa na mzunguko mdogo wa pesa kama ilivyo mikoa mingine ya pembezoni mwa nchi.
 
Wilaya ya Monduli imeendelea sana kuliko Mara nzima, kuanzia Barabara, mzunguko wa pesa, Taasisi zakielimu, za kidini n.k
Wilaya ya tarime tu uchumi wake ni zaidi ya arusha+kilimanjaro.
 
Kichwa pumbu povu limekutoka utadhani uko kwenye madhabahu...
Hakuna imani ya wazungu wala waarabu imeongelewa hapa
Hii ndio stendi yenu ya bweri?
Nakuona unapuyanga na kibaragashia hapo na shati ya ngazingazi....


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…