Nimetembea mikoa mingi Tanzania nimegundua kuwa Dodoma kuna nyoka wengi hatari kuliko mikoa yote Tanzania

Umefika Morogoro?
 
 
Niliwahi kuumwa na joka kubwa saizi ya mkono wangu Wilayani Rombo kijiji cha Kirokomu mashambani, kama unakaribia Kiraeni, bahati nzuri lilinigonga kwenye kiatu. Nilikua huko masomoni form one.
Pole na bahati yako ila huwezi weka kilimanjaro kwenye list ya mikoa yenye nyoka wakali.....Tabora, Kigoma, Shinyanga, Nachingwea huko, Dodoma, Singida, Morogoro na Tanga na list goes on lakini Tabora na Kigoma ndiyo baba zao.
 
Alichokisema mtoa mada hajakosea dodoma wapo nyoka wenye sumu kali na wakubwa nyoka ana rangi rangi kila mahali......

Tabora kuna nge, kenge, mamba, bila kusahau nyoka wakali kabisa, kwenye vichuguu, mibuyu, mashamba ya bangi koboko wanapenda sana kula bangi.....

Kanda ya kati yote kuna nyoka nenda singida apo Itigi mapori uone balaa la koboko.
 
Pole na bahati yako ila huwezi weka kilimanjaro kwenye list ya mikoa yenye nyoka wakali.....Tabora, Kigoma, Shinyanga, Nachingwea huko, Dodoma, Singida, Morogoro na Tanga na list goes on lakini Tabora na Kigoma ndiyo baba zao.
Nakubaliana na wewe 100%
 
Bado haujafika Tabora
 
Ndiyo mkuu wapo

Siha kuna sehemu ukitoka Ngarenairobi, ukifika Roseline. Kuna camp inaitwa Endarakwai.

Hapo kuna nyoka kibao. Ila si wengi sana. Kuna mpaka chatu. Ila si wale nyoka hatari.
Majina ya maeneo siyajui sana tulifata karoti kule, katika kutembea tembea kidogo kwenye majani marefu nlikanyaga nyoka mkubwa aiseee nlitoka nduki nimefika sehemu plain miguu inatetemeka siamini kama nipo salama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…