Nimetembelea shule inayoitwa 'Indian School Dar es Salaam'. Nimegundua wahindi wametuzidi akili sana

Kibongo bongo huu mtaala haufai hata kulia ugali kifupi ni mtaala wa kikoloni hauna tija yoyote kwa mwanafunzi unazalisha maboya tu

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Kwa kufanya hivyo ndo wametuzidi sana akili?
 
Je, wasafisha vyoo yaani matopasi nao ni wahindi?
 
Hata ukienda UK wahindi ambao ni raia wa tz ni wengi kuliko watz weusi, jamaa kwa hapa bongo wametuzidi uchumi
 
HAIWEZEKANI
 
Na hawaachi culture yao hata kama kazaliwa nchi nyingine
 
Kuwa na akili inaweza kuwa na maana nyingi kutegemea na kona(angle) unayotaka kukaa.

Kwa nini sisiwe sisi kukubali wao kuwa na shule kama hiyo kwenye arhi yetu isiwe ndio akili?
 
Mitanzania ni mijinga tuuu huo ndio ukweli halisi
 
Kuweka shule yao ndani ya nchi ambayo sio yao ni kipimo cha akili. Je Tanzania tuna shule yeyote nje ya Tanzania inayopelekewa mitihani ya necta?
Kwanza lazima kue na uihitaji huo.

Jiulize maswali yafuatayo Kisha ulejee kwenye swali lako hapo ju.

1:Ni wa Tanzania wa ngapi wako India?
2:Je wameenda huko kwa sababu zipi?

3:Je wanaweza kuendesha Shule huko India ,au kwingineko nje ya mipaka yetu?
 
Shule ikiwa ya Wahindi watupu inazushiwa ubaguzi lakini ikiwa waswahili watupu hatusemi ubaguzi
Wabongo hatujui maana ya ubaguzi, tunapinga ubaguzi wakujaguliwa, ila kubagua nisawa TU.
 
Ukweli India imetuzidi kila kitu ndiyo maana wakaamua wajenge shule inayofuata mtaala wao.kama sisi tungekuwa tuna mtaala mzuri hats wao wasingehangaika kuanzisha shule kama hizo.wagonjwa wengi wa tz ambao madaktari wa kibongo hushindwa kutibu huwapa rufaa kwenda India.operation kubwa kubwa zinazofanyika Muhimbili lazima utawakuta wanashilikiana na wahindi.kama unapesa ya kutosha peleka mwanao akasome shule za aina hizo.kiongozi gani mkubwa tz ambaye mwanae anasoma.shule ya serikali?jibu Hamna maana wanajua huu mtaala wetu ni majanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…