Nimetembelea shule za Dar es Salaam wanafunzi bado wanakaa chini mchangani, sijui mikoani kukoje!

Huyo mleta Mada atakuwa mwalimu wa upe Sasa mikowani inakujaje hapo kwaiyo dar sio mkoa nini tuanzie hapo ndo tuje kwenye madawati na sakafu
 
Huyo mleta Mada atakuwa mwalimu wa upe Sasa mikowani inakujaje hapo kwaiyo dar sio mkoa nini tuanzie hapo ndo tuje kwenye madawati na sakafu
Walimu wa UPE wote walishastaafu. Mwisho wa kuajiri walimu wa UPE ilikua 82/83. Hakuna MTU aliyeajiriwa 83 ambaye bado Yuko kazini.
Turudi kwenye mazingira magumu wanayosomea watoto wetu. Sema tu hatuna uwezo. Hata sisi wapiga kura tunapenda watoto wetu wakalie madawati Kama sisi enzi zetu.
Hela wanazoewa wakuu wa shule kwa ajili ya maendeleo ya shule zinafanyiwa auditing au ndio kula kwa urefu wa kamba?
 
Kama Dar hali iko hivi unategemea huko mikoani hali itakuwaje?
 
Kama Dar hali iko hivi unategemea huko mikoani hali itakuwaje?
Watu waliozaliwa Dar na kukulia Dar bila kutembea sehemu zingine wanchukulia mikoa mingine kama ni mbuga za wanyama.

Hali kama hiyo ingekua Moshi ndio ulipaswa ujiulize sasa kama hali ni hii Moshi ,je Dar ,mwanza nk itakuaje
 
Si kuna shule 2 hapo na ile SM Mbezi zote zipo eneo moja
 
Duh ulisoma hapo sio mkuu au?,nimepajua hapo kutokana na kijiwe changu fulani cha mojo moto moja baridi kilikiwa kinatazamana na hizo schools
 
Kwa sasa kipaumbele ni magari mapya ya serikali ya 2023...
 
Duh ulisoma hapo sio mkuu au?,nimepajua hapo kutokana na kijiwe changu fulani cha mojo moto moja baridi kilikiwa kinatazamana na hizo schools
Huyu atakuwa ni mwalimu was hiyo shule anatamani kuwa mchepuko was mwalimu mkuu
 
Huyu atakuwa ni mwalimu was hiyo shule anatamani kuwa mchepuko was mwalimu mkuu
Mimi nimesoma pale enzi za mwl Wakili halafu wanangu wanasoma pale Wana Ni keep up todate ndio maana napajua vizuri, isitoshe makazi yangu sio mbali na hapo.
Ni sisi ambao wanetu wanasoma pale ndio tunaumia. Wewe Kama mwanao anasoma English medium mshukuru Mungu na uache dharau.
 
Sasa si uende manispaa?hapa umeleta issue ya watoto kukaa chini au mchepuko wa boss?
 
Sasa si uende manispaa?hapa umeleta issue ya watoto kukaa chini au mchepuko wa boss?
Kama wahusika watajirekebisha, hakuna haja ya kwenda manispaa. Kama hawata jirekebisha wazazi tutaleta data, tarehe na picha.
Wazazi tuko tayari kuchangia ujenzi wa madarasa na madawati Kama kutakua na uadilifu katika matumizi ili wanetu wapate elimu Bora. Sio tuchange watu wakanywe beer.
 
Kuna rais aliponda matumizi ya Contraceptives pia akahimiza watu wazaane mpaka mayai tumboni yaishe na akiahidi atatoa huduma zote bure huku Waziri wa Afya naye akikazia kwa kupiga makofi na meno nje nje... imekuwaje leo twashangaa population yetu?
Ndiyo hayupo tena ndiyo madhara ya kutegemea mtu na sasa hivi nchi imefunguliwa wanyama wana kodishiwa ndege ya kuwapeleka Omani na Dubai, uku watoto wetu wana kaa chini
 
Hiyo sehemu mkuu wa wilaya yupo mbunge yupo mea yupo serikali ya mitaa wapo,hawana habari sababu watoto wao wanasoma shule za matajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…