Nimethibitisha jamii inayoongea Kiingereza ina uelewa mkubwa na IQ za juu kulinganisha na waongeaji wa Kiswahili

Nenda huko kwenye prukushani mwenyeweee. Tuachie tuijenge tanzania kwa uzalendo na mshikamano. Kwakuwa huna cha kupoteza ndiomaana unabwabwaja tuuu.
Wewe unajenga upande huu, at the same time viongozi wako wanabomoa upande mwingine, utafanyaje? Utaendelea kujenga? Ama utahakikisha kwanza kuwa kile unachokijenga hakibomolewi? FYI wakati wewe unatungiwa sheria za kukukamua wanasiasa wanapanga kuagiza land cruiser 400 za kuwatembeza popote wanapotaka kwenda, wanajilipa mishahara ya kufuru,wanajengeana majumba ya kufuru,wanapeana posho zisizo na sababu,wamekuwekea na sheria ya kuwalipa wake au waume zao ambao wapo majumbani tu wame relax,bima za maisha,afya,na mali zao unawalipia wewe, wao hawawajibiki kulipa kodi yoyote, wala kupanda au kushuka kwa gharama za maisha hakuwahusu wao, yaani wao ni kula, kunywa,kuongea kidogo, na kusafiri popote kwa gharama zako, huoni uchungu wewe?? Basi wewe ni mtu wa ajabu kabisa.
 
China wanazungumza kiingereza,? Japan wanazungumza kiingereza? South Korea wanazungumza kiingereza? Russia wanazungumza kiingereza? North Korea wanazungumza kiingereza? Malaysia wanazungumza kiingereza? Singapore wanazungumza kiingereza? Matafaifa yapo mengi yasiyozungumza kiingereza na yemeendelea vizuri sana, Lugha sio kikwazo , Maendeleo ni Mfumo uliopo #
Hayo mataifa yako Africa??? Ndo upumbavu wa watanzania reasoning zao ni za kifala kweli kweli, huyu huenda ni graduate kabisa
 
Ooh kumbe but they speak English right? Sasa kama English imetumika kama kigezo cha kujitambua na ukombozi kifikra kwanini wanakuwa na ukabila?Kwanini English isiwe unifying tool huko Nigeria na Uganda?
Kwani kuna mahali kwenye uzi mleta uzi amezungumzia English kama unifying tool?? Hiyo Uganda yenyewe theluthi mbili tu ya raia ndio wanajua English, kuna mamilioni wanajua lugha zao za kikabila tu.
 
Sasa usilalamike endelea kusifia wakenya Hilo tu ndo mnaweza watanganyika.
SIyo Tanganyika tu, dunia nzima inawasifu wakenya kwa ujasiri waliouonyesha, kasoro bibi na babu zangu wasiojua chochote zaidi ya neno Amani.
 
Ndo Tatizo letu sisi Watanzania, yani watu tunazungumza mambo mahimu, wanaanza kukukosoa kwamba hoo sio mbongo.
Kama mimi Tayari wanaanza kujiambia mimi mkenya , duuu
Hiyo ni heshima kubwa kabisa wamekupa mkuu, you are extraordinary.
 
Hayo mataifa yako Africa??? Ndo upumbavu wa watanzania reasoning zao ni za kifala kweli kweli, huyu huenda ni graduate kabisa
Mada inazungumzia na kulinganisha mataifa na lugha mbili tu, machawa wanaingiza lugha zisizokuwa kwenye mada ya msingi
 
Kumbe nawewe umeliona, kuna machawa akili zao zijui ziko je?
 
Nchi zote tatu za Afrika Mashariki, Uganda, Kenya na Tanzania zilitawaliwa na mkoloni mmoja kwa wakati mmoja. Waganda na wakenya wao lugha wanayotumia na kuimiliki ni Kiingereza na Tanzania ni waongeaji wazuri wa kiswahili tu, yaani waswahili.

Lugha ina tabia ya kuendana na utamaduni wake. Mfano waingereza na waongeaji wa Kiingereza ni watu wenye utamaduni wa kuwa wazi, wakweli na wathubutu. Waswahili wana tabia ya kuwa waoga, waongo na wanafiki.

Hali inayoendelea Kenya kisiasa na kiuchumi haitofautiani na ya Tanzania. Wizi, ufisadi na rushwa kwa viongozi vimetamalaki katika nchi zote mbili ila kuna tofauti ya jinsi ya kukabiliana nayo.

Wakenya wana uthubutu wa kusema ukweli hadharani, kujitokeza na kuupinga uovu huo. Tanzania tunasifia na kutukuza wezi, mafisadi na wala rushwa huku wengi wakiendelea na maumivu yasiyomithilika.

Hapo ndipo linakuja suala la lugha na utamaduni wake. Upande mmoja ni ukweli, uwazi na uthubutu na huku kwingine ni unafiki, uoga, uongo na ujinga mwingi.
Mungu atusaidie, amina.
Hiyo sio point kama umekaa uingereza utajua ninachosema.
Issue ni genetics za makabira ambayo hawana uoga na wanaweza kuwakabiri viongozi tz tunao tena wa mpakani za hizo nchi
 
Kwani kuna mahali kwenye uzi mleta uzi amezungumzia English kama unifying tool?? Hiyo Uganda yenyewe theluthi mbili tu ya raia ndio wanajua English, kuna mamilioni wanajua lugha zao za kikabila tu.
Kuna tatizo kwenye hoja zako wewe umesema sijui Uganda na Nigeria kuna ukabila and blah! blah!

Nimekuuliza wewe sio mtoa mada nyie si mnasema English speaking communities wanajitambua? Sasa ulipokuwa unazungumzia ukabila unataka mi nielewe nini

Mnaleta hoja kinzani sasa. Mnasema wazungumzaji wa kiingreza wanajitambua ukibanwa kidogo unasema sijui taifa fulani kuna ukabila.Sasa hawa ambao wanajitambua kwa kigezo cha lugha kwanini wakubali ukabila?Hakuna namna mtu atajitambua then tukasikia ni mkabila
 
Kwani kuna mahali kwenye uzi mleta uzi amezungumzia English kama unifying tool?? Hiyo Uganda yenyewe theluthi mbili tu ya raia ndio wanajua English, kuna mamilioni wanajua lugha zao za kikabila tu.
Uganda na Nigeria kama sio ukabila na dini wangekuwa mbali sana, hayo mambo mawili yamewafanya raia kukosa utulivu na ushirikiano kwa muda mrefu.
 
Kichina ni lugha inayozungunzwa na watu bilioni 1.3 idadi karibu sawa na Kingereza, sasa wewe na Kiswahili chako huko Mlimba utawasiliana na nani kwa ukubwa huo wa China??
Muulize Tanzania inazalisha nini katika world market, ili kiswahili kipate umuhimu wowote,.........nchi masikini kama Tanzania ndo ya kulinganisha na China sijui chawa wanamatatizo gani?
 
SIyo Tanganyika tu, dunia nzima inawasifu wakenya kwa ujasiri waliouonyesha, kasoro bibi na babu zangu wasiojua chochote zaidi ya neno Amani.

Na wewe endelea kupiga mapambio ya kusifu maana huwezi kufanya chochote kwako.
 
Wewe unajenga upande huu, at the same time viongozi wako wanabomoa upande mwingine, utafanyaje? Utaendelea kujenga? Ama utahakikisha kwanza kuwa kile unachokijenga hakibomolewi? FYI wakati wewe unatungiwa sheria za kukukamua wanasiasa wanapanga kuagiza land cruiser 400 za kuwatembeza popote wanapotaka kwenda, wanajilipa mishahara ya kufuru,wanajengeana majumba ya kufuru,wanapeana posho zisizo na sababu,wamekuwekea na sheria ya kuwalipa wake au waume zao ambao wapo majumbani tu wame relax,bima za maisha,afya,na mali zao unawalipia wewe, wao hawawajibiki kulipa kodi yoyote, wala kupanda au kushuka kwa gharama za maisha hakuwahusu wao, yaani wao ni kula, kunywa,kuongea kidogo, na kusafiri popote kwa gharama zako, huoni uchungu wewe?? Basi wewe ni mtu wa ajabu kabisa.
Hakuna nchi iliyokamilika kila kitu. Mafisadi na wezi wa mali za uma wataendelea kuwepo hadi kiyama. Ila amani na mshikamano wa raia ni jambo la kuheshimu saaana. Hao wakenya walipofikia wasipojirekebisha watakuja kujutaaa. Ifokiria huo uharibifu wanaoufanyaa, mfano bunge majengo, magari hadi maktaba, sasa hivyo navyo vimefia nini?
 
Singapore wanazungumza kiingereza?
Kingereza na Kichina ni lugha rasmi za Singapore, Yani Wasingapore wanaweza kuwasiliana vizuri na watu takribani billion 3 , sasa wewe na Kiswahili chako unaweza kuwasiliana na watu wangapi??
 
Nchi zote tatu za Afrika Mashariki, Uganda, Kenya na Tanzania zilitawaliwa na mkoloni mmoja kwa wakati mmoja. Waganda na wakenya wao lugha wanayotumia na kuimiliki ni Kiingereza na Tanzania ni waongeaji wazuri wa kiswahili tu, yaani waswahili.

Lugha ina tabia ya kuendana na utamaduni wake. Mfano waingereza na waongeaji wa Kiingereza ni watu wenye utamaduni wa kuwa wazi, wakweli na wathubutu. Waswahili wana tabia ya kuwa waoga, waongo na wanafiki.

Hali inayoendelea Kenya kisiasa na kiuchumi haitofautiani na ya Tanzania. Wizi, ufisadi na rushwa kwa viongozi vimetamalaki katika nchi zote mbili ila kuna tofauti ya jinsi ya kukabiliana nayo.

Wakenya wana uthubutu wa kusema ukweli hadharani, kujitokeza na kuupinga uovu huo. Tanzania tunasifia na kutukuza wezi, mafisadi na wala rushwa huku wengi wakiendelea na maumivu yasiyomithilika.

Hapo ndipo linakuja suala la lugha na utamaduni wake. Upande mmoja ni ukweli, uwazi na uthubutu na huku kwingine ni unafiki, uoga, uongo na ujinga mwingi.
Mungu atusaidie, amina.
Sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom