Nimetishika sana kutokana na kilichonikuta baada ya kujaribu kufanya tahajudi (meditation)

secretarybird

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
23,984
Reaction score
51,055
Wakuu, nimegundua kuwa tahajudi si kitu Cha mchezo. Usiku wa kuamkia Leo nijaribu ku-meditate na kilichotokea usiku kucha ni vituko.

Nilikuwa naota ndoto za ajabu ajabu, nilikuwa naongea mwenyewe hadi wife akawa ananishtua usingizini, n.k.

Kwa hiki kilichonitokea nimesitisha kufanya tahajudi hadi pale nitakapopata mwongozo mzuri wa jinsi ya kufanya hiki kitendo.

Nilikuwa naichukulia poa meditation sasa nimeshaanza kuiogopa.

Mshana Jr
Pascal Mayalla.
 
Hilo ni jambo la kawaida kabisa , kwa mtu unae anza hizo ndoto mbaya na kuona vitu vya ajbu ni mawazo yako , hofu zako na hisia zote haribifu zilizojichimbia kwa miaka mingi ndani ya kichwa chako .

Hivyo ukifanya mediation ukipata utulivu , ukienda kulala hizo hisia haribifu huibuka kwa njia ya ndoto nyingi na zenye kuchanganya zisizo na mpangilio .

Cha kufanya, fanya mediation kila siku asubuhi na jioni wala hauna haja ya kuogopa mawazo yako , kuna siku utaanza kufurahia matokeo ya mediation.
 
Hii nimeichukua.
 
Back
Top Bottom