Nimetoka kuangalia fujo za mwendo kasi, nimenotice kitu muhimu sana

Nimetoka kuangalia fujo za mwendo kasi, nimenotice kitu muhimu sana

Sawa.

Lakini mwananchi akishakubali kuitumia haki hiyo anatakiwa kuheshimiwa na kuachiwa aitumie hiyo anayosema ni haki yake.

Ndiyo demokrasia hiyo.

Peter Madeleka alikuwa CHADEMA.

CHADEMA ikakataa kushiriki uchaguzi.

Peter Madeleka akatoka CHADEMA na kwenda ACT iki atumie haki yake ya kikatiba ya kupigiwa kura.

Peter Madeleka ana haki ya kupigiwa kura bila vurugu, kwa sababu kachagua kushiriki katika uchaguzi.

Hata kama uchaguzi wake ni wa makosa, kidemokrasia ana haki ya kufanya uchaguzi wa makosa.

Msimnyime haki hiyo.
Ni kweli kabisa unachosema kuhusu haki ila haki haijatimia kwa watu wote wenye kuihitaji kivipi?
1. Kanuni ya Usawa (Equality Principle)
Watu wote wanapaswa kutendewa kwa usawa bila kujali rangi, jinsia, dini, hadhi au uwezo.Je wote
Wametendewa hivi wagombea wa chama tawala waliepuka uwepo wa usawa kwenye huu uchaguzi makusudi kabisa je haki ya mpiga kura itatoka wapi?

2. Kanuni ya Uhalali (Legitimacy Principle)

Sheria au uamuzi wowote lazima uwe halali kisheria na ufuate taratibu zilizokubalika.je sheria zote zimefwatwa mpaka kuiona hio haki tumeona ya luhaga mpina na ya samia je mwananchi kwa nini aingie kwenye sanduku la kura kwa madhila haya

3. Kanuni ya Haki ya Asili (Natural Justice)
Kila mtu ana haki ya kusikilizwa (right to be heard).
Hakuna mtu anayeweza kuwa hakimu katika kesi yake mwenyewe (rule against bias).je kwenye chaguzi huu imezingatiwa chadema walidai reforms kwanini hawakusikilizwa ?inakuwaje kwa mwananchi kama wewe ambaye uko nje na huwezi tekeleza haki yako je tutaihesabu au tupotezee?

4. Kanuni ya Uwiano (Proportionality Principle)
Adhabu au hatua zinazochukuliwa lazima ziwe na uwiano na kosa au hali husika.je wanacho pitia tundu lissu ,luhaga mpina na wengineyo walistahili kwenye kanuni ya uwiano inakataa kabisa

5. Kanuni ya Uwazi na Uwajibikaji (Transparency & Accountability)

Mchakato wa kutoa haki lazima uwe wazi na wale wanaotoa maamuzi wawajibike.je kwenye uchaguzi kuna uwazi na uwajibikaji wa kumfanya mwananchi apige kura yake na iesabiwe na kuheshimiwa jibu ni hapana hakuna dalili zote zinaonesha hakuna

6. Kanuni ya Upatikanaji wa Haki (Access to Justice)

Kila mtu awe na nafasi ya kupata huduma za kisheria bila vikwazo visivyo vya lazima.hapa sitapngelea sana sababu zake zinajulikana upatikanaji wa haki umeminywa ni ngumu kuiona

7. Kanuni ya Usawa wa Fursa (Fair Opportunity)
Kila mtu apewe nafasi ya haki ya kutetea maslahi yake bila kubaguliwa.kwanini baadhi wabaguliwe na baadhi waione hiyo haki kwanini viongozi ndo waipate hiyo haki ya usawa ila wananchi wasiipate

Kiongozi kiranga kama utaiongelea haki iongelee kwa hizi kanuni na sio
Upande mmoja wa kiongozi tu hata mwansnchi pia anazo ,mfumo wa uchaguzi pia unazo, kama uchaguzi umekosa misingi hii je bado tuuesabie ni wa haki.....ni bora wote tukose haki iliopinda kuliko tuiseme haki huku haipo ni kiini macho tu
 
Kwan nani kasema maandamano ni ya chadema?..sasa hiv watu washastuka..masuala la uchama yanaturudisha nyuma...wananch ndo wameamua
 
Sasa ule ule utani wa wanaume wa dar..rasmi nataka uzikwe...wamefikisha ujumbe kwa hawa watawala...dhihaka zote ziamie kwa wavuta bangi wa Arusha..ni kanda yangu ila wanachokifanya kwa sasa hata chizi hafanyi...kwel leo hii ndo wana Arusha wakuvalishwa mamiwani ya games kwel?nmesikitika sanaa
 
Kuharibu mali yoyote sio sifa wala tusishabikie hili na pia usitegemee police kutumia nguvu za ziada kwa jambo hili hasa tukielekea uchaguzi, Polisi sio wajinga kujuwa kuna mbinu kuwachokonoa ili wafanye jambo baya watu wapate sababu. Lakini wakijuwa kuwa ni serious basi nakuhakikishia watashughulikiwa.
 
Kuna jambo la msingi kabisa ambalo Linatakiwa lifanyike hili Polisi wafahamu uwezo wao ni mdogo
 
Ni kweli kabisa unachosema kuhusu haki ila haki haijatimia kwa watu wote wenye kuihitaji kivipi?
1. Kanuni ya Usawa (Equality Principle)
Watu wote wanapaswa kutendewa kwa usawa bila kujali rangi, jinsia, dini, hadhi au uwezo.Je wote
Wametendewa hivi wagombea wa chama tawala waliepuka uwepo wa usawa kwenye huu uchaguzi makusudi kabisa je haki ya mpiga kura itatoka wapi?

2. Kanuni ya Uhalali (Legitimacy Principle)

Sheria au uamuzi wowote lazima uwe halali kisheria na ufuate taratibu zilizokubalika.je sheria zote zimefwatwa mpaka kuiona hio haki tumeona ya luhaga mpina na ya samia je mwananchi kwa nini aingie kwenye sanduku la kura kwa madhila haya

3. Kanuni ya Haki ya Asili (Natural Justice)
Kila mtu ana haki ya kusikilizwa (right to be heard).
Hakuna mtu anayeweza kuwa hakimu katika kesi yake mwenyewe (rule against bias).je kwenye chaguzi huu imezingatiwa chadema walidai reforms kwanini hawakusikilizwa ?inakuwaje kwa mwananchi kama wewe ambaye uko nje na huwezi tekeleza haki yako je tutaihesabu au tupotezee?

4. Kanuni ya Uwiano (Proportionality Principle)
Adhabu au hatua zinazochukuliwa lazima ziwe na uwiano na kosa au hali husika.je wanacho pitia tundu lissu ,luhaga mpina na wengineyo walistahili kwenye kanuni ya uwiano inakataa kabisa

5. Kanuni ya Uwazi na Uwajibikaji (Transparency & Accountability)

Mchakato wa kutoa haki lazima uwe wazi na wale wanaotoa maamuzi wawajibike.je kwenye uchaguzi kuna uwazi na uwajibikaji wa kumfanya mwananchi apige kura yake na iesabiwe na kuheshimiwa jibu ni hapana hakuna dalili zote zinaonesha hakuna

6. Kanuni ya Upatikanaji wa Haki (Access to Justice)

Kila mtu awe na nafasi ya kupata huduma za kisheria bila vikwazo visivyo vya lazima.hapa sitapngelea sana sababu zake zinajulikana upatikanaji wa haki umeminywa ni ngumu kuiona

7. Kanuni ya Usawa wa Fursa (Fair Opportunity)
Kila mtu apewe nafasi ya haki ya kutetea maslahi yake bila kubaguliwa.kwanini baadhi wabaguliwe na baadhi waione hiyo haki kwanini viongozi ndo waipate hiyo haki ya usawa ila wananchi wasiipate

Kiongozi kiranga kama utaiongelea haki iongelee kwa hizi kanuni na sio
Upande mmoja wa kiongozi tu hata mwansnchi pia anazo ,mfumo wa uchaguzi pia unazo, kama uchaguzi umekosa misingi hii je bado tuuesabie ni wa haki.....ni bora wote tukose haki iliopinda kuliko tuiseme haki huku haipo ni kiini macho tu

Point zako zinaonesha uchaguzi hauna haki sehemu nyingi, lakini hazi justify kuwanyima wanaotaka kushiriki kwenye uchaguzi haki hiyo ya kushiriki kwenye uchaguzi.

Kwa sababu kuna watu wanaamini licha ya matatizo yote, njia sahihi ya kuyamalizq matatizo ni kushiriki uchaguzi na kunyoosha mfumo kwa kuutumia mfumo huu huu, si kwa kuususia na kuuvuruga uchaguzi.

Ukiwanyima nafasi hiyo utaongeza tatizo. Two wrongs do not make a right.

Yani hutakiwi kusema "Hapa hamna haki sehemu nyingi sana, sasa na mini nawanyang'anya watu haki zaidi hata hii ndogo waliyo nayo".

Haki haijatimia ni kweli, na kwa kweli haki haiwezi kutimia hata siku moja, tunajitahidi tu kuitimiza, lakini na wewe huna haki ya kuwakataza wanaotaka kupiga kura wapige kura.

Ni haki yao kupiga kura bila bugudha, despite matatizo yote yanayoweza kuwapo katika mfumo.

Katika demokrasia unahitaji kuwashawishi watu wasipige kura, si kiwazuia watu wasipige kura.

Ukimnyima mtu haki yake ya kupiga kura, au kupigiwa kura, na wewe utakuwa umevunja hizo kanuni za haki zote ulizozitaja.

Utavunja 1 kwa ku impose unavyoona wewe kwao.

Utavunja 2. kwa ku impose unavyoona wewe kwao

Utavunja 3. kwa kuwaondolea nafasi ya kusikilizwa wanavyotaka.

Utawavunjia 4 kwa kutaka sauti ya upande wako tu isikilizwe.

Utavunja 5 kwa kuwanyima wananchi kuchagua wanachotaka na kuwa responsible kwa kitakachotokea regardless kizuri au kibaya.

Utavunja 6 kwa kuwakosesha haki ya kikatiba.

Utavunja 7 kwa kuwanyima watu fursa ya kupiga kura.

Matatizo yote uliyoyataja yanaweza kuwa addressed bila kuwanyima watu haki yao ya kupiga kura na kusema ama watu wasipige kura ama wapige kura tuendelee na matatizo haya ni false dichotomy fallacu, ni non sequitur fallacy, ni strawman argument fallacy.

Kwa sababu mnaweza kuwaachia watu wapige kura halafu mkaandamana mpaka mkaiangusha serikali kama kweli mna ushawishi.
 
Mimi naona maandamano yafanyike siku nyingine yoyote lakini si siku ya kupiga kura.

Maana hiyo siku kuna watu wengi watataka kutimiza haki yao ya kikatiba kupiga kura kiroho safi tu na kukawa na fujo wanaweza kudhurika.

Haki yako ya kufanya civil disobedience inaishia inapoanzia haki ya mtu mwingine ya kupiga kura.
Hata wanaoandamana wanatimiza haki yao kikatiba..!!
 
Polisi wanaunga mkono hii ishu, hii ni nafasi ya pekee kuondoa wahuni kwenye mfumo, kuna mambo mengi naona yanaenda kutokea kabla ya uchaguzi…series of events ambzo wakikaa vibaya zinaenda kuibua jambo kubwa 29 OCT.

Hamis kigwangala yuko upande wa maandamano, anatoa Codes kijanja jinsi ya kudeal na utawala hiyo siku. Movement ikianza kuwa kubwa, watu wengi wa CCM wataflip, kwasasa wengi wanaangalia upepo.
Kigwa kamwaga codes zote kimkakati, hii inaonyesha hata wana veggies wataandamana..!! Hawako tayari na yanayoendelea kwenye kijumba chao cha kijani kibichi..!!
 
Hata wanaoandamana wanatimiza haki yao kikatiba..!!
Ni kweli.

Lakini haki moja haitakiwi kuvunja haki nyingine.

Ukiwa na haki ya kupanda basi haina maana una haki ya kumkanyaga mtu mwingine aliyepanda basi.

Wewe unaweza kutimiza haki yako ya kupanda basi bila kumkanyaga mtu mwingine mwenye haki ya kupanda basi kama wewe.

Una haki ya kususia uchaguzi na kuandamana lakini huna haki ya kuvuruga uchaguzi na kumkataza mtu mwingine kushiriki uchaguzi kama yeye kaona anataka kutumia haki yake hiyo.

Kwa nini mnataka kulazimisha watu wafanye mnavyotaka nyie?
 
Polisi wa Tanzania hawana utayari na hawatoshi kuzuia maandamano makubwa ya ghafla.
Hizi fujo na maandishi yawezekana yako orchestrated na 'vitengo' ili kuanza kuwabaini taratibu na mapema wahamasishaji wakuu wa wanachowaza kitatokea!!! Na wakisha wabaini kabla ya siku husika wafanye jambo!!! Hii Nawaza!

Pia uharibifu unaoratibiwa wa miundombinu mfano barabara Mtwara Dar na mingine...ni njia nyingine ya kuwezesha kuchomoa hela kwenye "kibubu" chetu. Hii Nawaza pia!

Be wise kipindi hiki....Fanya maamuzi ambayo hayatakuzulu na hayatazulu miundombinu yetu ambayo inatusaidia wote.

Asanteni kwa kunielewa.
 
Back
Top Bottom