Nimetoka kuangalia fujo za mwendo kasi, nimenotice kitu muhimu sana

Nimetoka kuangalia fujo za mwendo kasi, nimenotice kitu muhimu sana

Haki moja inaishia haki nyingine inapoanzia.

Wanaoandamana wana haki ya civil disobedience, lakini haki hiyo ikianza kuingilia haki ya wengine kupiga na kupigiwa kura kunakuwa na conflict.

Ku resolve hiyo conflict maandamano yasifanyike siku ya kupiga kura.
Mimi mwana CCM lakini ccm kutekwa na kikundi cha wahuni hapana alafu wenye mamlaka ya mwisho na nchi ni wananchi so watakokua wengi ndo watashinda ccm wamekua na dharau sana kwa wananchi sio ccm wote kile kikundi cha wahuni unaona walivyo mwambia Maxmellody Mkurugenzi wa jamii foraham zile ni dharau kwa wananchi kwamba watapiga kelele wiki mbili watanyamaza acha wananchi waamue nini kwenye nchi yao ule mwavuli wa aman ya kulinda viongozi na mali zao umepitwa na wakati CCM. Wanaogopa badaliko ni wale walioshiba wananyonyaji lakini maskini haogopi mabadiliko by JK Nyerere
 
Kama unataka kuandamana, uwe imara, jiandae mana sio rahisi kama tunavyodhani, ni kujidhatiti kweli kweli kwa lolote, Zanzibar kwenye uchaguzi hata mkitembea watatu barabarani hilo ni Tatizo
 
Nina support sana maandamano.
Shida kwa upande wangu japo tunaishi mkoani, baba yangu ni polisi na ni mtu mwema tu, huku watu wengi wanampenda kwa sababu ni rafiki wa kila mtu
Lakini maandamano huku si rahisi kutokea, maandamano yanaweza kuzidi Dar halafu wakamu allocate huko mzee wangu aje kusaidia, na watu hawamjui hata watamchukulia tu kama polisi wengine
Wanaweza kumuua, hii kitu inanipa hofu sana, sipo tayari kupoteza mzazi kabisa. Napata shida nisupport maandamano au nisi support. Niko njia panda, sijui kipi sahihi
Siyo kila polisi mbaya lakn wapo wabaya kweli ww acha mageuzi yafanyeki kama baba yako ni mtu wa haki na huku kwenu watu wanampenda atakuwa salama tu
 
Unakubali kwamba watu wengine ambao wanaweza kuwa na mawazo tofauti na wewe na wao pia wana haki?

Au wewe tu na watu wanaofikiri kama wewe ndio mna haki?
Kila mtu anahaki lakn watu wengi tukiomba haki zetu atupewi .mfano maandamano ni haki ya kikatiba lakn atupewi lakn hao ccm kila kitu wanaruhusiwa kwa sababu wao wapo kwenye dola.


Jambo la msingi hapo ni siku hiyo kila mtu ambanie haki yake tu .wew ukiona busara kupiga kura kapige .
Mm nikiona ni haki yangu kuandamana nita andamana
 
Sawa.

Lakini mwananchi akishakubali kuitumia haki hiyo anatakiwa kuheshimiwa na kuachiwa aitumie hiyo anayosema ni haki yake.

Ndiyo demokrasia hiyo.

Peter Madeleka alikuwa CHADEMA.

CHADEMA ikakataa kushiriki uchaguzi.

Peter Madeleka akatoka CHADEMA na kwenda ACT iki atumie haki yake ya kikatiba ya kupigiwa kura.

Peter Madeleka ana haki ya kupigiwa kura bila vurugu, kwa sababu kachagua kushiriki katika uchaguzi.

Hata kama uchaguzi wake ni wa makosa, kidemokrasia ana haki ya kufanya uchaguzi wa makosa.

Msimnyime haki hiyo.
Hao wanaoenda kupiga kura Ili kubariki uongozi wa utekaji na uuaji wa sisi watanzania sio watanzania hivyo hawana haki ya kupiga kura watanzania tupo barabarani siku hiyo
 
Kumbe hujamsikia Samia; au ulipuuza kwa vile yeye kila jambo analizungumzia kama mipasho!

Mipango ili8iyopo ni kwa Balozi wa nyumba 10 mitaani; awakusanye watu wake wote awapeleke kwenye vituo vya kupigia kura.
Kwa hiyo, siku hiyo ya October 29 tazamia kutembelewa na kukusanywa na Balozi wa eneo lenu; halafu mtaswagwa kwenda kituoni kupiga kura.

Sasa mimi hapa kwangu nafikiria; huyu mtumwa wa Samia hata hatujuani. Siku hiyo kweli atakuja nyumbani kwangu na kunihimiza nikatumiwe kuinajisi nchi hii?
Sijui kama atakuja na polisi na mtutu wa bunduki. Kitu watakacho pambana nacho mbele yao kabla ya kuwafikia waliomo nyumbani kwangu ni Geti la chuma. Mimi sitakuwa nyumbani siku hiyo, nitakuwa na waTanzania wenzangu huko vituoni au barabarani kuhakikisha hakuna kura itakayopigwa kwenye kituo chetu cha kupigia kura.
Maelekezo ya kutofungua geti nimekwisha yatoa kwa wahusika. Wakitaka kuvunja hilo geti; hiyo ni hiari yao.
Kwa itojeshe kusema kwamba balozi siku iyo anaweza kunilazimisha nikapige kura 😂😂😂. Sema aje amejipanga kweli kwa maana atakuwa yupo kwangu na mm ndio nina mamlaka napo
 
Nimetoka kuangalia fujo za mwendo kasi, nimenotice kitu muhimu sana.

Polisi wa Tanzania hawana utayari na hawatoshi kuzuia maandamano makubwa ya ghafla.

Sasa swali langu la msingi sana, ikitokea hawa Wananchi wakaamua kufanya fujo vituo vingi vya kupigia kura, ofisi za serikali kadri iwezekanavyo, italeta implication gani kwenye uchaguzi na maandamano?

Mada iko mezani kila mmoja aijidili kimkakati sana, aseme faida na hasara ya maoni yake.
Mbona waongea kinadharia zaidi. Hebu wakusanye wenzio kwanza mjaribu hicho unachofikiria. Ingieni field mtapata majibu kisha ndo mrudi hapa kuandika uhalisia
 
Namba ya Polisi ni ndogo mno ukilinganisha na idadi ya wananchi hapa nchini.
ikitokea kwamba wananchi wamesala kabisa
askari mmoja atapigwa na wananchi zaidi ya 100
fikiria huyo askari atakuwa na hali gani.
wananchi wana mawe, mipini ya jembe, panga, visu, sime, mikuki, majambia, n.k
Kwa mgawanyo mia ni wachache sana
 
Mbona waongea kinadharia zaidi. Hebu wakusanye wenzio kwanza mjaribu hicho unachofikiria. Ingieni field mtapata majibu kisha ndo mrudi hapa kuandika uhalisia
Mbona waongea kinadharia zaidi. Hebu wakusanye wenzio kwanza mjaribu hicho unachofikiria. Ingieni field mtapata majibu kisha ndo mrudi hapa kuandika uhalisia
Jana tumefanya na hamna boya alietugusa polisi waoga sana wanaishia kupiga virisasi vyao yaani mwaka 2025 unamtisha mtu kumuua wamechelewa sana na inakula kwao
 
Pemba tu, eneo dogo lenye watu wachache, polisi walijazwa hasa huko, lakini baada ya kuwaua baadhi ya wanachama wa CUF, wananchi walichachamaa na kuua afisa wa polisi. Na vita ikaishia hapo.

Nguvu ya polisi ipo pale wananchi wanapowaheshimu kama mamlaka ya kutunza usalama na sheria, lakini wananchi wakifikia uamuzi kuwa polisi ni adui zao, polisi hawana uwezo kabisa wa kupambana na wananchi.
 
Write your reply...jamaa kavunjika mguu kwenye fujo za jana pia ana nundu kisogoni yupo hapa zahanati ya msewe na mke wake analia tu hela hana jamaa winga kkoo
 
Mimi naona maandamano yafanyike siku nyingine yoyote lakini si siku ya kupiga kura.

Maana hiyo siku kuna watu wengi watataka kutimiza haki yao ya kikatiba kupiga kura kiroho safi tu na kukawa na fujo wanaweza kudhurika.

Haki yako ya kufanya civil disobedience inaishia inapoanzia haki ya mtu mwingine ya kupiga kura.
Huo uchaguzi wenyewe usha nyima watu wengine haki zao
 
Hao jamaa nawapa big up ila ili ujumbe ufike vizuri ilibidi gari zichomwe moto hizo.
Kuharibu kitu kinachokusaidia mwenyewe ni ujinga uliyotukuka. Haya Serikali imeleta gari mpya hebu fikiria ungechanganya na zile zilizoharibiwa kama zisingeharibiwq jumla ungekuwa umepunguza tatizo kwa asilimia ngap?
 
Wananchi wagombee magari uchwara ya mwendokasi huku wao na watoto wao wanamejaza maBentley kwenye yards zao. Ndani ya Mwendokasi watu wamejazanaaa, bado hayafiki on time vituoni. Hovyo hovyo tu. Hela zote za kodi za hao wananchi wanagawana. Yani Samia amejua kutuonyesha rangi zake halisi.
Kabisa ,inatia hasira ,yaani Rozirozi moja ya "Dully" unanunua basi za mwendo kasi 50 ,ukijumlisha Rozirozi aliyehongwa "DG-EYE-S" na pia Rozirozi ya rafiki yake "Dully" ,unapata jumla ya basi za mwendokasi 150 ambazo zingemaliza tatizo la usafiri kimara.

Hawa jamaa wanahondomola mali za TAIFA huku wananchi wakiteseka kwa kukosa usafiri ,afya ovyo ,maji ivyo ,barabara tu dar nyingi vumbie ila ameenda kujenga lami mbweni kote ambapo wamejenga mighorofa halafu hawakai wameweka shambaboyz tu wao wanakaa masaki/oyesrebay.
 
Back
Top Bottom