Nimeuza kiwanja changu milioni 10, nataka ninunue bodaboda 3. Hii biashara mnaionaje?

Nadhani tofauti kubwa ya Muuza mahindi na mwenye bodaboda ni kuwq mwenye hiyo bodboda anapata hiyo hela pasipo kufanya kazi. Ila mwenye mahindi lazima akafanye kazi ndio apate hiyo hela. Wewe unaweza ukawa na shughuli nyingine unaifanya hiyo inakiwa ziada.
 
Kwa maelezo Yako, hii pesa 10,000,000 akiweka UTT inaweza kumpa faida ya shs 100,000 Kila mwezi. Baada ya miezi 15 atakuwa na faida ya shs 1,500,000+10,000,000(Mtaji).
Hii inafaa kama una mishemishe zingine za kipato. Hapo ni kama umehifadhi fedha Yako wakati unasubiria kitu Cha kuifanyia.
 
Wewe ni kichaa kbs nina kuhakikshia hiyo hela unaenda kuipoteza wabongo hawa huwez wapa mali yako halafu ukae geto wakutafutie ksha wakuletee pesa utalia kinyawawa tafuta biashara ambayo utaifanya mwnyw battle to battle acha uvivu mkuu nenda kapambane mwnyw ungekuwa uku nlipo ningekushauri na kukupa kampani ununue pool table tu hukosi 15 mpk 20 per day bei ya pool table ni mil 2 tu au tungeingia ubia unikabidhi pool within a year hunidai hata mia mbovu kaz kwako tatzo watu mnadhan pesa ipo dsm tu huku mikoan vitu vdogo vdogo watu wanaingza sn hela per day mfano uku ukajenga banda zuri ukaweka pool table, tv watu waangalie ligi ya bongo humohumo, vinywaji humohumo, bonanza, pemben weka chips nina kuhakikshia within a year ww ni mtu mwngne. KUNA JAMAA YNG YE ANAFANYA BIASHARA YA MAYAI YA KUCHEMSHA ANA MADOGO 3 AMBAO PER DAY WANAUZA MAYAI 40 KILA KCHWA MAANA YAKE 120 KILA MAYAI 40 YAKIISHA FAIDA NI 6500 PGA MARA 3, MISHAHARA YAO NI ELFU 30 TU KWA MWEZI pata pcha sasa.
 
Bodaboda itakula kwako mapema kabla misa ya kwanza na ukifanya masihara utapata kesi kuua mwendesha bodaboda wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…