Nimevunja kibubu muda huu, siamini nilichokikuta ndani

Labda vibubu navyo vina makato yake.
 
Hongera sana brother. Kwa taarifa yako,kibubu sahihi kabisa ni "akili" yako. Uwe na nidhamu ya kweli katika matumizi ya fedha tu!!.
.
.
That's all
 
Tumia Tigo kibubu
 
Hapa nimekaa kwenye sakafu nafikiria na usiku huu plus baridi hili natamani niende nikachukue kitimoto lost ya hii hela yote iliyobaki niondoe mikosi!
Hapo sijaelewa, why 23,000 tu mbona umeweka zaidi ya hiyo?
 
Bila
Tupia walau picha ya kibubu mkuu.

Pole sana
 
Hapo sijaelewa, why 23,000 tu mbona umeweka zaidi ya hiyo?
Mambo ya chuma ulete mkuu, yaani hapa natamani nikamletee vurugu yule muuza vibubu hata kwa maneno tu nimzingue.
 
Nini?haiwezekani
 
Humo ndani unaishi na nani, aweza kuwa ndo chuma.

Benk makato, kibubu chumaulete, mtu ajilie hela yake kesho ina Mungu.
 
Hii pia ilikuwa inanitokea sana, nilipokuwa mdogo nilikuwa na shughuli nyingi za kunipatia pesa, Na nilikuwa napata pesa sana, nilitengeneza kibubu cha kuweka pesa nikawa natunza kila ninavyopata, Ajabu ninapokuja kufungua nikakuta kiasi kidogo sana, kumbe kaka yangu ambaye tulikuwa tunalala pamoja amezipitia.
 
wasalimie hapo utt
 
Aisee pole sana niliwahi sikia hii mambo kumbe vibubu sio poa
 
Humo ndani unaishi na nani, aweza kuwa ndo chuma.

Benk makato, kibubu chumaulete, mtu ajilie hela yake kesho ina Mungu.
Ndani nairhi mwenyewe tu mkuu, na tangu ninunue hajaingia yeyote ndani kwangu.
 
Ndicho kilichomtokea mleta mada.

Au inawezekana hata alikuwa 'anajiibia mwenyewe akilewa' [emoji41][emoji23][emoji1787][emoji1787]...

Lkn wabongo na imani za kichawi unawatenganishaje..?!
 
Wakuu kama kuna mtu haamini hii kitu, anunue kibubu (huenda vibubu vingine havina chuma ulete, sielewi katika hili) aweke hata buku kila siku (kwa walau siku kumi)
And then avunje aje atupe mrejesho!
Hakuna chuma ulete,kama hujui kusave kwa kudunduliza,utaishia kutafuta excuses ili ujitengenezee unafuu..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Mimi naweka vibubu huu mwaka wa tatu na hamna shida kabisa
Watu wengi wanapenda kutoa visingizio kwenye kushindwa kwao.

Chuma ulete ni excuse inayopendwa na watu wazembe walioshindwa kudhibiti mahesabu/matumizi ya pesa... au wafanyakazi wezi wanaoibia mabosi wao kwenye sehemu za biashara walizoaminiwa kuzisimamia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…