Nimevunja kibubu muda huu, siamini nilichokikuta ndani

kipindi niko form two kuna mtoto wa mjomba alikua anatunza pesa zake kwenye kibubu, nilikua nazichomoa kwa kutumia spoko, mpaka nilinunua simu ya samsung kisirisiri, siku anapasua kibubu akauta elfu kumi na sita tu, akaenda kwa mganga cha ajabu mganga akamtaja mtu mwingine mi hakunitaja😀😀😀 waganga ni wachonganishi nyie
 
Mkuu bora uishie hapo hapo, mimi yamenikuta na wala siyo mzembe au hayo uliyotaja hapo
 
Hadithi tamu. Ila imatoka kabla ya mda wake. Ingetoka kesho ingependeza.
 
Saa nyingine hakuna Cha chuma ulete Wala wauza vibubu ,,Kama unakaa na watu nihaohao wanakuuibia mkuu,,hela za noti kuiba kwenye kibubu nirahisi mno,,mm naeka Ela kwenye kibubu miaka na miaka siku nikifulia nachukua mkasi navuta noti😅😅😅au kisu navuta noti...hivo Kama unakaa na watu wachunguze usikute wamekuibia na siku ingine kwenye kibubu dumbujiza kipande Cha mkaa
 
 
Yaani kwa kifupi tu; HAKUNA CHUMA ULETE!!
 
Tarehe 4. 7,000/=
Tarehe 5. 12,000/=
Tarehe 6. 10,000/=
Tarehe 7 nikaweka chenchi chenchi kama za elfu 3.
Tarehe 8 nikaweka 20,000/

Leo Jumatano ni tar 8 September, hii thread imeandikwa jana tar 7 September.

Ila naona tarehe 8 ambayo ilikuwa haijafika nayo umeweka.

Ufafanuzi tafadhali.
 
ahahaha stuka tunza hela kwenye kibubu cha mzungu
 
Kibubu hackers wamekudukua
 
Ahaaa kumbe ndiyo nyie! Nakumbuka tulivokua wadogo na mdogo angu huyo alipita na hela yangu kwenye kibubu tena ilikua 150! Nililiaa aisee sitosahau afu akabisha siyo yeye maana kibubu kilikua kimefungwa vilevile kama hakijaguswa😂
🤣🤣🤣Poleni sana ndugu zangu... Nadhani ni wakati wa kutusamehe ili tisipatwe na mikosi
 
Madelu atakuwa kaweka chip ya tozo hadi kwenye vibubu
 
Hapo kwa ada ndo uliharibu. Hebu mtafute umuombe msamaha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…