Bwana bwana na Mimi leo nitoe yangu kidogo;
Ilikuwa mwaka 2019 nimemaliza chuo kikuu nje ya nchi nikatinga Tanzania. Nilikuwa na kimtaji kiasi kwa hiyo wakati nasaka ajira nilikuwa napiga biashara biashara bila uzoefu wowote, mara papu mtaji ukaisha baada ya kama mwaka hivi na ajira hakuna hata matumaini japo nilipiga Hadi level ya masters degree.
Sasa bwana nikawa nimeamua tu kuoa maana umri nao ulikuwa unaota mabawa. Wakati naona kuna rafiki yangu niliyesoma naye kutoka Ireland akawa amenitumia kama 2M hivi lakini kama unavyojua maswala ya kwenda ukweni, kununua hiki na kile n.k hii pesa nayo ilifika wakati ikaisha japo nilijaribu kununua mpunga wa 1M na bahati mbaya hata haukupanda bei hata buku.
Kizungumkuti kikaja wakati wife ana ujauzito kama miezi 7 kwenda 8, ndani nina 100K tu bado kodi, msosi, na mazagazaga mengine. Basi bwana nikaona hapa njia ni moja tu.
Asubuhi moja nikachukua 50K wife nikampatia 50K nikamuaga nikamwambia kuna mchongo nimepata sehemu naenda. Nikapanda lori kigumukigumu toka Dar hadi Mwanza kisha nikaingia Sirari. Kwanini Sirari? Niliona mchongo niliokuwa nao kichwani kama nikifanyia Dar au Mwanza itakuwa issue sana kwani mara kibao nilikuwa nakutana na washikaji nilipiga nao shule na chuo hapa Tz kabla sijapata mchongo wa scholarship.
Haya sasa nimeingia Sirari kule naamini kabisa kukutana na mtu anayenijua ukizingatia mkoa naotokea ni nadra sana. Nimefika kule nikiwa na 10K, namshukuru dereva wa Lori niliongea naye kiutu-uzima akanifikisha Mwanza tokea Dar kwa 30K.
Kufika Sirari nikalala guest ya 4K nikala 1K nikawa na balance ya 5K, hapo nimeshamwomba dogo langu ambaye yuko chuo walau kiasi kidogo lakini naye anazingua sana japo nilimsupport sana wakati nipo Europe.
Imefika asubuhi kazi yenyewe nilikuwa nawaza “KUSUKUMA TOROLI” dadeq. Bahati nzuri mimi huwa nina bahati ya kuwahi kuaminiwa na watu kwa hiyo kuna jamaa niliongea naye vema akakubali nikae kwake kwa siku kadhaa wakati najipanga. Mungu ambariki sana. Bwana bwana baada kama ya siku tatu huyu jamaa akanikopesha pesa nikanunua toroli nikaingia barabarani. A masters degree holder from a well recognized and highly respected university in the United Kingdom. Unaweza dhania ni hadithi lakini trust me nilifikia hatua hii.
Sasa kizungumkuti kikawa ni kupata wateja, kila mtu akiwa na mzigo anawaita wengine ambao tumepack matoroli pamoja, pengine nadhani kwa kuniangalia walijua vema ningeweza kuwa charge zaidi hivyo waliangalia wale wenye hali ya chini sana kimwonekano. Kazi ikawa ngumu sana. Wife 50K imeisha, bado mwezi mmoja ajifungue, huku hata nauli ya kurudi Dar sina.
Kama baada ya siku mbili hivi nikawa napiga stori na jamaa hivi naye Mungu ambariki. Nikamshirikisha wakati nilionao. Jamaa bwana akanipa wazo na akaniunganisha na mtu mwingine. Wazo lenyewe sasa, kwa kuwa nina passport ni rahisi kuingia Kenya kutokea Sirari. Kule inabidi nifuate MIRAA au mchicha kama hii kitu wanavoiita. Haki ya Mungu kwa wakati ule niliona kama NEEMA ya Mungu. Kesho yake nikajiandaa mapema mapema jamaa akanipatia cash ya Kenya safari ikaanza bwana. Mimi ilikuwa kwamba nahakikisha mzigo unafika Sirari. Mimi nikamuuga jamaa yangu aliyenipokea japo sikumwambia kama nafuata miraa Kenya badala yake nilimwambia naenda kupakia mzigo kwenye gari kule na kushusha tena Sirari kwa hiyo nitapata pesa.
Aliyesema Mungu si Athumani alikuwa sahihi bwana. Mzigo nikafikisha na nikapata kama 200K hivi. Mara 2nd round mara 3rd. Nikawa na kama 500K ikabidi nitume 400K kwa ajili ya maandalizi yote ya kujifungua wife ikiwa ni pamoja na kumsafirisha bimkubwa kutoka bush ili aende kusaidia kwani ndo ilikuwa uzao wa kwanza.
Mungu anisamehe hii kazi nilipiga karibu mwezi mzima na nusu nikapata pesa nzuri na kuja Dar kwa ajili ya kuwa na wife wakati anajifungua. Kweli nimefika ndani ya week akajifungua na ndani ya week hiyo hiyo nikapata mchongo halali na hadi sasa nimeajiriwa na maisha yanaenda poa sana.
HUU NI USHUHUDA TU SIYO USHAURI.
Aquila non capit muscas!