Nimpeleke mtoto shule ya milioni 1.5 au hela nimuwekezee UTT au hisa?

Mkuu Ugumu wa Maisha usifanye mjifiche kwenye kichaka cha kuwa rudisha watoto nyuma.

Pambaneni wamalize msingi EMS
You are talking about yourself wewe ndo kwako maisha ni magumu
 
For Average Person Mwenye Mzunguko wa not more than 2M kwa Mwezi

Panga hivi elimu ya Mwanao

1. Nursery & Primary Government
2. Secondary Private Tena nzuri za kikatoliki(NB Hapa ndo pana shule 50% ya watoto huko kayumba wanachemka)
3. Advance Government
4. Chuo mlipie Ada

Sielewei ni kwann mzazi anapambana kumsomesha mwanae kwa gharama la kwanza mpaka la 7 private, Halafu ashindwe kulipa Ada ya 1.3M kwa mwaka chuo.

Mwishowe unamwachia mwanao na deni la mil30 maskini
 
Nawe jitahidi mwanao ajitafutie mtaji. Kazi yako ni kumpa elimu tu. Zamani watu walikuwa wanakufa wakifikia miaka 50, hivyo urithi ulikuwa na maana. Siku hizi mpaka unamuona kitukuu. Hivyo unachuma ili zikufae uzeeni ukiwa 90+ la sivyo ukivigawa ati unatoa urithi, Watoto watakudedisha mapema
Afu mnakaa na kuanza sema wahindi wezi
 
Wakuu kuna mtoto wangu kaanza shule mwaka huu, chekechea ada yake ni milioni 1.5 ukijumlisha na vikorokoro vingine inaweza fika jumla milioni 1.7

Sio muumini sana wa hizi shule, ila mama yake ndio aling'ang'ania sana tumpeleke huko baada ya kuona rafiki zake nao wamepeleka watoto wao shule za private na wanaongea kiingereza kingi wakiwa na umri mdogo na pia anasema mtoto tukimpeleka shule za serikali atateseka6

Sasa nimefikiria, kumpeleka mtoto hadi amalize shule ya msingi, then sekondari, je hizo pesa za ada badala ya kumlipia shule ya private nikamhamishia serikalini ambako hata hivyo atakua ananuliwa vitabu na materials nyingine , halafu hiyo ada ya private nikawa naiwekeza kwenye mfuko wa UTT au kununua hisa za kampuni inayofanya vizuri tu kila mwaka, au kuiwekeza kwenyw kununua ardhi

Baaadae mtoto akiwa na miaka 20 ama 25 huko atakuwa na mtaji wa kuanzia maisha halafu connection nitampa mimi kwenye biashara zangu

Pia nimefikiria kumpeleka mtoto shule za kawaida kutamjenga awe 'mgumu' awe na kuweza kumudu mazingira halisi ya mtaano baada ya kumaliza masomo, kuliko mazingira ya kupelekwa na kurudishwa na school bus ambayo hayamjengi

Mimi mwenyewe ni msomi mwenye degree, lakini kazi ninyoifanya haihusiani kabisa na elimu yangu, na ilinibidi ni adapt mtaani japo kwa maumivu na hofu yangu ni kuwa mwanangu naweza kumsomesha kwa gharama kubwa halafu elimu isimsaidie kwenye maisha kama mimi, na akawa hana hata skills za kutoboa mtaani, mimi kutokusoma hizo shule za gharama naamimi kumenisaidia kidogo

Dunia inabadilika, wasomi wengi mtaani kazi hakuna na mbaya zaidi kazi nyingi zitaenda kuwa automated miaka ijayo,
Mnunulire ardhi kwa wingi wahenga walisema mali utaipata shambani
 
Experience and real world.....hivi kusoma kwa shida na karaha ndio experience nzuri ya maisha?? Watanzania kwa nini tunautukuza umasikini kama ni sifa?? Unasema unamuandaa aje kufanya biashara kama zako yet unamuandaa kwenye mazingira magumu serious??
Ndio mazingira magumu hutoa watu wagumu, lakini mazingira laini huzalisha vilaza wengi wasiojitambua.
 
yaani 1.5 ni ghali kwa mtoto ninaye mpenda??, Kama mdogo angu nime lipa 3m

mwanangu nita mfanyia nini, hahaha .
Kulipa hio 1.5 au 3 sio issue, issue nikua unakuta unalipa ada zote hizo lakini mtoto ukimlinganisha na watoto wa Kayumba unakuta wanazidiwa uwezo wa kufikili katika mazingira halisi.
 
yuko vizuri, kingine ninacho fanya ni kumpa udhamini wa mazingira Bora.

hiyo hoja ya kuzidiana Akili, bado maana wote Wana kariri tu.
wachache Kwa umri huo, Wana fikiri hoja
 
Elimu sio ghali bana ni namna ya ku manipulate watu watoe hela kwa wajanja wachache,mbona maarifa yapo free hata YouTube unaweza unakomaa tu ukajua how to invest/trade stocks market na ukawa successful.
Gharama ilipo ni wewe kujitoa kuisaka elimu,mie nimesoma nimemaliza bachelor ya Engineering sijatumia hata 1M from std wani mpaka chuo, na nimesoma na nje pia Russia na udsm coet , yaani sijatumia milioni na pia nimesoma boarding miaka sita nimetoka na divisheni wani pote ,nimesoma tabora boys and ilboru.
Nje huko nasoma kwa hela za Russia and Tanzania, mie sijaona hizo Gharama mie ishu ilikuwa kusoma na kufaulu tu mbona. Watu wanakuza elimu bana kuwa ni gharama hakuna cha gharama sema ni Ile ya binadamu ya kutaka kutukuzwa kuwa yeye yu mjanja aka ego inamu drive Ila hakuna kitu.watu wanasoma online wanapata degree zao. Yaani ukiwa na hamu Kali yaani Ile kiu ya kutaka kusoma unasoma bana mbona.
Vilaza ni wengi mkuu, hawawezi kukuelewa, mtu anajitambua anajitambua tu haijalishi kasomea mazingira gani. Hata ukiangalia viongozi wengi wa sasa na watu wenye uwezo mzuri wa kufikili wengi wao wamesoma government. Sema wanachokosa wengi wao ni maadili yakutokupenda rushwa na ufisadi.
 
Wakuu kuna mtoto wangu kaanza shule mwaka huu, chekechea ada yake ni milioni 1.5 ukijumlisha na vikorokoro vingine inaweza fika jumla milioni 1.7

Sio muumini sana wa hizi shule, ila mama yake ndio aling'ang'ania sana tumpeleke huko baada ya kuona rafiki zake nao wamepeleka watoto wao shule za private na wanaongea kiingereza kingi wakiwa na umri mdogo na pia anasema mtoto tukimpeleka shule za serikali atateseka6

Sasa nimefikiria, kumpeleka mtoto hadi amalize shule ya msingi, then sekondari, je hizo pesa za ada badala ya kumlipia shule ya private nikamhamishia serikalini ambako hata hivyo atakua ananuliwa vitabu na materials nyingine , halafu hiyo ada ya private nikawa naiwekeza kwenye mfuko wa UTT au kununua hisa za kampuni inayofanya vizuri tu kila mwaka, au kuiwekeza kwenyw kununua ardhi

Baaadae mtoto akiwa na miaka 20 ama 25 huko atakuwa na mtaji wa kuanzia maisha halafu connection nitampa mimi kwenye biashara zangu

Pia nimefikiria kumpeleka mtoto shule za kawaida kutamjenga awe 'mgumu' awe na kuweza kumudu mazingira halisi ya mtaano baada ya kumaliza masomo, kuliko mazingira ya kupelekwa na kurudishwa na school bus ambayo hayamjengi

Mimi mwenyewe ni msomi mwenye degree, lakini kazi ninyoifanya haihusiani kabisa na elimu yangu, na ilinibidi ni adapt mtaani japo kwa maumivu na hofu yangu ni kuwa mwanangu naweza kumsomesha kwa gharama kubwa halafu elimu isimsaidie kwenye maisha kama mimi, na akawa hana hata skills za kutoboa mtaani, mimi kutokusoma hizo shule za gharama naamimi kumenisaidia kidogo

Dunia inabadilika, wasomi wengi mtaani kazi hakuna na mbaya zaidi kazi nyingi zitaenda kuwa automated miaka ijayo,

Shida ya Kuwa na watoto bila Elimu, na Kama una Elimu, basi una Elimika; Mama yake ana akili kuliko wewe, urithi wa mtoto ni Elimu, bora, full stop!
 
yuko vizuri, kingine ninacho fanya ni kumpa udhamini wa mazingira Bora.

hiyo hoja ya kuzidiana Akili, bado maana wote Wana kariri tu.
wachache Kwa umri huo, Wana fikiri hoja
Hoja nayoizungumzia ni utambuzi wa mambo tu madogo madogo. Hata namna yakiitambua akili ya mtoto kua huyu yuko vizuri unamuelewa mapema tu.
 
Duh chekechea analipa ada sawa na mwanafunzi wa chuo au zaidi duh , udaktari ada 1.8M engineer ada 1.7M
 
Shida ya Kuwa na watoto bila Elimu, na Kama una Elimu, basi una Elimika; Mama yake ana akili kuliko wewe, urithi wa mtoto ni Elimu, bora, full stop!
Elimu bora unaipima vipi?. Kama unampeleka mtoto elimu ya michezo au kipaji maalumu kamlipie ela yeyote. Lakini kama ni elimu hii ya BODMAS acha kupoteza pesa zako.
 
Wakuu kuna mtoto wangu kaanza shule mwaka huu, chekechea ada yake ni milioni 1.5 ukijumlisha na vikorokoro vingine inaweza fika jumla milioni 1.7

Sio muumini sana wa hizi shule, ila mama yake ndio aling'ang'ania sana tumpeleke huko baada ya kuona rafiki zake nao wamepeleka watoto wao shule za private na wanaongea kiingereza kingi wakiwa na umri mdogo na pia anasema mtoto tukimpeleka shule za serikali atateseka6

Sasa nimefikiria, kumpeleka mtoto hadi amalize shule ya msingi, then sekondari, je hizo pesa za ada badala ya kumlipia shule ya private nikamhamishia serikalini ambako hata hivyo atakua ananuliwa vitabu na materials nyingine , halafu hiyo ada ya private nikawa naiwekeza kwenye mfuko wa UTT au kununua hisa za kampuni inayofanya vizuri tu kila mwaka, au kuiwekeza kwenyw kununua ardhi

Baaadae mtoto akiwa na miaka 20 ama 25 huko atakuwa na mtaji wa kuanzia maisha halafu connection nitampa mimi kwenye biashara zangu

Pia nimefikiria kumpeleka mtoto shule za kawaida kutamjenga awe 'mgumu' awe na kuweza kumudu mazingira halisi ya mtaano baada ya kumaliza masomo, kuliko mazingira ya kupelekwa na kurudishwa na school bus ambayo hayamjengi

Mimi mwenyewe ni msomi mwenye degree, lakini kazi ninyoifanya haihusiani kabisa na elimu yangu, na ilinibidi ni adapt mtaani japo kwa maumivu na hofu yangu ni kuwa mwanangu naweza kumsomesha kwa gharama kubwa halafu elimu isimsaidie kwenye maisha kama mimi, na akawa hana hata skills za kutoboa mtaani, mimi kutokusoma hizo shule za gharama naamimi kumenisaidia kidogo

Dunia inabadilika, wasomi wengi mtaani kazi hakuna na mbaya zaidi kazi nyingi zitaenda kuwa automated miaka ijayo,
Kwahiyo ada Kila muhula utakuwa unalipa 375000

Mwache mtoto asome hapo hiyo pesa hata usilipo lipa ada itaenda katika mambo mengine
 
Back
Top Bottom